Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Mimi naona kama kuna vitu vinachanganywa, kushindwa kuongea kabisa kiingereza hilo ni jambo na kuongea ila sio kwa ufasaha hilo ni jambo lengine.

Shida yetu sisi ni kushindwa kuongea kiingereza kwa ufasaha, kama ingekuwa kusoma masomo kwa kiingereza inatosha kufanya mtu ajue kuongea kiingereza kwa ufasaha basi watanzania tungekuwa tunaongea kiingereza kwa ufasaha ila haipo hivyo.
 
Angeongea Kiswahili kibovu ndipo ingekuwa hoja!

Kwani maprofesa wa Uingereza wanajui Kiswahili!
Nadhani mleta hoja yupo sahihi ni ajabu kwa mtu aliyesoma hadi kuwa profesa halafu hajui english maana ndio lugha yetu ya kufundishia elimu ya juu, sasa huyu mtu alifaulu vipi huko kote na kuandika research huku hajui english?
Lazima hapo kuna kitu hakipo sawa ,alidefend vipi papers zake chuoni ambapo lugha ya kufundishia ni english?
Alifaulu vipi secondary na advance huku lugha kuu ni english? Hapo lazima tuhoji
 
Naambie ni ngazi gani ya elimu TZ, wanafundisha Conversational English??
Hakuna, ni ngeli ya kufanyia mitihani na kumudu uelewa wa elimu ya taaluma, ukiendanelimu ya juu, hata university profs ambao wanaheshimika globally katika taaluma zao hawako vema kwa hiyo conversational English, na hata wazungu wako hivyo, ngeli wanaijua very basic kwa ajili ya ku connect na wengine nje ya lugha yao
Ni colonial mentality kuwa professionals lazima waonyeshe conversational proficiency ya ngeli
 
Tunategemea graduate aweze kukngea english maana ndio major language of comminication kwa level yake tuache kutetea ujinga, dunia siyo kijiji matokeo yake ndio yale ya waziri wetu aliyetoa speech huko nje wote tukawa tunaona aibu na sisi ni english speaking country
 
Mkuu kumbuka shida inayojadiliwa hapa ni kiingereza cha kuongea tu.
 
100%

Ndio maana wengi wanaokomaa na hoja za Kiingereza ni malimbukeni, na hawajawahi kugoka nje ya nchi.

Kwanza Wazungu walivyo *******, hata kama unajua English ukiongea lafudhi yako yanajifanya hayakuelewi.

Hata huko Uingereza watu wana lafudhi zao.
 
Kwahiyo shida ipo wapi mkuu ambayo wewe unaona inatakiwa irekebishwe?
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Anaitwa nani??
Chuo anachofundisha??
 
Mkuu kumbuka shida inayojadiliwa hapa ni kiingereza cha kuongea tu.
Oooh! Kumbe cha kuongea tu? Maprofesa wetu wakifundisha huko madarasani wako sawa wanashusha nondo kwa kimombo safi. Shida inakuja kwenye kuongea tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘

Sikuuelewa mjadala; na najitoa rasmi πŸ™πŸΏ
 
Shida hata hawa wanaokosoa unakuta nao wana tatizo hilo hilo labda iwe wao wamesomea nje ya nchi.
 
Mbona kwetu ni kawaida tu my friend, english sio mother language yetu, tunaisomea tu.
 
Shida hata hawa wanaokosoa unakuta nao wana tatizo hilo hilo labda iwe wao wamesomea nje ya nchi.
Mimi nimeona hili jambo ni kuisoma na kujifunza lugha ukubwani inakua ngumu hasa katika utamkaji Ila na uzembe unachangia Kama janabi na magufuli
 
Kweli Ila kwetu imekuwa gumzo prof anaongea broken
Masomo yao magumu hayo muda wa kuzingatia lugha ataupata wapi masomo yao yapo kwa lugha za masomo yao hakuna past wala present tense kama Course zingine unakuta mwaka wa kwanza mpaka wa pili wapo na Kiingereza mara Soma lingine nalo lina viingereza tu mimi siwezi kushangaa kutokana na aina ya masomo yao watu wa Mechanics nao wapo hili Kundi akijua ni juhudi zake binafsi..
 
Wewe ndio mjinga.
 
Kwahiyo shida ipo wapi mkuu ambayo wewe unaona inatakiwa irekebishwe?
Kama tunatoa graduate ila basic things ambazo tunategemea wawe nazo hawana tuangalie mfumo wetu wa elimu wapi tunakosea, otherwise mawaziri wetu wakifika nje ya nchi hawatotuwakilisha vizuri na hawatotaka tusikie hata wakiongea kwenye hadhara za kimataifa kwa kuogopa aibu, kifupi elimu inayotolewa ni duni ndio maana wenye hela wanapeleka watoto wao nje ya nchi
 
Oooh! Kumbe cha kuongea tu? Maprofesa wetu wakifundisha huko madarasani wako sawa wanashusha nondo kwa kimombo safi. Shida inakuja kwenye kuongea tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘

Sikuuelewa mjadala; na najitoa rasmi πŸ™πŸΏ
Sawa mkuu ila kama unaona kiingereza kinachotumika kwenye kufundishia kinamfany mtu kuweza kuongea kiingereza kwa ufasaha basi tusingekuwa na hii shida.
 
Wewe ndio mjinga.
Sawa we mwerevu! Usharidhika? Ukishiba wanzuki uwe na Adabu kijana, kama babako hajakupeleka shule ukamtukane yeye sio uletee random people matusi kwa shida zako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…