Elimu ya Bure kwa Wasafirisha Maiti zinazogoma kwenda Kuzikwa Kwao ili zisikudhuru kwa Ajali mbaya barabarani

Elimu ya Bure kwa Wasafirisha Maiti zinazogoma kwenda Kuzikwa Kwao ili zisikudhuru kwa Ajali mbaya barabarani

sema uliendesha kwa makini tu, shida ni hizi imani haba ni tatizo kwa wanadamu.
Zina nguvu siku ikikufika.
Pana gari kabuku Tanga iligoma kuwaka kaitwa kila fundi hola,siku mbili,akajitokeza mzee mmoja akamwambia dereva Acha utoto njoo,vua nguo zote kaa kwenye siti kanyaga gia uende,dereva kafanya vile na gari ikawaka wakaondoka eneo hilo akaenda valia mbele nguo.
Sayansi bado ni changa Sana kwenye elimu zingine.
 
1. Chukua Jiwe Dogo rusha upande wa mbele lilipo Jeneza Marehemu wako hata kama hakutaka Kusafirishwa Kwao atafika tu na wala hamtadhurika njiani na Gari yenu haitopata Ajali.

2. Chukua Jiwe Kubwa liweke Juu ya Jeneza hapo mnafika nae Kijijini Kwao Salama na wala hamtopata Jambo lolote baya Njiani hasa Ajali.

3. Mkimuingiza Marehemu ndani ya Gari lenu au lile mliloliandaa hakikisheni mnaanza Kuingiza ule upande wa Miguu ( na siyo Kichwa ) na hapo atafika na hakuna ambaye atadhurika au Ajali mbaya kutokea.

Atakayefuatisha hivi nilivyoelekeza hapa na bado Marehemu akakataa kwenda Kwao nakuruhusu Unidai Kiasi chochote kile cha Pesa na nitakupa kama ipo Mfukoni.
Hili neno ni jema. Sasa mkuu; Je, kama umesahau na mkafika mbali njiani ukakumbuka hizo mambo unarekebisha vp au ndo basi tena?
 
We safirisha maiti yako uache kufata haya masharti uote moto wake
Mkuu, kinachowasaidia watu wabishi katika hoja hii ni ile huruma ya watu waliopo au wasindikizaji. Vinginevyo likishawatokea, wangewaambia "Haya endelea na sayansi/ubishi wako hapo au jisaidie mwenyewe shenzi kabisa."
 
Safari ya yeyote ya kusafiririsha marehemu lazima kuweka kipande cha mkaa kwenye usafiri....
 
Wait...

Unasema Marehemu anagoma kuzikwa?

Anagomaje?

Anavyogoma anaweka kizuizi gani kuashiria amegoma?

Anasema sitaki?

Huyo atakuwa amezimia anawa ektia tu
umeongea kisasa sana mwenzio kaandika kimila
 
Waulize wanaosafirisha sio mimi.
Mchawi mama yako
Ukiona mtu anaamini habari hizi za kishirikina ujue na mama yake yuko namna hiyo. Watoto huwa wanajifunza mambo mengi kutoka kwa mama zao. Sasa wewe ulijuaje kuwa maiti zinaweza kugoma kusafirisha?
 
Wazee wengi wamekufa na hawakufundisha vijana wao mila, vijana wanajiona wameelimika sana na wanaita mila ni imani za kishirikina.

Miaka fulani tuliwahi kusafirisha msiba kwenda mkoa fulani, kumbe marehemu alikuwa ametoroka kwao na hakupenda kabisa kurudi huko mkoani kwao. Tulikoswa koswa na ajali nyingi zile za uso kwa uso, pamoja na gari kufa mara nyingi. Baada ya kuwaambia wazee, wakatuambia tuweke jiwe kama mleta uzi alivyosema, baada ya hapo safari ilikuwa nyepesi, hakuna kuharibika kwa gari wala kukoswa koswa na magari.

Kuna mambo mengi sana yamenifanya niamini mtu hafi, ni pumzi tu ndio inakata ila roho inaishi nasi.
 
Ni jambo la kushangaza kidogo kwamba wengi wetu tunaamini (na ndivyo tulivyo fundishwa katika mafundisho ya Imani)kwamba mtu ni Mwili na Roho. Kwa mwili mtu hukimbia, huongea, hukasirika, hupigana, hucheka n.k. n.k. Hilo lipo ni wazi kabisa. Lakini inapokuja hoja ya Roho na mambo yake wengi wetu hukimbilia kusema ni Ushirikina. Tunasahau kwamba kama Mwili unavyoweza kutenda, hata Roho nayo pia huweza kutenda. Sasa kwa kuwa hatujui bayana Roho hutendaje ndio hapo baadhi yetu tunatafuta majibu rahisi kuwa huo ni Ushirikina na kwa ujinga huo tunaendelea kuumia.
 
Back
Top Bottom