Mwalimu is the most intelligent Tanzanian hilo ni sahihi na nchi hii ilivyo leo ni akili zake! mf kufanikiwa kuwapumbaza na kuwahangaisha kinoma raia wote kwa miaka yote ya uhai wake na mbio za mwenge zisizo na kichwa wala miguu!! Mwalimu kutumia kifimbo kujiweka tofauti na kuwapa raia sintofahamu kuwa labda ni fimbo ya kichawi! na watu wote bongo walimuogopa kweli hata Mungu akamuweka uwanja wa taifa alipokufa ili kila mmoja amshuhudie kuwa amekwisha wasimuogope tena waogope Mungu! yasemekana mwili wake ulianza kuharibika pale uwanjani!!
Mwalimu alitoa kali kwa kuchonga meno, kubuni kauli mbiu kibao za kuvuruga akili za watu mfano siasa ni kilimo, uhuru ni kazi, chama kushika hatamu ( hatamu ni neno la kiswahili maana yake kamba za kuongozea farasi) , zidumu fikra za mwenyekiti maana yake yeye tu ndo ana akili wengine vilaza, kuchagua wasaidizi vilaza kina Kiwewe, kuandika vitabu vya siasa ya hovyo ya ujamaa iliyodumaza akili na uchumi wa wabongo, kuchukua uhuru kwa akili si nguvu, kuondoa ukabila kupitia sera za elimu kuchagua wanafunzi kutoka mikoa tofauti na kuwachanganya kusoma shule za mikoa tofauti, kuwapangia wafanyakazi vituo vya kazi mikoa mingine, kulinda mipaka yetu na kujenga jeshi imara ili tusivamiwe na yeye asifanyiwe mapinduzi, kuikalia Zenj kiakili, kutumia kiswahili kuunganisha raia, kuua uchifu nk, ila mapungufu yake ni mengi mno!!
kumkosoa Mwalimu si kosa kabisa kitaaluma hata yeye binafsi ndani ya roho yake alijua sababu alisoma ulaya!!ukisoma bongo pekee unakuwa mjinga plus kwenye baadhi ya mambo! mf bongo elimu yote ni kukariri ulaya elimu ni kuelewa, bongo swali moja jibu moja tu la mwalimu, ulaya swali moja majibu mia ya wanafunzi yote majibu sahihi ukiyatetea majibu yako!!
wazee wenye mawazo ya kikoloni na kijinga waliojaa bongo kama Mzee Mtui ndio mashabiki wake si vijana wasomi , bahati mbaya wazee hawa wamebakiza miaka kama 20 tu wote wafe (bi idhinllah) maana miaka yenyewe si mingi ni sabini tu ikizidi themanini kinachofuata ni kurudi mavumbini kwa nyimbo na mapambio! mimi naamini wazee wote wakifa nchi nchi itazaliwa upya kwa kuongozwa na vijana ambao hawakutawaliwa!!nchi itapaa kiuchumi!
Kutokana na kutukuzwa mno na wazee wenzake Mwalimu alijisahau akajaa kiburi na majivuno akatamalaki na kudhani ana shea na Allah akatamka hadharani kuwa ana afya ya kutosha na atamuona Rais wa awamu ya tano! Allah akamtoa uhai bila watu kujua kwa siku kadhaa mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi mkuu, chezea Mungu wewe!!
Mwalimu hakupenda kukosolewa, utamaduni mbaya mno aliowaachia viongozi wetu wajinga kabisa kuwahi kutokea duniani sababu ulaya imeendelea kupitia ukosoaji!! ukosoaji ambao huitwa mawazo mbadala! bongo siku hizi wakosoaji huitwa wachochezi! huwa nikicheka sana ujinga wa mtu mweusi kulazimisha watu kupenda chama chetu sababu by nature hatuwezi kufanana mawazo sababu binadamu ni tofauti kila kitu!! jinsia, elimu, kazi, makazi, wazazi, malezi, umri, dini, kabila, exposure, friends, dreams, goals, income!!
