Elon Musk ataka kujenga jiji mwezini, ndoto yake inawezekana?

Oyaa huyo jamaa utajisumbua tuu
Ni hanaga hoja kabisa.. Tena siku hizi ndo amelijua hilo
Binti kwenye ubora wako, mijadala kama hii wewe kuwa msomaji tu, maana imevuka upeo wako wa kufikiri.
 
Huyo jamaa ana hatari sana Kwa anaepinga au kuona kama anaigiza namuonea huruma yeye na uzao wake
 
Binti kwenye ubora wako, mijadala kama hii wewe kuwa msomaji tu, maana imevuka upeo wako wa kufikiri.
Boya nini
Wewe uko chini sana mentally,

Elon nimemfatilia sana,
Wewe umekaa kunakiri vitu sivyo na uelewa navyo unakuja kubishana na wataalam?

Bora umesha jua where you belong.
 
Boya nini
Wewe uko chini sana mentally,

Elon nimemfatilia sana,
Wewe umekaa kunakiri vitu sivyo na uelewa navyo unakuja kubishana na wataalam?

Bora umesha jua where you belong.
Tulia binti, jenga hoja kwa utulivu ueleweke.
 
Anawapiga watu kamba ili stocks zipande apige ela. Ana ahadi nyingi ambazo hazijatekelezeka. Alianza na Mars na alisema kufikia nadhani 2025 binadamua atakuwa ashaweka makazi now naona kaachana napo. Mpaka sasa rocket yake ambayo inapaswa kuwa ndiyo inasaforisha watu na mizigo hazijawa tayari kila test linaibuka tatizo.
Starlink inafanya poa na soace X haitengenezi faida maana mteja mkubwa wa soace X ni Starlink kama ambavyo mteja mkubwa wa cyber truck alikuwa space x.
 
Boya nini
Wewe uko chini sana mentally,

Elon nimemfatilia sana,
Wewe umekaa kunakiri vitu sivyo na uelewa navyo unakuja kubishana na wataalam?

Bora umesha jua where you belong.
Halafu boya ni huyo baba ako unayemuanzishia uzi kila siku, half witted bastard!
 
Halafu boya ni huyo baba ako unayemuanzishia uzi kila siku, half witted bastard!
Utatoa mapovu na kuichachafya bipolar mpaka uchoke.. Issue ni kuwa ulikua na moto sasa umeenda unako belong (dumbness) ... Huna maarifa, huna influence, huna kitu... Yaani unakesha jf bure ni heri urudi kijijini ukaendelee kumsaidia mashamba ng'ombe wewe
 
Sawa binti.
 
Nilitegemea labda ungeniambia gharama za kujenga mji mwezini ni kiasi hiki, na anaweza kuzimudu hivi.

Nilitegema ungeniambia changamoto za kujenga mji mwezini ni hizi, na atazimudu hivi.

Nilitegemea utaniambia gharama hizi za kujenga huo mji mwezini atazirudisha hivi.

Nilitegemea unioneshe necessity ya huo mji, kwa nini unahitajika. Kwamba hii si a white elephant vanity project tu ambayo inajitengenezea tatizo na kulitatua bila ya hilo tati,o kuwapo kiukweli.

Sasa hivi, ukiondoa hoja ya kwamba watu wanahitaji kuwa na sehemu nyingine ya kuishi ili kitu kibaya kikitokea duniani, kikasababisha "extinction level event" ya kuua watu wote duniani, maisha yaendelee huko nje ya dunia, ukiiondoa dhana hiyo, hakuna point ya kujenga mji mwezini. Labda kujenga base ya scientific research, kitu ambacho hakihitaji mji wa watu wa kawaida kuishi.

Idea ya kujenga mji wa watu kuishi mwezini haina mashiko kwa sababu hapa duniani sehemu za kuishi hazijaisha, pia kwa sababu ni gharama sana.

Unapotaja dola bilioni 2.9 katika hesabu za kujenga nyumba mwezini inaonesha hujaelewa gharama zinazohusika hapa, hujaelewa suala la Return on Investment, hujajua gharama za kumsafirisha mtu mmoja tu kutoka duniani mpaka mwezini, achilia mbali kum support huko, kuweka mifumo ya hewa, chakula, kazi, ecosystems zote.

