Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Viongozi wa Klabu ya Yanga SC wamehitimisha kikao chao na serikali kilichofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu kuhusu hatma ya dabi ya Kariakoo.
Baada ya kikao, Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said, aliwahakikishia wanachama kuwa uongozi wa klabu upo imara na utaendelea kupigania maslahi yao.
"Tumefikisha ujumbe wetu tuliokuwa nao kwa Waziri, na niwahakikishie wanachama wa Yanga viongozi wao ni imara na tunapigania maslahi ya klabu yetu" -Eng. Hersi
Kwa upande wa Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Ally Haji baada ya kikao kizito kati yao Serikali, Bodi ya Ligi pamoja na Shirikisho la Mpira Nchini TFF ametoa neno lake moja juu ya kilichoendelea kwenye Kikao hicho kwa Wanachama na Mashabiki wa Yanga.