Embu tuchambue Siasa kidogo kutokana na haya matukio

Embu tuchambue Siasa kidogo kutokana na haya matukio

Matusi yanatoka wapi?

Ndio maana nimesema kwa mtazamo wangu na sio wako nimeongelea kwa upande wangu elewe
Umeandika upumbavu kwani umelazimishwa kumkubali Lissu?, amewahi kukubagua wewe?.
i
 
Sitachangia kwa lisu sababu sijaona hoja yako kama ina mashiko, ila kwa upande wa Gwajima alikua wapi siku zote?

Yes mtu mwenye akili timamu lazima ujiulize hili swali why now? Yeye ndo anamajibu sahihi zaidi, ila ukiangalia matukio ya utekaji kipindi hicho yalikuwepo ila sasa ni mengi zaidi,kipindi hicho tuliaminishwa ni "watu wasiojulikana", ila kwa sasa watekaji wanakuja na magari/uniform zinazodhaniwa na police na wanajitambulisha hivyo,(rejea kwa Ali kibao na Mdude)... Lazima apatikane panya wa kumfunga paka kengele na gwajima kajitolea hilo regardless na hidden motives zake zingine.
 
Gwajima ni mganga njanjaa ambae natafuta pakutibia njaa yake kwanini asiongee kipindi kibao anatekwa au mdudu ndio maana nasema tz hatuna viongozi wapo kwa maslahi yao binafsi
Sitachangia kwa lisu sababu sijaona hoja yako kama ina mashiko, ila kwa upande wa Gwajima alikua wapi siku zote?

Yes mtu mwenye akili timamu lazima ujiulize hili swali why now? Yeye ndo anamajibu sahihi zaidi, ila ukiangalia matukio ya utekaji kipindi hicho yalikuwepo ila sasa ni mengi zaidi,kipindi hicho tuliaminishwa ni "watu wasiojulikana", ila kwa sasa watekaji wanakuja na magari/uniform zinazodhaniwa na police na wanajitambulisha hivyo,(rejea kwa Ali kibao na Mdude)... Lazima apatikane panya wa kumfunga paka kengele na gwajima kajitolea hilo regardless na hidden motives zake zingine.
 
1. Kusema Lissu anatembelea Upepo wa kupigwa Risasi, utakua umeamua kujipotosha.
Kwa nyakati za hivi karibuni sijawahi kumsikia hata akiongelea hilo swala.
Pia hata kama akiamua kuliongela hilo swala ni haki yake na vile waliofanya hivyo hawajawajibishwa ndio inazidi kumpa uhalali wa kulidai hilo.
Lissu kwa sasa anadai mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi, na Katiba kwa ujumla.

2. Askofu Gwajima hayuko serikalini, yeye kwa mujibu wa Katiba ni mwakilishi wa wananchi bungeni.
Ana sehemu mbili za kuongelea moja ni Bungeni, ambapo Spika ameonesha hana nia ya kusikiliza hoja ya utekaji
UWanja wa pili ndio huu ambao ameamua kuutumia.
Halafu kusema kuwa analitumia swala la utekaji kujinufaisha kisiasa, ni kweli na Ndivyo Siasa ilivyo, lakini ni kweli pia Utekaji upo na unapaswa kukemewa.na alichofanya Gwajima ni sahihi kabisa.
 
Gwajima ni mganga njanjaa ambae natafuta pakutibia njaa yake kwanini asiongee kipindi kibao anatekwa au mdudu ndio maana nasema tz hatuna viongozi wapo kwa maslahi yao binafsi
Labda kama umeanza kumfaham geajima juzi ndo utamuita "mganga njaa"... Lakini inawezekana kweli akawa ni "mganga njaa na anatafuta tiba ya njaa yake".... Waambie maboss zako WAACHE KUTEKA WATU NA KUUA DAMU ZISIZO NA HATIA
 
