Engine oil gani ni nzuri kwa Gari aina ya IST?

Yes...kwa ist si vizuri kutumia hiyo oil...hiyo ni nzito sana
Mkuu nashukuru sana kwa maelezo mazuri. Mimi gari yangu ni Subaru Impreza cc1500. Wakati gari imekuja service ya awali kabla sijaitumia ilitumika Castro oil 20w50. Kwa kuzingatia maoni ya wadau humu ni kuwa sio oil sahihi. Je, nibadilishe nitumie 5w30 au niendelee na hiyo 20w50?
 
Angalizo wakuu kama gari yako ishaejda makilomita mengi na ushaweka sana oil zetu zile mineral oil SAE 40 ,20W 50W angalia sana ukihamia kwny hzi full synthetic na nyepesi kama 5W 30 oil inaeza vuja mana zinapenya penya sana coz ni nyepesi...

So utapo hamia huko kwny hizo nyepesi uwe makini kucheki level kama mkweche wako ushavuka kilomita laki moja other wise baki tu huko kwny hzo nzito nzito
 
Mkuu bado hujachelewa..nakushauri shift from 20w50 to 5w30 au 10w30 haraka iwezekanavyo....
Hizi oil zenye namba kubwa kama sae 40 na hizo 50 ni nzuri zaidi kwa high mileage engines na heavy duty vehicles kama madala dala, canter, fuso..

Hizi gari zetu ndogo za petrol inapendekezwa zaidi oil ambazo ni multi grade na viscosity yake iwe 30 at optimum operating temperature..

Go for 5w 30/ 10 w 30 mkuu....unaweza kutumia hiyo hiyo Castrol, total au kampuni nyingine yoyote inayoaminika..
 
Asante sana. Nitazingatia ushauri wako.
 
Wadau nina ist ya 2006, juzi niliipiga sehemu radiator ikapinda ikagusa fan na kuzuia fan kuzunguka... Kulikopelekea motor kuungua.

Baada ya motor kuungua fan ikashndwa kuzunguka na mashine ikaanza kuheat.

Shida yangu ni kuwa nishaweka motor zingine kama 2 hivi na bado injini inaheat kwa kilometer chache tu hata 30 hazifiki na maji yanaisha kabisa.

Nb.
Rejeta haivuji, sasa hapa solution ipo vipi.
Je kuna aina ya moto special kwa hizi gari, au fan special,. Na ni wapi naweza nikaipata na kwa gharama gani maaana nateseka saana na nina safari. Ya kwenda bukoba week ijayo.
 

blades za mota uliyoweka na uliyotoa zinalingana?
vipi mzunguko wa motor upo sawa ? kuna motor zinazunguka anti clockwise, kuna zingine clockwise , hizi zinatofautiana kufunga na kama fundi alikosea hilo matokeo yake ni kuchemsha , gari ikiwa sationary inachemsha pia?
 
kuna oil wanasema inafaa kwa gari ambayo imeenda sana kilometer, je kati ya 5W30 na 10W30 ipi inafaa kwa iliyoenda kilometer nyingi? na je vipi kuhusu 5W40 ni bora kuliko hizo mbili hapo juu?
 
Duh kweli inahitaji ufundi.... Nisaidie utundu wa kugundua izo blades pamoja na iyo anti clockwise
 
Kingine mwambie kuweka maji kwenye Radiator sio sawa. Siku hizi tuna coolants
 
Ni dm nikuelekeze mbinu
 
Naomba kuuliza kidogo, ikiwa gar ina km laki 2 zen nikabadili injin na kuweka nyingine, bado maswala ya kilometa kwenye matumiz ya oil yana husika tenaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukibadilisha engine hapo ni sawa na umerudisha nyuma milage number ya gari sababu umeipa engine nyingine... So unatakiwa hata total milage pale ureset.... ianze upya.
 
kuna oil wanasema inafaa kwa gari ambayo imeenda sana kilometer, je kati ya 5W30 na 10W30 ipi inafaa kwa iliyoenda kilometer nyingi? na je vipi kuhusu 5W40 ni bora kuliko hizo mbili hapo juu?
Kama gari limeshaenda km nyingi sana mathalani zaidi ya 150k, 5w40 au 10w40 ndiyo pahala pake
 
Aisee nimeenda kwa fundi karekebisha kitu kidgo saana sasa sijuh km itahiti au raha..

Anadai feni ilikuwa inapuliza nnje kwemye rejeta badala ya kuvuta ndani... Kuna switch kachomoa akachomoa kitu ndani ya switch akageuza switch akarudishia basi..

Hapa ndio nipo natest ntaleta mrejesho
 
yap
ndio nilichomaanisha , nilikuuliza kama gari ikiwa stationary ina heat, hukurespond.
kwa kawaida kama blades zinapuliza nje gari ikiwa starionary tatizo la kuchemsha halijioneshi maana kunakuwa hakuna air resistance, ila ukianza kutembea hewa ya nje inapuliza ndani na feni inapuliza nje , hapo kunakuwa hakuna air movement, na gari inachemsha kirahisi kabisa
 
Hawa mafundi wa uchochoroni hawa wanabalaa kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…