Eti Wema mzuri zaidi kumzidi Zari?

Eti Wema mzuri zaidi kumzidi Zari?

attachment.php


Kumbe! Imebainika kuwa maneno ‘gold digger ’ katika ulimwengu wa fursa yanamaanisha kuwa ni mtu anayeona fursa na kuzitumia katika ‘ kufaiti’ kupata mafanikio (utajiri ) kwenye maisha.

Zarinah Hassan ‘ Zari The Boss Lady ’
Ndivyo alivyo mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz ’ , Zarinah Hassan ‘ Zari The Boss Lady ’ ambaye humwambii kitu linapokuja suala la kuona fursa na kuzifanyia kazi

PAMOJA NA HAYO, WEMA MREMBO ZAIDI
Pamoja na sifa hiyo iliyomfanya Zari kuwa mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki lakini kwa mujibu wa mashabiki waliomuona ‘ laivu’ usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye shoo yake ya Zari All White Party katika Ukumbi wa Mlimani City walisema aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla yake , Wema Isaac Sepetu ni mrembo zaidi kuliko yeye.

Wema Sepetu na Zari The Boss Lady
Likiwa ndani ya mjengo , Ijumaa Wikienda liliwashuhudia wadau wengi ambao walimuona Zari kwa mara ya kwanza wakimshangaa na kudai kuwa yupo tofauti na anavyoonekana.

Kwa mujibu wa mashabiki hao , picha ambazo wamekuwa wakiziona kwenye mitandao ya kijamii zinakuwa zimeeditiwa (kuhaririwa ) na kwamba ukimuona ‘ live ’ huwezi kuamini .

YUPO TOFAUTI NA KWENYE PICHA
“Jamani siamini kama huyu ndiye Zari tunayemuona kila siku kwenye Instagramu maana yupo tofauti sana.

“Kwa waliokuwa wanasema anamzidi Wema wamenoa . Wema ni habari nyingine, ” alisema mmoja wa warembo waliokuwa wakisukumana kumuona Zari.

“Mimi nadhani ni kwa sababu labda amezaa watoto watatu na sasa ana ujauzito wa Diamond wa mtoto wa nne so hawezi kumfikia Wema ambaye bado hajazaa, ” alisema mrembo mwingine akimtetea Zari .

MAKE - UP 100%
“Hamna bwana, kinachombeba Zari ni make - up (vipodozi ) ambavyo anatumia kwa asilimia mia moja lakini Madam (Wema ) hata asipotumia make - up lazima utampenda tu, ” alisema mwingine aliyedaiwa ni Team Wema.

Kuhusu make - up , Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa watu wa Timu ya Diamond ya Wasafi Classic Baby (WCB ) ambaye yupo kitengo cha mapambo ambaye alithibitisha kuwa Zari hufanyiwa make - up kwa muda mrefu hadi mwenyewe akubali kuwa yupo sawa.

Mdau mwingine aliliambia gazeti hili kuwa Zari ni mjasiriamali na ameona kwa Diamond kuna fursa ndiyo maana akakubali kumbebea ujauzito lakini si kweli kwamba ni mrembo kuliko Wema.

“Ameona fursa kwa Diamond . Kwa mfano shoo kama hii (Zari All White Party ) asingeweza kuifanya bila kuwa na ‘ koneksheni’ na Diamond , ” alidai mdau mwingine .

ZARI AMEONA FURSA
Habari zinasema kuwa Zari ameona kuna fursa nyingi Bongo ndiyo maana amekubali kufunga ndoa na Diamond bila kujali kigezo cha umri. Ana umri wa miaka 34 wakati Diamond ni 26.

Akijibu swali juu ya uraia wake wa Uganda na Afrika Kusini na kwamba yeye na Diamond wanatarajia kuishi nchi gani mwanamama huyo alifunguka :

“Tutaishi hapahapa (Bongo ). Kwa utamaduni wetu (Waafrika ) inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote .

“Watanzania ni watu poa sana , siwezi hata kuwalinganisha ni wakarimu sana . ”

HISTORIA INASEMAJE?
Kuna madai mazito kuwa Zari si mtu wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hana fursa ya kimaendeleo kwani historia inaonesha kwamba wanaume wengi aliowahi kuwa nao walikuwa ni watu wenye nazo.

HAJAWAHI KUWA NA MWANAUME HOEHAE
Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa naye wanaosemekana kwamba hawakuwa watu hoehae ni pamoja na aliyekuwa mumewe , Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu akiwa ni mmoja wa mabilionea nchini Uganda.

Wengine ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda , mtoto wa mjini nchini Uganda , Farouk Sempala , Jenerali Jeje Odong , wasanii wa muziki, Moze Radio na Weasel , Aziz Azion , Isaiah , Robert Ogwal a .k .a Rasta Rob , Exodus , DJ Shiru , mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond

Acheni kulinganisha PERFUME na USHUZI....Wema hamfikii Zari kwa uzuri na hatamfikia maisha yake.
 
