Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 14,421
- 40,936
- Thread starter
- #61
Kwa average ya maisha ya vijana kibongo bongo naweza nikasema nipo kwenye uelekeo mzuri kwenye karibu maeneo yote.Mleta mada una tatizo sehemu pole sana. Anyway wanawake sio chanzo cha matatizo yako bali destiny na fate havipo upande wako.
Suala la elimu tangu primary nilikua nashika namba za juu darasani. Sekondary olevel ninesoma azania sekondary pale magomeni na alevel ninesoma mzumbe morogoro uko kote tayari nishakichafua sana. Chuo nime-graduate kazi ya economics and finance sio kwa kupata first class tu, but first class with honors.
Suala la mahusiano nipo njema. Nimeoa. Mimi na mke wangu tuna mtoto mmoja wa kiume ambae kwa sasa ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hakuna migogoro nyumbani kwangu.
Nikiwapa vijana miongozo ya standard za kuzingatia wakati wa ku-settle na mwanamke haimaanishi kwamba kwangu kunawaka moto. Najaribu tu kuwapa muongozo kwa sababu mimi kama mmoja wa kijana ambae nime-dedicate maisha yangu kuwainua vijana wenzangu naona changamoto wanazopitia na wengi washakuja kuniomba msaada, kwa mantiki najiona nawajibika kuwaongoza ambao bado hawajayatimba
Suala la kipato nipo njema pia. Nilishafanya kazi moja ya benki kubwa hapa bongo kama business banking officer.
Niliacha kazi benki baada ya kupata ofa nzuri zaidi Delloite kama statistic analyst officer.
Niliacha kazi Delloite pia baada ya kupata ofa nzuri zaidi USAIDS kama financial suporvisor. Nikafungua kampuni yangu ya masuala ya auditing na baadae nikacha kazi USAID'S ili nielekeze mkazo zaidi kwenye kamouni yangu.
Kampuni inafanya vyema na nimeajiri vijana kadhaa. Kwahiyo sipo katika phase ya kuhitaji msaada wa kuinuliwa kimaisha. Nawaongelea madogo na vijana waliokwamba. Mimi mwenyewe nipo njema.