Edo Kumwembe: Viongozi wa Nchi Masikini wanapenda sana ufahari, alichokisema Tarimba si kipaumbele cha Mtanzania

Hii ni dalili ya kupoteza vipaumbele vya msingi
Wananchi wanahitaji huduma bora na sio maigizo ya mamlaka.
 
Kwani wakipewa plate number zitawaongezea nini na itatupunguzia nini sisi wananchi wa kawaida?
Kwanza unaelewa hata maana neno "mbunge" kweli wewe..?

Mbunge sio mtawala. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi ktk eneo fulani dogo la nchi/taifa ktk mkutano wa Bunge kama walivyokaa kwa sasa huko Dodoma..

Mbunge unatoka miongoni mwa wananchi. Kiuhalisia unatakiwa kuishi maisha ya wananchi. Kama ni daladala, mbunge anapaswa kupanda daladala, aende kwenye soko wanalokwenda wananchi waliomchagua nk...

Ni makosa mbunge kujiweka kwenye nafasi ya "mtawala" kiasi cha kutaka kuishi maisha ya kujitenga na wananchi
 
Wananchi wasipo jifunza ku wa hold accountable hawa wabunge. Watazidi kuwadharau
Shida ni moja... waliiba uchaguzi wengi wakaingia huko.. na hata sasa ndio plan yao, ndio maana unaona wabunge wanaongea hivyo kwakuwa anajua akipitishwa tu na chama, wataiba kura atakuwa mbunge. Haya maoni sio ya mbunge ambaye anategemea kwenda kufanya kampeni ili achaguliwe na wananchi. Wanajua hawako accountable kwako zaidi ya rais, ndio maana viongozi wote unasikia mama mama mama.

Kwenye hili sita acha kumlaumu JPM, ndio aliyeanzisha wizi wa uchaguzi kwa kiwango hiki cha kutisha na kuua maana nzima ya uchaguzi.

Lakini kuna wajinga bado hawaelkewi kwanini No Reforms No Election
 
Kwanza unaelewa hata maana neno "mbunge" kweli wewe..?

Mbunge sio mtawala. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi ktk eneo fulani dogo la nchi/taifa ktk mkutano wa Bunge kama walivyokaa kwa sasa huko Dodoma..

Mbunge unatoka miongoni mwa wananchi. Kiuhalisia unatakiwa kuishi maisha ya wananchi. Kama ni daladala, mbunge anapaswa kupanda daladala, aende kwenye soko wanalokwenda wananchi waliomchagua nk...

Ni makosa mbunge kujiweka kwenye nafasi ya "mtawala" kiasi cha kutaka kuishi maisha ya kujitenga na wananchi
Wewe stress zinakusumbua. Unafikiri Mbunge akiishi maisha yako ndio ugumu wako wa maisha unaisha!? Tafuta hela dogo!
 
Tarimba alisema Wakiwa barabarani wapishwe na wafike haraka huko waendako, changamoto zetu wananchi mtazionea wapi kama mnataka kujitenga na sisi wananchi wa kawaida? Kinondoni Oktoba mjitafakari sana.View attachment 3365448hyo no reform no election niyachadema tuvyama vingn vyote vnashiriki uchaguz so n pointless n waingie wapambane wao ndo waje wabadilishe wanayotaka
 
Nchi zilizoendlea wabunge mawaziri wanaendesha mpk baiskel ye hajaridhka na maisha expensive wanayopata anataka na private number hyo selfshness
 
Mbunge wa Kinondoni, Abasi Tarimba, amependekeza wabunge wawe na namba maalumu za magari (Plate Number) ili kurahisisha utendaji wao wa kazi na kuwatambulisha kirahisi wanapokuwa nje ya maeneo yao ya kazi, hasa kwa kuwa hawawezi kupeperusha bendera nje ya maeneo rasmi ya kibunge.

Tarimba ametoa pendekezo hilo Jumatano Juni 11, 2025, wakati wa mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kanuni za Bunge kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge iliyosomwa na Naibu Spika, Mussa Zungu, suala ambalo limeibua hisia mseto miongoni mwa wananchi.

Mwanahabari Edo Kumwembe ni miongoni mwa waliotoa hisia zao kuhusu mchango wa Tarimba, ambapo ameonesha masikitiko yake kuhusu maoni na mapendekezo ya Mbunge huyo dhidi ya umaskini, changamoto na hali ya kudumaa kwa maendeleo kunakoshuhudiwa kwenye Jimbo la Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi.

"Viongozi wa nchi maskini wanapenda sana ufahari ambao hauna maana yoyote. Nilikuwa naangalia hapa namuona Rais wa Ufaransa na Waziri Mkuu wa Sweden wote wamekuwa wakitumia treni za abiria kwa safari zao na kwenda kazini. Hawa ndio wanaotupa sisi nchi maskini misaada, mambo ya usafiri, plate number kwenye magari hawajali.

Angalia maoni na mahitaji ya Mbunge wa Tanzania, angalua barabara zilizopo, angalia mashimo kwenye barabara za Kinondoni. Unajiuliza kipaumbele ni barabara, plate number au ni yale mashimo?

Tuna shida zetu nyingi, huwezi kutamani nyama kwa nchi maskini wakati hata maharage watoto nyumbani hawapati. Alichosema Tarimba sio Kipaumbele."- Edo Kumwembe, mwanahabari na Mtangazaji wa Wasafi Media.
1749793336339.png

Source:Jambo Tv
 
View attachment 3366500
Source:Jambo Tv
Ovyo kabsa punjolo
 
Eddo Kumwembe huyu mlevi wa kutupwa? Huwa anaingia studio anapepesuka
 
Back
Top Bottom