Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

Ngoma ndio Kwanza inaanza kupigwa....
Naamini ipo siku Mwamedi atasema tu ilikuwaje Hadi akatekwa Karibu na Ikulu...Time will Tell
Matukio ya aina hii yalikuwa yanafanywa na kundi la siri la watu kwa nia ya kuichafua Serikali ya JPM; changanya na za kwako!
 
View attachment 2386088
Legacy inazidi kuzamishwa chini zaidi. Mwendazake alikuwa wa hovyo sana

====
Aliyoandika Kabendera

Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.

Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.

Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.

Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.

Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.
 

Attachments

  • Screenshot_20211029-110122.png
    Screenshot_20211029-110122.png
    204.6 KB · Views: 2
Kwa huu mkeka unaochipua ni suala la mida tuu. Mlio karibu na makonda bashite mshaurini aombe asylum hata South Africa.

Kuna watu wazito waliumizwa na matendo yaliyotokea wakati Hayati akiongoza nchi wakidhani yalikuwa na baraka za Hayati Jiwe chuma.
 
Huo uhuru wako wa maoni nauheshemu. Kila jambo lina miiko yake.
Kwa hiyo nchi hii ni ya Kikwete?Kikwete mwenyewe wa hovyo hovyo.Anawaza kupiga picha na LIANA.Mungu atafanya maajabu tutapata mtu Kama JPM soon.Wahuni na vilaza wote tutawateketeza
 
Kwa hiyo nchi hii ni ya Kikwete?Kikwete mwenyewe wa hovyo hovyo.Anawaza kupiga picha na LIANA.Mungu atafanya maajabu tutapata mtu Kama JPM soon.Wahuni na vilaza wote tutawateketeza
Thubutu, hakuna tena sukuma gang kupewa nafasi kubwa serikali, Watanzania wamejifunza kwa Mwendazake
 
Kabendera anamsemea kikwete sio!!?

Ili iweje!?katumwa na muhusika Ili apate sababu na kumsghulikia nani!!?

Tusubiri!!
 
Makamu au PM wangeweza sema nini mbele ya mbabe yule? Waweza nipa namna mojawapo ambayo wangeweza kuukataa uovu wa Jiwe maana hata kujiuzuru tu ingekula kwao
Zipo namna nyingi za kuukataa uovu......kuukalia kimya uovu na wewe ni sehemu ya uovu......
 
Back
Top Bottom