Mkuu, wakati sisi tunaoa, kula, kunya na kuabudu kuna watu wanakaa wanaangalia miaka 100/200 ijayo itakuaje kisha wanakuja na plan ya kuepusha hatari.
Tutawaita majina yooote sijui freemasom, sijui Illuminat sijui kina nani ila mwisho wa siku ni lazima hawa watu wawepo kusaidia maisha yaendelee, otherwise pweza wanaovuliwa ili waliwe na binadamu wataisha, Samaki wataisha, ng'ombe hawatatosha, kuku hawatatosha hata tukibuni mbinu za kuwakuza siku mbili ili wafae kuliwa.
Tutakata miti yote ili tujenge nyumba na magorofa, maisha yatakuwa kwenye hatari ya kupotea.