Ethiopia inaenda kuvunjika kama Yugoslavia

Wagweno si kama wachagga chunguza utagundua
Kwa wapare kuna wagweno......nasikia hata mila zao kidogo ni tofauti na za wapare wengine hao ndo nasikia walitokea Ethiopia maana wana tamaduni nyingine ambazo ni tofauti kdg na za wapare wabantu
 
Duuuh....taifa lina "ukabila" Hilo...

Yaani pamoja na kuwa hawamsupport Abiy,ila kwenye "mtanange" wamekaa Upande wake....πŸ˜‚πŸ˜‚

Mwalimu Nyerere ALIONA MBALI SANAA....

May His Soul Rest In Peace aamen aaamen.
 
Wako vizuri wale na umoja. Makabila mengine wivu tu. Ila Abiy angechelewa tu kidogo tu sasa kungekuwa na taifa la Tigray. Amhara wamemsaidia sana jamaa. Nembo ya Tigray na bendera hapi chini
...bora kawawahi...maana ni mwanajeshi huyo!!!

Halafu Kuna kipindi BATTALION ya jeshi ilikwenda kumvamia ikulu...akawatuliza...je nao walikuwa wanaongozwa na hayo ya UKABILA Jeshini?!!!!
 
Duuuh....taifa lina "ukabila" Hilo...

Yaani pamoja na kuwa hawamsupport Abiy,ila kwenye "mtanange" wamekaa Upande wake....πŸ˜‚πŸ˜‚

Mwalimu Nyerere ALIONA MBALI SANAA....

May His Soul Rest In Peace aamen aaamen.
Kwakweli japokuwa alikuwa na mabaya mengi tu lakini kwenye hili la kuthibiti ukabila mwalimu Nyerere kwakweli alifanya la maana sana
 
 
Hatareee....

Kwangu Abiy Ahmed ni "kiona" mbali...
Abiy anafuata siasa za "mandela" japo hazifanani na " hayo"πŸ˜‚

Ni mtazamo tu....kwa wale wenye mitazamo ya kila mtu "ashike chake" kama ilivyotokea kwa SUDAN KUSINI na UINGEREZA kutoka EU,ama Polisario kuachana na Morocco basi ABIY AHMED ni kizingiti....

Ila kwa sisi tunaotaka unification (japo Kuna kipindi ni ngumu) kama mwalimu Nyerere basi ABIY AHMED ni HERO HASWAAA....
 
Mkuu ulipotelea wapi. Kipindi sijajiunga JF nilikuwa nakuona sana humu sikuhizi kulikoni
 
Kumbe wewe ndio Coppenhagen DN?
 
Oooo....

Demokrasia ni mfumo mzuri na bora ilioje kwa "wastaarabu" si "Walugaluga".....

Ndio mana BARA ARABU wanapata shida sana kwa kulazimishiwa mfumo "alien"....

Sasa ona kichekesho,nchi Kama Lebanon ambayo kidogo ina values za nchi za kimagharibi(wafaransa) lakini bado NGOMA mbichi.......

So Abiy Ahmed ajitahidi kubalance....aendelee kuihuisha DEMOKRASIA kidogodo....ajenge nchi kimkakati...ila WAKOROFI asiwaonee "SONI"....

Naona Jawar ameshapigwa kesi ya TREASON na TERRORISM loooh pagumu hapo...
 
Nguseroh unakosea kuwapendelea Watigray kisa eti "ni wazuri na smart". Ethnicity yeyote inayoleta ujuaji huwa siikubali kabisa na Abiy namuunga mkono sana.

Hizi jamii za Ethiopia pamoja na ugumu wake zinatakiwa ziisikilize Federal government. Vita ilitakiwa iwepo zamani pale jamii zilipoanza kumiliki majeshi, hakuna jambo la maana linatokea kila mmoja akiwa na jeshi lake.

Abiy namuunga mkono sana ila nina wasiwasi na Egypt kama haihusiki kwa siri. Kuna uzi nilichangia nikasema Egypt hawezi jiangaisha kupigana na Ethiopia wakati kuna ethnicity. Anatoa fedha Na silaha tu anatumia gharama kidogo na anakaa na majeshi yake kwake.

Naona tutakuwa na vita kama Biafra
 
Hawa ndugu zetu wenye asili na nywele za kikemikali na pua ndefu kidogo wanajionaga class fulani hivi, acha wanyooshane tu mpaka watakapopata akili.
πŸ˜‚πŸ˜‚
Mkuu binadamu wenzako hao....ha ha ha waache na hulka zao...
Tumeumbwa tofauti...
Tuna experience tofauti....

Yaap ndio hivyo wanachapana tena
 
Huyu alipaswa aungana na Abiyy ili atumie ushawishi wake kuiunganisha nchi ila jamaa anatumia kete ya ukabila kusaka madaraka.
 
Huyu alipaswa aungana na Abiyy ili atumie ushawishi wake kuiunganisha nchi ila jamaa anatumia kete ya ukabila kusaka madaraka.
Nimewaza Kama WEWE...huyo JAWAD ni mkabila sana tu.....

Halafu ukabila wake unaonekana kwani yeye ni PURE Oromia ila Abiy Ahmed ni chotara(Oromo+Amhara).

Ukabila ni kitu KIBAYA MNO....
Ukiukumbatia kipindi fulani ujue kitakuja KIPINDI nguvu hizo ZITAPOTEA....angalia TIGRINYA kwa miaka mingi walivyokuwa WANATAMBA chini ya Zenawi....leo NGUVU ile imewandoka....WANAITAFUTA TENA my foot....

Rip Baba wa Taifa JKN,aaamen aaaamen!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…