Eti mtu anajisifia ni PhD, halafu PhD ambazo hazina mchango wowote kwenye maendeleo ya nchi hii


Kuna PhD nyingi ambazo hazina uhusiano wowote na hali halisi ya huku mtaani. Na kizuri hata mitaa kwa mujibu wa majina yake, hayazitambui.

Hazina msaada wowote kwa mtu binafsi mwenye hiyo PhD, wala kwa wannaosoma ili wapate maarifa, wala kwa ujenzi wa Taifa letu changa, linalohitaji kweli watu makini, wanaojituma na kutoa majawabu kwenye changamoto zetu zilizoko kwenye jamii.

Nyingi ya hizo kitu ndio chanzo cha mdororo wa maarifa na ongezeko la umaskini. Ni chanzo cha wezi na majambazi wa rasilimali lukuki zilizopo, kwa ujanja na uongo uongo wao. Ni chanzo ya kutumia vibaya nafasi na dhamana mbalimbali wanazokasimiwa.

In fact, ni moja ya mambo ya uafrika wetu ambao wengi tunajibeba na kutaka kuheshimiwa au kufahamika kwa sifa ambazo wala hatuna.

Mtu proper, hata awe na degree kadhaa, huwa anapenda aitwe kwa jina lake tena bila mbwembwe. Maana amekamilika. hana sababu ya kuanaza kuonyesha yeye n i msomi ili atambulike. Wasomi wanajuana kwa mambo yao bila hata kuambiana wamesoma nini
 
Kulist community development umechemka...hao ndio injini ya maendeleo..inaonekana wewe huna elimu ndio maana unawivu na elimu za watu...ruka urukavyo,sema usemavyo ila elimu sio ya kuibeza hata kidogo
Kwa Tanzania hawajasaidia chochote hao watu. Hata wa sayansi nao hawana mchango.
Mwafrika Ni janga tu hasa mtanzania.
Nioneshe maendeleo gani hapa nchini tumepata kutokana na wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…