Edo Kumwembe: Viongozi wa Nchi Masikini wanapenda sana ufahari, alichokisema Tarimba si kipaumbele cha Mtanzania

Edo Kumwembe: Viongozi wa Nchi Masikini wanapenda sana ufahari, alichokisema Tarimba si kipaumbele cha Mtanzania

Mchambuzi wa masuala mbalimbali ya Kijamii ikiwemo Michezo na Siasa, Edo Kumwembe kupitia Kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi FM amechambua kauli iliyotolewa na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba ambaye alipendekeza Wabunge wapewe 'plates number' maalumu zitakazowatambulisha barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku.

Tarimba alisema Wakiwa barabarani wapishwe na wafike haraka huko waendako, changamoto zetu wananchi mtazionea wapi kama mnataka kujitenga na sisi wananchi wa kawaida? Kinondoni Oktoba mjitafakari sana.

Kusoma alichokisema Tarimba, bofya hapa - Mbunge Abbas Tarimba apendekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu ili magari yao yatambulike barabarani

Video: Wasafi FM


Tuliwategemea viongozi wa dini katika kupigania haki na usawa katika rasilimali za nchi lakini viongozi wa dini hasa waislam wamekua wabinafsi wasiozingatia hata yale yaliyoandikwa katika vitabu wanavyotuhubiria .

Leo hii kwa mtu asiye muislam katika nchi hii hakuna Shehe anayeaminika tena.

Wakati huu ambapo kila mtu ameona jinsi uchaguzi unavyoharibiwa makusudi kwa sababu ya kutafuta maslahi na kudharau kura za wananchi kwa maneno na matendo ya watawala na Makada wa CCM tulitegemea Mashekhe bila kujali dini ya Rais waseme na kukemea juu ya udanganyifu unaofanywa na Wasimamizi na tume ya uchaguzi . Naamini kabisa kama Mashekhe wangekemea kwa wazi kwa kuzingatia maadili ya uislamu na dini ya kiislam inayoamini katika Haki leo Rais ambaye pia ni muislam angesimama na kukemea matendo ya mauaji ,utekaji ,wizi wa kura na vitisho na hujuma katika kuandikisha wapiga kura . Rais ambaye pia ni muislam angejitathmini na kurejea katika mafundisho ya dini ya kiislam ambayo yanataka kiongozi kuwa mkweli na mtenda haki.

Lakini yanayoendelea ni kama vile mashehe wanasimaa na watawala kuwapa moyo wa kufanya wanachotaka tena bila hofu wakati wanajua wazi kuwa wanasiasa na watawala wengi hawana maadili ya kidini na wanapaswa kufundishwa na kukumbushwa .

Unamkuta Kiongozi wa dini anashabikia uchaguzi kufanyika kwa kusimamiwa na watu wale wale waliovuruga uchaguzi kwa namna ile ile . Sijui wanategemea amani gani katikati ya dhuluma .
Yaani chini ya msaada na hamasa kubwa ya Mashekhe ubwabwa leo hata kumtaka mtu radhi kiuungwana tu ni kosa . Yaani mpinzani hata aling'olewa jicho au akiuawa halafu wakatokea watu hata kama ni wakubwa wakaomba radhi inakua ni kosa la jinai kumuomba mpinani Msamaha . Tena mpinzani mwenye cheo cha juu kabisa kwenye chama chenye wanachama karibu nusu ya watanzania .
Halafu eti hali kama hiyo kuna mashehe wanasimama na watawala wa namna hiyo ?
Na ukiona Kiongozi mkubwa wa Dola amesema jambo hadharani basi ujue ndio msimamo ya Rais . Yaani kama Rais hajawahi kuonyesha roho ya kuguswa na mambo ya dhulma yanayofanywa kwa wananchi mpaka wengine kuuawa na kupotezwa basi ni lazima na walioko chini yake waogope kuonyesha roho ya kufikirika au kuumizwa na matendo hayo .

Yaani ni kama vile Serikali ya CCM wameweka maadhimio ya kuwakomesha wapinzani kwa kutumia nguvu hata kwa kuwamaliza kwa vipigo ,mauaji na utekaji na kupotezwa .

Hili la RPC kuchukizwa na kumtisha na kumkamata Mtu aliyeomba msamaha kwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria vilivyofanywa na ndugu yake limetufumbua macho .