Hakika Zari ni mzuri!Kwakweli Wema hawezi kumfikia hata kidogo!
 
Jamani Kigoma kuna shida nyingi. Waache kutusumbua watumie pesa zao kusaidia nyumbani walikotoka wazazi wao. Waache kuchezea fedha huku town. Tungefurahi kupata picha za kijijini kwao na familia zao. Wasijekuwa kama k☆××mba kafa kamwacha mzazi kijijini hoi na mwingine mjini kwenye nyumba za kupanga.

Wewe umesaidiaje ungehorozesha wafate mfano kama unadhani wao hawajali wazazi wao.

Shida za Kigoma kawaambie mkyu wa mkoa, mbunge, madiwani ndio kazi yao kufanya.
 
Na huyu wanasema ndio anafanya global publisher anahongwa na wema na ametokea kwenye tv program yake so anakula hela ili ampaishe wema hadi anaandika upumbavu mkubwa kama vile sio mwandiahi wa habari....

Alipataje kazi huyu imelda?

Uwiiiiiii! Jamani hili ni zimwi au mwanamke?
Ila nasikia ni chakula cha boss wake na anampenda vibaya sana!
 
Mmmhhhh na huo unene kuvaa nguo za wazii 😆😆

ha ha ha...wakati mwingine bora hizi habari wangeandikaga waandishi wa kiume...
Baada ya kuona picha ya mwandishi nilijua tu lazima kibao kimgeukie....
 
Sasa Idris akapost picha kama kawa....kumbe hakuichakachua....duh ilipodakwa na kuanza kuzunguka ndio wema akamuomba aifute akaichakachua na kupost ingine kwa bahati mbaya yake ilishazunguka...ndio hiyo miguu aka edit then wakamtumia airushe tena....

Yaani mikorogo na michiriI imejaaa...kumbe anachakachua picha hata za usoni kwake kudanganya. Makeup inamkataaaa...matako ya mchina

Zari ni hakunaga

Mhhhh wema kaozaje jamani? Hivi akizaa huyu atafaa kuangalia kweli?
Yaani sijui hao wanaume zake wanajisiake akivua nguo!
 
Idris anakua mcharo jamaniii mbona hiyo picha hajaifuta ipoo ,,ila zari ana ngozi nzuri jamaniii

Nimesoma kuwa aliiweka yenye miguu chakavu akatoa. Ok thanks now nimeona bado ipo ila aliongeza iliyopo janet na dogi wamekaa nao. Cheers
 
Uwiiiiiii! Jamani hili ni zimwi au mwanamke?
Ila nasikia ni chakula cha boss wake na anampenda vibaya sana!

Kama chakula cha bosi basi inaonyesha kwanini yeye na w wanaelewana katika tabia mbovu.
 
Mhhhh wema kaozaje jamani? Hivi akizaa huyu atafaa kuangalia kweli?
Yaani sijui hao wanaume zake wanajisiake akivua nguo!

Kwa kweli bora angeacha tu kutaka kushindana na mke wa Chibu. Yaani anamuacha Chibu halafu anataka afanyaje aishi anagonga mlango kumbembeleza na ndio hawezi tena imetoka hiyo....lazima atakuwa ameenda kwa mganga maana kundi lake wote hao ndio wamekaa kushinda kwa baba kudaka biashara kwa inayowaingia....

Anauzi bora atulie na akemee washabiki....ndio kwanza anasafiri na akina dogi sasa kwenda mwz...so anayapenda na atazidi kutukanwa na kushuka mashabiki wameshamkimbia na wanazidi kusepa wanaojielewa.
 
Kwa kweli bora angeacha tu kutaka kushindana na mke wa Chibu. Yaani anamuacha Chibu halafu anataka afanyaje aishi anagonga mlango kumbembeleza na ndio hawezi tena imetoka hiyo....lazima atakuwa ameenda kwa mganga maana kundi lake wote hao ndio wamekaa kushinda kwa baba kudaka biashara kwa inayowaingia....

Anauzi bora atulie na akemee washabiki....ndio kwanza anasafiri na akina dogi sasa kwenda mwz...so anayapenda na atazidi kutukanwa na kushuka mashabiki wameshamkimbia na wanazidi kusepa wanaojielewa.

Kwani dougie ndio yupi katika zile picha za mwanza? Hebu tuwekee hapa basi maana mimi sijajua kuhusu hilo.
 
Mhhhh wema kaozaje jamani? Hivi akizaa huyu atafaa kuangalia kweli?
Yaani sijui hao wanaume zake wanajisiake akivua nguo!

Kweli mikorogo ni hatari sana wana moyo wa chuma aisee mi siwezi kabisa kutokuheshimu mwili tu.Akizaa si ndo majanga itakua sasa au afikishe thelathini na tano utamsahau.
 
Back
Top Bottom