Hujajua changamoto za kisaikolojia, za kukabili radiation. Changamoto za meteorites, changamoto za kukosa hewa. Changamoto za vumbi la glass mwezini. Changamoto za joto na baridi kali. Changamoto za gravity na biology yetu. Changamoto za supply chain.

Unapofananisha suala la magari ya umeme na kujenga mji mwezini nakucheka kwa kuwa huelwi somo la awali kabisa la kulinganisha vigu. Ukitaka kulinganisha vitu, chagua vitu vinavyofanana. Magari ya umeme ya hapa duniani na kujenga mji mwezini ni changamoto mbili tofauti kabisa.

Kama Elon Musk ana uwezo huo, hujauelezea kwa detail hapa.

Umeuelezea kama muumini wa dini anayeamini mambo bila uhakiki.

Bandiko lako linaonesha wewe ni muumini wa Musk zaidi ya mtu anayeangalia data, yani umeanza kwa imani kabla hujajua changamoto zikoje.

Ndiyo maana umeshindwa hata kuzitaja changamoto umeenda moja kwa moja kuonesha una imani na Elon Musk.

Una imani na Elon Musk kwenye kukabili changamoto gani?
 
Hufahamu kwamba Musk ndiye alikuwa risk taker? Mwaka 2008 kampuni ilitaka hadi kufilisika..

Unaelewa kwamba engineer anapoajiriwa mshahara wake analipwa kama kawaida, kampuni iingize faida ama hasara yeye mshahara wake upo pale pale.. na hata kampuni ikifilisika Engineer anaweza kuhamia kampuni nyingine..

Kingine Musk ndiye chief engineer na designer naielewa rocket, hilo hata wahandisi anafanya nao kazi wamethibitisha... uaifikiri ni mtu wa kukaa ofisini na kuhesabu fedha.. jamaa yupo vizuri kwenye rocket science...

Musk anafanya pia maamuzi ya kiufundi... kuna kipindi walitaka kutengeneza Starship kwa carbon fiber Musk akawakataza na kuwaambia watumie chuma cha pua...

Bmw, Ford, General motors n.k kabla ya Tesla kuwa serious na EVs kampuni nyingi za magari waliona gari za umeme hazina faida , kabla ya spaceX kutengeneza rocket zinazorudi duniani zikiwa wima, engineers na watu wengine walisema haitawezekana...
Kumbuka hiko kipindi engineers walikuwepo, wataalamu walikuwepo, alikosekana tu kiongozi mwenye maono ambae anngewekeza kwao na kuwaambia washirikiane kutengeneza gari ya umeme ya kiwango na rocket itakayoweza kutua ikiwa wima...

Bila maono ya Musk, ku take risk hao engineers wangekuwa kampuni zingine wakifanya kazi za kawaida.. Musk ndiye mbeba maono...

Nijifunze swali lako mhandisi mkuu wa injini za rocket kwenye SpaceX, Tom Mueller alisema Musk ana uelewa wa ndani sana kuhusu rockets na jinsi zinavyofanya kazi, Musk huwa anashirikiana na engineers wengine wakifanya mahesabu magumu ya sayansi ya rockets...

Sio engineer mmoja tu aliyeshtushwa na uwezo wa Musk...

Musk anasoma vitabu sana, na ana passion na interest na anachokifanya.. ndio maana imetokea akawa na uelewa mkubwa wa masuala ya rockets...
 
Nikisema unaandika kishabiki unatakiwa uelewe, haya maelezo yote hapa haujajibu kile nilichotaka kufahamu, unazunguka zunguka tu.

Tesla ilianzishwa na nani?
 
Bandiko lako linaonesha wewe ni muumini wa Musk zaidi ya mtu anayeangakia data, yani uneanza kwa imani kabla hujajua changamoto zikoje.
Huu ukweli hataki kuukubali, lakini ndio uhalisia wake, jamaa ni muumini tu wa Musk, anatoa hoja za kishabiki sana kuliko uhalisia wa jambo lenyewe.
 
Wewe ndiye ulipaswa kuuliza hayo maswali, maana hata swali lako lilikuwa general sana...

