TANZIA Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

TANZIA Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Taarifa zaidi itatolewa na familia na Serikali. Poleni wote

====


EDWARD NGOYAI LOWASSA AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mtoto wake Fredrick Lowassa amethibitisha

Pia, Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2008 na kuweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzulu.
Pole kwa familia
Tanzania imepoteza kiongozi mahiri
 
Kahama watamkumbuka kwa kuwasaidia kuwapunguzia makali ya maisha hasa katika suala la maji. Kabla ya kupeleka mradi wa Ziwa Victoria, ndoo ya maji ya lita 20, iliuzwa 500/=. Lakini baada ya mradi, ndoo ya lita 20 ikawa inauzwa 20/= enzi hizo.

Hii ndo aina ya viongozi tunaowataka na siyo takataka zinazotuongezea ugumu wa maisha kila uchao kwa kutuwekea kodi na tozo za kipuuzi zisizo na tija wala manufaa kwa nchi, isipokuwa kwa wapigaji (mafisadi) na kikundi cha wahuni wachache.
 
My feeling ni kwamba aliondoka siku nyingi Sana SEMA Protokali za kikubwa ndio.zilichekewesha kumtangaza!!


Nafsi yangu inaniambia yupo mwingine hatangazwi Hadi Hawa kwanza watangazwe ndio huyo atafuata coz yeye ni mkubwa zaidi kuliko Hawa wanaotangulia Sasa hivi!!

Ngoja tuone!!

Kwamba Ndani ya mwezi huu watamtaja na yule mwengine Wa kibarakashea? Ama kweli dunia tunapita.
 
Back
Top Bottom