Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 673
- 865
Mama nasikia ana unasaba na Ali Hassan Mwinyi. Kwa hiyo inaelekea huko ndo anakoazima akili.Kweli, wengi magavana waliopita walikuwa ma Dr. na ma Profesa. Historian inakwenda kujirudia. Mnamo mwaka 1989 wakati Gavana Charles Nyirabu anastaafu, Mhe. Mwinyi alimteua Bwana Gilman Rutihinda, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha,kuwa Gavana wa Benki Kuu.
Nadhani mama anazingatia weledi na uzoefu kwenye sekta husika. Kikubwa ni matokeo. PhD sio issue.
Ila wakati wa AHM ndo sarafu ya Tanzania ilishushwa kutoka Tshs. 100/- kuwa ndo noti kubwa kuliko zote mpaka kufikia Tshs. 10,000/- kuwa ndo noti kubwa kuliko zote.
Kwa hiyo mama tusije tukashangaa akiiporomosha sarafu yetu na kuja kutuacha na manoti yenye sifuri nyingi zaidi.