Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Yote kheri safari njema mzee, kina sisi tutasimama na upinzani mpaka CCM itoke madarakani....Aluta continua.
 
Ama kweli mzee kabanwa kila sehemu,mme wa mwanae leo mwaka wa ngapi sijui yupo Lumande. But why wanatangaza ndani ya kipindi cha msiba wa Taifa?
Mkuu wewe na uelewa wako unasema tuna msiba wa Taifa? Tafadhali!
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
 
Kama jinsi wote tunavyokumbuka mshike mshike kati ya lowasa na Dr slaa kipindi cha 2015 .

Hawa watu walikuwa ni sawa panya na nyau ndani ya nyumba.

Dr slaa alikuwa haungani na cdm kumkaribisha manywele chamani na ndio akachukua uamuzi wa kukaa kando na siasa.

Kwani mzee manywele alikuwa akihusishwa na ma issue ya ki fisadi ambayo hadi leo hayajapatiwa majibu pamoja na mahakama ya mafisadi kufunguliwa.

Sasa leo hii mzee manywele kaamua kumfuata mzee Dr slaa huko huko aliko,hahahaha patamu hapa.


Je kwa kitendo hiki cha mzee manywele kumfuata mzee slaa ccm ,slaa atachukua uamuzi gani?

Kama kweli mzee slaa ni mzalendo ni basi afanye maamuzi magumu yakurudi cdm kwani mbaya wake karudi ccm

Tofauti na hapo wananchi hawatamuelewa kabisa Dr slaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongela mzee wetu umetambua ukweli na umerudi nyumbani, ni heri umeachana nao wazandiki karibu karibu nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…