Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Hahaha!kama kuna sehemu yoyote ya jiji hili aulize tu niko vizuri kulijua nje ndani.
Uko vizuri halafu hujui Maisha club imehama muda mrefu??!!! By kesho pale watakuwa washazungusha mabati kuvunja lile jengo tayari kupandisha tower mpya.
 
Sasa Maisha club nimebugi wapi?unajua shule ya sekondari Oysterbay ilipo?ngoja nikuelekeze utaelewa tu,ukitoka St.Peter kabla mataa ambayo sasa hayapo unanyoosha hiyo barabara kuna hotel jina limenitoka sasa kabla hujafika hicho kilima na kabla ya kituo cha mafuta Puma na ni upande huo huo wa shell ndipo maisha ilipo,kuna watu watasaidia ninachokwambia.
Kaka usiangaike kumwelekeza,huyu anataka umweleleze kupitia hii njia ya msasani(CCBRT) ndo anaonekana kaikariri
 
Haaaaaaaaaaaaaa nilikuwa sipo update bana maana kitambo sana sipo dar,nipo mkoani nakula matunda ya nchi haaa
Haha h sawa kiongozi.. Mwenzako kanibishia hadi mwisho kakimbia...mimi nilikubali kuwa sijui ilipo embassy hotel japo nimefanya kazi hapo bustani karibu na ifm kwa zaidi ya mwaka...
 
Haha h sawa kiongozi.. Mwenzako kanibishia hadi mwisho kakimbia...mimi nilikubali kuwa sijui ilipo embassy hotel japo nimefanya kazi hapo bustani karibu na ifm kwa zaidi ya mwaka...
Mjini kila siku vitu vinachange,nakumbuka tu iliunguaga wakaikarabati upya lakin sikuwa na taarifa kuhusu kuamishiwa makumbusho,...nachojua makumbusho kitambo kulikuwa na mzalendo pub na kila ijumaa kulikuwa na jide pale
 
Kaka kweli mkoani kumenoga.. Mzalendo sasa hivi haipo tena pale kuna jengo linapandishwa pale...
 
Kaka kweli mkoani kumenoga.. Mzalendo sasa hivi haipo tena pale kuna jengo linapandishwa pale...
Duh!!kweli hatare sanaaa,mzalendo palikuwa poa sanaaa na zile kwato style music za yule dj haaaa,so yule dj yupo wapi kwa sasa??na hile restaurant pale chini millinium tower hipo pale au imehama pia???
 
kwa taarifa ni kwamba hoteli nyingi zipo hoi bin taaban kwa sera za sasa za kubana matumizi na utawala wa kibabe
 
Wadau siku ya Tatu sasa napita eneo hili naona mafundi wakichomelea bodi ya gari(Lori).

Ina maana ssasa ni karakana rasmi kwa kazi hiyo!?

Tujuzane jamani!
Hata mimi nimeona kama vile wanataka kuanza ukarabati. Hiyo hoteli iliuzwa wakati wa ubinafsishaji na kama sikosei ni Ndesamburo kupitia Keys Hotel ndiyo walionunua. Baadaye ukazuka mgogoro juu ya madai ya waliokuwa wafanyakazi dhidi ya PSRC au LART wakitaka walipwe stahiki zao ndiyo umiliki uhamishwe. Hapo hapo kulikuwa na wahindi kupitia KJ Motors nao walikuwa wakidai, nadhani nao walikuwa na hisa.
Huenda nayo imo kwenye orodha iliyotoka kwa Msajili wa Hazina ikitaka wale wote walionunua mali za serikali waziendeleze kabla hawajanyang'anywa. Kama nakumbuka Tanzania ilikopeshwa na Ufaransa ili kujenga hoteli hiyo ikiwa chini ya TTB.

Binafsi naamini walionunua hiyo Embassy na Motel Agip (kina Mantheakis) walifanya hivyo ili kuzidhoofisha kwani huyo huyo Mantheakis ndiyo alikuwa anaanzisha Sheraton ambayo kwa sasa ni Serena (baada ya kuwa Royal Palm na kisha Movernpick).
 
Kwanza Uwa Nashangaa Kuona Hiyo Hotel Iko Hivyo Miaka Yote Hii!!!!!!!! Mahotel Mengi Tu Yameuzwa, Lkn Hiyo Inaoza Tu Pale!! SIJUI Ina Shida Gani, NADHANI Kuna Tatizo Pale, Kwani Hata Kubadilisha Matumizi Nako Imekuwa Ngumu!!!??
 
Back
Top Bottom