Mwalimu alikuwa mtu mbinafsi sana hakutaka mawazo ya mtu mwingine yamzidi akili, waliompinga walipotezwa wengine kina Kambone walihama nchi! Kuna watu waliochukizwa na sera zake mno hata mmoja akadiriki kumuua hadharani kwa risasi mkuu wa mkoa wa Iringa wakati huo bwana Klerruu muuaji huyo aliitwa Mwamwindi! Mwalimu wetu mkuu aliona watu wote bongo ni vilaza na ni nyumbu, (farasi!)
Mwalimu alikuwa mtu katili mno rohoni bila kuonesha usoni basi buana jamaa alichukia mno matajiri na kusahau ni Mungu ndie hugawa mali basi akawadhulumu watu wasio na hatia mali zao bila huruma akapora watu hasa wahindi na majumba yao na mashule yao waliyojenga kwa majasho yao kupitia sera yake ya dhulma ya utaifishaji akaita Msajili wa Majumba, ule ulikuwa ni wizi! lets call a spade a spade!! kuna sera pia alianzisha ya uhujumu uchumi ambapo ukiacha majizi ya mali ya umma kutupa pesa na mali zao kwa hofu ya kukamatwa kunao watu wengine walitupa pesa zao za halali!!!
Mwalimu alikuwa mdini wa kutupwa na udini unaendelea hadi leo bongo katika ajira serikalini na elimu za juu! ukihesabu wakristo walio katika ajira serikalini ni mara mbili ya dini zingine, sera ya kutumia namba za mitihani ya Kigoma Malima iliokoa jahazi kidogo! Hapa ndipo waislamu huwa hawasemi alale pema peponi bali husema ‘ Mungu amlaze mahali panapomstahili’
Mwalimu alitupotosha kiuchumi na kutuletea umaskini tulionao hadi leo kwa kuanzisha ujamaa ambao yeye mwenyewe hakuuelewa na walio chini yake hawakuuelewa! huwezi kuulewa ujamaa kama unaweka kapuni ubepari vinaenda pamoja! makazi , maisha na shughuli za kiuchumi viliharibika kabisa alipoanzisha vijiji vya ujamaa falsafa iliyofeli sababu nchi ilijaa watu wajinga! kuna watu waliliwa na simba walipohamia kwenye mapori mapya kuanzisha vijiji vya ujamaa!!
Mwalimu alikuwa mjinga mno kutoelewa kuwa ujamaa ni ideology ya kipumbavu na huwezi kuanza nayo kujenga nchi sababu kiutaratibu na kimaumbile binadamu hasa yule maskini ni selfish by nature ukimpa rasilimali za kikundi au nchi bila sheria na shuruti na mabuti na virungu daima ataanza kujaza tumbo lake kisha tumbo la mkewe kisha matumbo ya wanawe kisha ukoo then ndo akumbuke kikundi ( capitalist premise)! ili nchi iendelee lazima ianze ubepari kwanza watu wamiliki njia za uchumi na kulipa kodi kubwa zinazoendeleza nchi, nchi ikiendelea mbali katika ubepari ndo mnarudi kwenye ujamaa sababu ujamaa....... ( hapa si darasani ningefundisha kwenye hili tu najua kuliko mwalimu!)!
Mwalimu alitumia rasilimali za nchi ya bongo kipumbavu tena bila ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni kwa kuanzisha vita zisizokwisha eti kukomboa Afrika nzima lengo yeye na kina Nkrumah ndo wawe viongozi wa Africa nzima, the pride we carry to this day Wabongo kwa sifa! hatujaanza sisi kaanza Mwalimu!! huu ulikuwa ujinga mtupu sababu tuliowakomboa hawatusaidii chochote leo! rasilimali tulizotumia kukomboa mataifa yote tungetumia kujenga nchi!
Mwalimu alipigana vita na Uganda na kuua maelfu ya askari kumrudishia kiti best yake Obote! this was a big disaster kwenye economy!
Mwalimu alijitengenezea umungu mtu na kutaka kuabudiwa na falsafa hiyo mbaya kabisa bado inaishi bongo kwa kuwa viongozi hupiga magoti kuomba kura na wanapopewa dhamana hupiga watu hao mabomu ya machozi, mabuti na virungu! tunalaani sana aina hii ya uongozi!
Nakiri mimi si shabiki wake ila ni shabiki wa Mkulu kindakindaki