Dola bilioni 2.9 wanayotoa NASA kwa SpaceX ni kwa ajili ya kutengeneza Starship HLS.. sio kujenga majengo mwezini...

Kuhusu suala la mionzi, vumbi la mwezi na baridi kali mwezini, wanasayansi wamegundua mwezini kuna mapango ya kivolkano ambayo yapo ndani ya ardhi, si juu ya ardhi, hivyo watajenga hio miji huko kwenye mapango kuepuka baridi, mionzi na vumbi huko mwezini..

Mwezini huko watajenga gas station , kwa kutumia barafu iliyopo mwezini watazalisha oxygen na hydrogen ambapo hydrogen itatumika kama fuel kwenye rocket, kwa mwezi kuwa kama gas station ya vifaa vinavyokwenda anga za mbali ama sayari zingine itapunguza gharama za fuel za rockets.. hio tayari ni biashara itakayorudisha pesa ambazo zimewekezwa (ROI)..

Mwezini pia kutafanyika uchimbaji wa nishati safi , watachimba helium 3 ambapo mwezini kuna tani zaidi ya milioni.. duniani helium 3 kwa mwaka mzima inapatikana kilo 10 hadi 20 duniani kote kwa ujumla.. helium 3 ina thamani kubwa.. kwa kuanzisha uchimbaji huo wa helium 3 huko mwezini lazima fedha waliowekewa zitarudi na faida juu(ROI).
Maana gram moja pekee ya helium 3 ni dola karibu 19,000... je huo ni mradi wa hasara? Usiseme tu zaidi ya kutengeneza makaazi mengine ya binadamu huko mwezini hakuna faida nyingine ya maana...

Vingine ulivyouliza hapo naona havina mashiko..
 

Umeona swali general kwa sababu hujaweza kulinyambua tu, pengine kwa sababu unajibu kiimani zaidi ya kwa data.

Unasema vingine havina mashiko wakati swali la muhimu kabisa hujalijibu.

Ukiondoa research, ambayo haihitaji watu wa kawaida kwenda kuishi kwenye mji mwezini, na mambo ya binadamu kuwa multi planetary species, ambayo kwa watu wa kawaida bado ni ndoto za kifalsafa tu, kwa nini watu waende kuishi mwezini kwa gharama kubwa sana wakati dunia bado ina uwezo wa kuhimili watu kuishi kwa gharama ndogo sana?

Hujajibu swali hili.

Na hili ndilo swali la msingi kabisa hata Musk akisema anauza shares za kampuni watu waende kuishi mwezini, investors watauliza hili swali kwanza kabla hata ya details za feasibility ya kuishi huko.

Is there demand? Why would anyone, apart from a few die hard enthusiasts, want to go there?
 
Wabongo huwa mnataka matokeo ya haraka na shortcuts.. huu utamaduni wa kupenda vitu rahisi rahisi ndio maana kuamini mtu anaweza akafanya mambo magumu huwa hatuamini..

Jamii zetu zimetujenga kuamini mambo magumu hayawezekaniki na vyema kutokujisumbua na hapo ndipo wazungu walipotuacha...

Watu wana projects toka miaka ya 1980s mpaka leo hawajakamilisha na wanapambana.. hakuna excuses wala kukata tamaa...

Juzi nasoma mtandaoni naona rockstar games wanaachia GTA VI mwishoni mwa mwaka huu , wametumia miaka 14 kutengeneza video game...

Hio miaka 14 engineers na programmers wanakwenda kazini na wanarudi nyumbani, wanalipwa mshahara , miaka 14, ndipo ujue watu wapo serious...

Mwaka 2000 ungemuambia Mwafrika hasa mbongo kwamba 2026 kutakuwa na AI ambayo itaweza kuwaza kama mtu, itaweza kufanya mambo ya kustaajabisha, itaweza kuimba na hata kupiga story na binadamu, wengi wangesema ni uongo na uzushi, haitawezekana, here we are...

Waliotengeneza AI wangekuwa na akili za hovyo kama zetu , wangekuwa na akili hizi za kupenda vitu rahisi na shortcuts, kuamini haiwezekani.. leo hii AI isingekuwepo.. na mtaendelea kushika mkia mpaka mwisho wa dunia msipobadili fikra..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…