Ewe kijana/baba/mzee, kama una nafasi moja ya kutoa msaada. Msaidie mwanaume

Wanaozeshwa mapema, wanapewa kazi nyingi za nyumbani, wanaonewa kidogo mkuu.

Ila bado naona kama wengi hawana uthubutu.

Pia sisi wanaume tunaumizana wenyewe unakuta kijana ana wasifu mzuri wa kazi ila anapewa binti kwasababu ya kalio lake kubwa linalomvutia bosi.
 
Wanaume tumeumbwa mateesoo, mateeesooo, kuhangaikaaa
 
Bado tunarudi pale pale mzee mwanzangu. Hakuna sehemu ambayo nimesema mwanaume asifanye kazi au awe shoga.

Madhira mengi anayokutana nayo mwanaume yanasaidika lakini anapuuzwa tu kwa sababu ni mwanaume. mfano umepita mitaa ya uswazi ukaona vijana wadogo wanacheza mpira wakiwa na vifaa chakavu. Hivi kama uwezo unaruhusu kuwanunulia tu gozi la ng'ombe na zile koni za mazoezi ilo ni suala la ku-complicate kiasi hicho. Miaka ijayo kwenye kundi la hao watoto anaweza akatoka messi hapo. Utakua umechangia safari yake ya mafanikio
 
Shule ya msingi nilisoma shule ya bweni kijijini. Utotoni nilikua mtundu sana bi mkubwa akaona anipeleke bweni ili apumzike na kesi za mtaani. Kwaiyo najua hali ya uko kijijini ipoje. Nakumbuka tulikua tunafanyaga mitiani ya ujirani mwema. Almost top 50 ni watu wa bweni ambao tunatokea mijini. Perfomance za watu wa day ambao ni wa hapo hapo kijijini ni za chini sana
 
Ni sawa ila kumbuka huwezi kuimaliza dunia kwa kumsaidia kila mwenye uhitaji umuonaye.
 
Ni kweli kabisa, Man you wrap it. Kile ambacho wengi hawataki kukubali ni kwamba mifumo ya kijamii imejengwa kwa namna ya kumpa mwanamke huruma na kipaumbele hata pale ambapo hajastahili.

Ukiangalia hata katika ngazi ya kifamilia, mara nyingi baba hubaki kama “provider” tu, watoto wengi huwatenga Baba zao na kuwa karibu zaidi na Mama.

Wakati wa migogoro ya kifamilia, hasa talaka, mfumo wa kisheria humfavor mama zaidi na kumkandamiza Baba. Hii ni mifano ya wazi ya namna mfumo unavyompa mwanamke kipaumbele bila kuangalia uhalisia wa mchango wa mwanaume.

Mashirika mengi ya misaada na miradi ya kijamii hujikita zaidi kwa wanawake (mfano: mikopo ya vikundi vya wanawake, mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake), huku wanaume wakiachwa pembeni kana kwamba hawahitaji msaada wa kijamii.
 
Hatuwezi kupata msaada kwenye mifumo ya kimamlaka wala kutoka kwa wanawake. Suluhisho pekee kwa wanaume ni kupigana tafu wenyewe kwa wenyewe.
 
As a feminist, nina supports movements zote za makundi maalumu, brotherhood ikiwemo. Lakini ngoja nikupe cheat code:

Wanawake hatusaidiwi kwasababu tunapendwa, tunasaidiwa kwasababu ya “title” tuliyopewa “kiumbe dhaifu “.

Kwahiyo ili mwanaume asaidike kwa urahisi ni lazima tum-nominate kama kiumbe dhaifu kwanza, 😅 Apparently a man is villain, huwezi jitolea kumsaidia a Villain . Mfano wako: Kusimamisha kumpa mwanaume lift kitu kitakachokuja kichwani ni what if akinikaba akachukua gari au chochote, naelewa ni mfano tu na sio wanaume wote wako hivyo na mtu yeyote hata mwanamke anaweza kuwa a villain 🦹 Ila fikiria dhana nzima ya nilichosema.

Kisaikolojia, Ulishawahi kujua kwanini watu wanasaidia? In most cases a sense of Pride na kuestablish utawala.

Kaka; Vitu havitokei tu lazima narrative zibadilishwe kwanza. Me and you, We don’t make rules!
 
Kumwangalia mwanaume kama kiumbe dhaifu nayo ni narrative pia. Sio lazima tumpe iyo title ya udhaifu ndio tumsaidie. Tunaweza kumsaidia kwa kumwangalia mwanaume nae ni binadamu ambaye kuna wakati anakwama. Hapa jf kuna vijana nineshawapiga tafu na hata usename zao sizikumbuki, kwaiyo kumsaidia mtu sio lazima iwe kwa lengo la kumtawala
 
Kwani binti kiziwi, mwanamke sio dhaifu?
 
Nashawishika kusema walioleta feminism ni watu ambao ufikiri wao ni mkubwa, kama tu walioleta dini.

Maana yangu kusuggest narrative ile ilikuwa ni kukuonesha kuwa ili kitu kiwekwe on action lazima idea yake iwe global! Huruma sio hisia ya kidunia so as love, lazima kuwe na kingine kizito zaidi……..
 
Nashawishika kusema walioleta feminism ni watu ambao ufikiri wao ni mkubwa, kama tu walioleta dini.
Tukiingia kwenye feminism tutatoka kabisa nje ya mada maana hata wewe mwenyewe kama unahalalisha mwanamke kupewa favoritism kwa kigezo cha gender victimhood automatically unapingana na feminism ambayo inasema mwanaume na mwanamke wapo sawa.

Usawa maana yake qualifications ziwekwe wazi kila mmoja achujwe kulingana na uwezo wake. mfano ubunge, sifa za mbunge ziwekwe wazi, watu wachukue form, waende kwenye kampeni, wapigiwe kura, washindi wakawalishe wananchi bila kujali kigezo cha jinsia. Hiyo ndio feminism yenyewe., sasa tukisema pale bungeni tuweke viti maalumu kwa ajiri ya wanawake tu hiyo sio feminism tena, isipokua ni gender descrimination.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…