Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 6,696
- 6,734
Hivi mtu unajisifia una PhD kumbe PhD yenyewe ni ya sociology,law, education,public administration, accountant, public relations, community development n.k hizi PhD ambazo hazin faida yoyote zaidi ya mtu kupoteza muda tu darasani bila msingi wowote ule hizi zinatakiwa zifutwe nakuendelea hazisaidii kuleta maendeleo zaidi nchi inaenda kudidimia tu na watu kukalia uchawa tu kwa PhD ambazo
hazina mbele wala nyuma
Shame on them
Kuna PhD nyingi ambazo hazina uhusiano wowote na hali halisi ya huku mtaani. Na kizuri hata mitaa kwa mujibu wa majina yake, hayazitambui.
Hazina msaada wowote kwa mtu binafsi mwenye hiyo PhD, wala kwa wannaosoma ili wapate maarifa, wala kwa ujenzi wa Taifa letu changa, linalohitaji kweli watu makini, wanaojituma na kutoa majawabu kwenye changamoto zetu zilizoko kwenye jamii.
Nyingi ya hizo kitu ndio chanzo cha mdororo wa maarifa na ongezeko la umaskini. Ni chanzo cha wezi na majambazi wa rasilimali lukuki zilizopo, kwa ujanja na uongo uongo wao. Ni chanzo ya kutumia vibaya nafasi na dhamana mbalimbali wanazokasimiwa.
In fact, ni moja ya mambo ya uafrika wetu ambao wengi tunajibeba na kutaka kuheshimiwa au kufahamika kwa sifa ambazo wala hatuna.
Mtu proper, hata awe na degree kadhaa, huwa anapenda aitwe kwa jina lake tena bila mbwembwe. Maana amekamilika. hana sababu ya kuanaza kuonyesha yeye n i msomi ili atambulike. Wasomi wanajuana kwa mambo yao bila hata kuambiana wamesoma nini