Sipo upande wowote ila nimejaribu kuwaza hivi tu
➡️➡️➡️ Ile kusema tu eti huna upande tayari umeshaonyesha kuwa una upande!
Nafikiri angejikita kwenye kutafuta zaidi mapungufu ya serikali na kuwaweka watu katika umoja hao wanzanzobari na waislamu ndio hao hao anao wategemea kuwaomba wampigie vote
➡️➡️➡️ Mapungufu gani ya serikali ambayo hayajulikani? No Reform, No Election lengo lake ni kurekebisha mfumo wa uchaguzi ili uwe fair hatimaye achukue dola na kushughulikia hayo mapungufu. Mengine yote ni makosa madogo madogo tu ya kiufundi!
Gwajima kipindi hayo yote yanatokea alikuwepo lakini leo hii anakuja mbele za watu na kusema kuwa kwamba serikali ni mbovu means na yeye ni mbovu kwa maana nyingine mimi na mchukulia kama mtu ambaye anataka madaraka ila kwa alivyo ona kwamba mwaka uhu kama yupo nje ya mchezo so anatafuta namna ya kurudi mjengoni so ana amua kutoa siri ila mtu kama huyu ni mbaya sana katika ustawi wa taifa hafai kuwa kiongozi
➡️➡️➡️ Siasa ni sayansi. Ni mchezo wa timing na balancing. Ukikosea hapa tu umekwisha. Kwa Gwajima huu ni wakati sahihi maana ndiyo kuna impact kubwa sababu ya uchaguzi. Ni timing perfect kabisa. Isitoshe Gwajima ana pesa na hategemei hela za ubunge ili kuendesha maisha yake. Angeweza kujikalia zake kimya akajikita kwenye kazi zake za kiroho bila shida yo yote badala ya kuingia katika kazi hii ya hatari ya kutetea wanyonge. Na hakuna timing mbaya kwenye utetezi wa wanyonge. Kwa hili GWAJIMA, pamoja na mapungufu yake yote, apewe tu maua yake
Hawa wawili kwangu naona bado wanapwaya sana na viongozi wa dini ni mara nyingi naona viongozi wa dini wanaitwa ikulu wanaongea na Rais wyh mawazo yao na mitazamo yao wasitoe wakati uho na waende madhabahuni kutoa matamko ili serikali ifwate matamko yao?
➡️➡️➡️ Wakiitwa ikulu unaona serikali ndiyo huwa inafuata mapendekezo yao? Uitwe ikulu ukazungumzie ishu ya utekaji? Wao wameona kuja kutafuta nguvu ya umma ndiyo njia sahihi maana huko kwingine imeshashindikana. Na wako sahihi📌
Kuna vitu vya kujiuliza sana na kuumiza kichwa na kuwaza kwa upana zaidi
Hakuna kitu cha kujiuliza wala kuumiza kichwa sana. Nchi inatafunwa na mafisadi. Maisha ni magumu kupindukia huko mtaani. Mtu asiye na cheo wala madaraka akiinua kichwa kusema ananyamazishwa. Na hawa wanaojitolea maisha yao kuwaamsha nao bado mnawapinga kwa vile tu pengine tu watu kama wewe mnaangukiwa na makombo kutoka meza kuu katika dhifa ya taifa. Ungeni mkono jitihada hizi ili raslimali za nchi hii ziwafikie hata hawa wanyonge wanaoishi kwa dhiki kuu. Watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe vyenu vinategemea juhudi zenu za sasa.

Hitimisho: Mada uliyoianzisha kidogo ni nzito, imekuzidi uwezo na hauna hoja thabiti zilizosimikwa katika ukweli, uhalisia na mategemeo ya jamii. Na ndanimwe kuna chembechembe za uchawa. Pengine tu itakubidi uwekeze nguvu kwenye mada zako za upishi na uachane kabisa na mada hizi zinazohitaji tafakuri jadidi mnyambuliko - haijalishi kama ni haki yako ya kikatiba kuandika cho chote na hata kuwa chawa! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️

20241203_231958 (1).jpg
 
Back
Top Bottom