Kama bado wale Mashekhe ubwabwa na wapenda rushwa na zawadi wanaona kwamba wapo sawa basi wajue wanajitengemezea hali mbaya sana baadae katika jamii .

Kwa mfano Siku mungu Samia atakapoondoka kwanye enzi na utukufu wake wenye mwisho halafu akaja mtu mwengine akagusa maslahi yao na kutawala kwa hila na uonevu watashindwa kukemea na wakiomba msaada watu Watawakimbia .

Hakuna dhulma nzuri hata kama imefanywa na mtu wa dini yako bado ni dhulma .

Mwenyezi Mungu katika Torati ya Musa alielekeza kuwa Tumpende Yeye kuliko vitu vyote na tuwapende Jirani zetu kama nafsi zetu wenyewe.

Jirani sio lazima awe wa dini yako wala ndugu yako bali ni mtu yeyote anaweza kuwa ni jirani yako .
Sasa kwa Mashehe waliopo Tanzania leo katika utawala wa CCM unaolalamikiwa kwa kuumiza wapinzani wao ndani na nje ya chama ni aibu kubwa sana kumpenda Rais kuliko Mungu na pia kupenda nafsi zao wenyewe na kuona nafsi za wengine hazina thamani hata wakiuawa basi wauawe tu maana serikali inalinda amani ya nafsi zao.

Sijajua Mtume Mohamad alielekezwa nini kuhusu kuwapenda jirani zetu na kumpenda Mungu .

Lakini Yesu Kristu aliyepewa sifa kubwa katika vitabu vya Biblia na Koroni alifundisha kuwapenda majirani kama nafsi zetu . Na alipoulizwa jirani yetu ni nani alisema kuwa ni mtu yeyote anayekusadia katika shida yako bila kujali dini yake au undugu wake.

Sasa leo hii chini ya serikali ya CCM wafu wengi wameuawa na kupotea wakiwemo mashehe ,Mapadri , wanasiasa ,waumini wa dini zote lakini bado kuna Watu tena viongozi wa dini wakubwa kama Malasusa na Mashekhe wengi hawajakinai kusikia vilio vya watoto yatima na wajane wao wanashirikiana na walioshindwa kukomesha hayo mauaji kwa sababu ya fedha wanazopewa na waliokalia madaraka .

Tanzania tumepata bahati kuwa na watu ndani ya vyama vyote vya siasa kuwa na watu wasiopenda rushwa kama Gwajima na Lisu . Hawa ndio waliosababisha kuona wema na ubaya unajitenga . Waovu wamejidhihirisha na wema wa,ejidhihirisha wakati huu wa Gwajima ndani ya CCM na Lisu ndani ya Chadema .

Ni uamuzi sasa wa CCM kubaki kama chama cha watu waovu kama anavyojisifia Tulia Aksoni au chama cha wapigania kweli kama ahadi ya Chama inavyosema kuwa nitasema kweli daima ,Fitina kwangu ni mwiko ,sitapokea wala kutoa rushwa ,nitatumia elimu yangu kwa faidi ya wote .
Rais Samia ameshindwa kujitenga na wabaya .Ameonekana wazi kuunga mkono matukio yanayotokea ndio maana hakemei maana ameridhika nayo .

Wananchi tunatakiwa tuwachague viongozi wenye Historia inayoeleweka na wanaojipambanua wazi kuchukia maovu katika jamii ikiwemo mauaji ,rushwa ,utekaji,kesi za uongo ,hukumu zisizo za haki ,utesaji na wizi wa kura .
 
  • "Ponjoro" linamaanisha mtu ambaye ni mvivu, asiyefaa, au asiyejituma, lakini maana hii si rasmi.
  • Katika muktadha mwingine, linaweza kuwa tusi au kejeli, kama kusema mtu ni bure au hana msaada wowote.
  • "Yule jamaa ni ponjoro tu, kazi hawezi!"
    (Inaweza kumaanisha: "Yule mtu ni mzembe au hana maana.")
NA GABACHORI NI MTU GANI
 
Nimejaribu kuwaza kwa sauti katika mapendekezo ya Wabunge wawili katika kikao cha mwisho na cha budget cha Bunge letu. Mapendekezo ya Mh Msukuma na Mh Tarimba Abbas katika kipindi hiki yamesababisha niwe na wasiwasi na wabunge wetu. Kwanza inaonekana kama wamejihakikishia wanarudi kwenye bunge lijalo na wala hawana wasiwasi katika uchaguzi ujao kama watapata kura au la...ndiyo maana wanaomba vitu binafsi na siyo kwa ajili ya wapiga kura wao. Katika kipindi hiki kigumu sikutegemea wabunge kuomba vitu kama hivi..wangesubiri wakirudi bungeni ndiyo wapeleke haya mapendekezo yao..otherwise they are selfish..
 
