Hizi namba kila moja ina tafsiri yake.
Unapokuta mfano 5W 30. Namba ya kwanza kabla ya W inawakilisha uzito wa oil. Kadri namba inavyozidi kuwa ndogo, ndivyo oil inavyozidi kuwa thin hivyo kuwezesha better performance at the cold start.
W simply inawakilisha winter wengine wanasema Weight wengine wanasema Watt...lakini inawakilisha Winter..
30 inawakilisha viscosity ( ile hali ya oil kuwa kama ina nata nata fulani hivi.)
Hii ina maana kwamba injini inpopata joto lake la juu ambalo linatakiwa ili ifanye kazi vizuri, viscosity ya oil hii bado itabaki katika kipimo hicho cha 30 ambacho kimewekwa na watengenezaji, hali kadhalika kwa oil namba 40 au 50
Kwa mantic hii oil 5w 30 ni nyepesi kuliko 10w 30.
Oil hizi zenye namba mbili yaani 5w 30 kwa lugha nyingine zinaitwa multi grade oils....ni oil ambayo imetengenezwa kufanya kazi katika mazingira ya baridi sana na joto sana.
Lakini hizi SAE 40 za kawaida ni mono garde....hizi ni maalumu kwa mazingira ya joto tu...na ndiyo maana kwa siai tulioko huku Arusha ikifika lile baridi la mwezi wa saba, kama gari ni ndogo na umeweka SAE 40, ukiliwasha asubuhi utasikia injini inavuma sana kwa muda mrefu...injini ikishafikia joto kiasi fulani ndiyo unaona inatulia...wakati unasubiri injini ipate moto, unakuwa unasaga vyuma..
Ukifuatilia zamani nchi zenye baridi kama huko Ulaya, walikuwa na oil za aina mbili..nzito kwa ajili ya msimj wa joto na nyepesi kwa ajili ya msimu wa baridi....watu walilazimika kumwaga oil msimu wa bari na kuweka oil nyepesi ya kukabiliana na baridi...hali kadhalika msimu wa joto, walimwaga oil nyepesi na kuweka nzito.
Kuepuka purikushani hizo, ndiyo Society of Automobiles Engineers (SAE) wakaja na oil ambayo ni mult grade mfano 5w30, 10w 30,10w40 n.k....oil hii ukishaiweka haichagui baridi wala joto wewe ni kuangalia tu muda wa service ukifika unaimwaga.
Hatari ya SAE 40 kwa garo dogo, haijalishi unaishi Dar au Arusha.... ukiwasha gari asubuhi wakati injini imepoa, oil hii kitaalam huchelewa kufika sehemu za juu za injini kutokana na uzito wake...pale inapichelewa, vyuma vinaendelea kusagana na unaendelea kuua injini yako taratibu...
SAE 40 ukitumia kwa magari makuu kuu sana haina shida...mfano madaladala au gari ambalo mileage imeenda juu sana pengine zaidi ya 180000km..