Wakazi wa kinondoni tena manyanya karibu kabisa na ghorofa zake wanakatiza na ndoo za maji kichwani tena ya chumvi mpaka sasa huku huyu mpuuzi anaomba plate number ili akipita watu waseme mbunge yule anapita...
Kwa upumbavu ulivyokithiri Tanzania 🇹🇿 atapatiwa anachokiomba...subiri utaona
Ile mitaa yotevilitakiwa ipigwe mkeka miundo mbinu iboreshwe!
Sasa kituko wamepiga lami Togo Street upande ule wa Togo tower
Lami imeishia nusu,barabara yanyewe imejengwa kihuni tu

Ova
 
Ponjoro inaropoka hayo kwa sababu ana uhakika wa kurudi bungeni Kwa ubunge wa kupewa, kwa uchaguzi huru hii ponjoro haiwezi kurudi bungeni
 
Ponjoro akili yake ya kipuuzi sana...anaendelea kuhara kwa mdomo wake
Yeye amelimbikizia tu huko na kuna mambo mengine wanafanya wanayajuwa wenyewe
Jiwe angekuwepo mitaa yote miundo mbinu ingekuwa vzr
Ila hawa wanaosimamia kunondoni sahv wako kimaslahi yao wenyewe
Edo kaongea maana kakulia kinondoni na anaijuwa vzr

Ova
 
Ponjoro inaropoka hayo kwa sababu ana uhakika wa kurudi bungeni Kwa ubunge wa kupewa, kwa uchaguzi huru hii ponjoro haiwezi kurudi bungeni
Idd azan anamlia timing tu
Ila kinondoni ina mitosis hainaga viongozi imara wengi huwa dili dili tu ona biafra pale wanachokifanya

Ova
 
Mchambuzi wa masuala mbalimbali ya Kijamii ikiwemo Michezo na Siasa, Edo Kumwembe kupitia Kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi FM amechambua kauli iliyotolewa na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba ambaye alipendekeza Wabunge wapewe 'plates number' maalumu zitakazowatambulisha barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku.

Tarimba alisema Wakiwa barabarani wapishwe na wafike haraka huko waendako, changamoto zetu wananchi mtazionea wapi kama mnataka kujitenga na sisi wananchi wa kawaida? Kinondoni Oktoba mjitafakari sana.

Kusoma alichokisema Tarimba, bofya hapa - Mbunge Abbas Tarimba apendekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu ili magari yao yatambulike barabarani

Video: Wasafi FM
 

Attachments

  • cf0ea736521de32f5d65e1a6b7fd56a4_1747824734726.mp4
    579.6 KB
Mi nakubaliana na Talimba,

Wabunge wapewe hizo number plate maalum, lakini wasiishie hapo kwani hao ni watu muhimu mno katika taifa, wapewe pia ulinzi ili tusije kuwazuru pindi tunapochangamana nao, lakini wasiishie hapo TU hata makazi inabidi watengenezewe na makazi Yao maalum wasije kuchangamana na watu maskini.

Lakini wasije kusahau na makaburi Yao pia, kwa ujumla mbunge asiruhusiwe kuchangamana na watanzania maskini wasije kuambukizwa maradhi Bure.
 
Mi nakubaliana na Talimba,

Wabunge wapewe hizo number plate maalum, lakini wasiishie hapo kwani hao ni watu muhimu mno katika taifa, wapewe pia ulinzi ili tusije kuwazuru pindi tunapochangamana nao, lakini wasiishie hapo TU hata makazi inabidi watengenezewe na makazi Yao maalum wasije kuchangamana na watu maskini.

Lakini wasije kusahau na makaburi Yao pia, kwa ujumla mbunge asiruhusiwe kuchangamana na watanzania maskini wasije kuambukizwa maradhi Bure.
Ulimaani Tarimba Abbas mbunge wa Kinondoni maana hakuna mbunge anaitwa Talimba Tanzania. Labda wa Bunge la Kenya.
 
Back
Top Bottom