Ewe kijana/baba/mzee, kama una nafasi moja ya kutoa msaada. Msaidie mwanaume

Ewe kijana/baba/mzee, kama una nafasi moja ya kutoa msaada. Msaidie mwanaume

As a feminist, nina supports movements zote za makundi maalumu, brotherhood ikiwemo. Lakini ngoja nikupe cheat code:

Wanawake hatusaidiwi kwasababu tunapendwa, tunasaidiwa kwasababu ya “title” tuliyopewa “kiumbe dhaifu “.

Kwahiyo ili mwanaume asaidike kwa urahisi ni lazima tum-nominate kama kiumbe dhaifu kwanza, 😅 Apparently a man is villain, huwezi jitolea kumsaidia a Villain . Mfano wako: Kusimamisha kumpa mwanaume lift kitu kitakachokuja kichwani ni what if akinikaba akachukua gari au chochote, naelewa ni mfano tu na sio wanaume wote wako hivyo na mtu yeyote hata mwanamke anaweza kuwa a villain 🦹 Ila fikiria dhana nzima ya nilichosema.

Kisaikolojia, Ulishawahi kujua kwanini watu wanasaidia? In most cases a sense of Pride na kuestablish utawala.

Kaka; Vitu havitokei tu lazima narrative zibadilishwe kwanza. Me and you, We don’t make rules!

Hapo feminism imekudanganya. Hamsaidiwi kwasababu ya narrative ya kwamba nyinyi ni dhaifu. Ni kwasababu ya asili ya mwanaume kupenda ku "prove" kwamba ana uwezo wa ku "provide". We are naturally sacrificial. Some women abuse our tendency to volunteer to help them.

But many times it's our own fault. We go too far. Mbaya zaidi ukiwa "simp" au niseme "ignorant" unasaidia mwanamke hata pale ambapo mwanamke hahitaji msaada wako. Na wanawake mlivyo "humble" au tuseme "wajanja" huwa mnapokea tu mkipewa msaada hata kama ni kwa shinikizo. Binafsi huwa silaumu wanawake kwa hii tendency yao. Nalaumu wanaume kwa kudhani wanawajua wanawake kumbe hawawajui hata. I learned the hard way.
 
As i said earlier, we don’t make rules, they do…. Wanawake kusaidiwa has nothing to do with women, has everything to do with men, Gladly sisi tunapata matokeo, lakini viungo, ladha (Pride) anapata mwanaume. Naelewa hili ni somo gumu sana watu kulielewa sababu some of you mnasaidia genuinely from a point of love/huruma/sacrifice ila from the beginning haikuwa hivyo, haikutakiwa kuwa hivyo 😅

Narratives zinawekwa kujustify mambo fulani fulani, Na ili mambo yawe at large lazima narrative ziwe global.

Naturally sacrificial? why yall don’t sacrifice for your fellow men? Kwanini mkachagua kuwa sacrificial kwa wanawake? Imebidi watokee wanaume kama mleta mada karne ya 21 kuhamasisha brotherhood.

Trust me hii dunia sio ya kwangu mimi na wewe.

Otherwise… your mind is gorgeous… you can think and think.
 
Tukiingia kwenye feminism tutatoka kabisa nje ya mada maana hata wewe mwenyewe kama unahalalisha mwanamke kupewa favoritism kwa kigezo cha gender victimhood automatically unapingana na feminism ambayo inasema mwanaume na mwanamke wapo sawa.

Usawa maana yake qualifications ziwekwe wazi kila mmoja achujwe kulingana na uwezo wake. mfano ubunge, sifa za mbunge ziwekwe wazi, watu wachukue form, waende kwenye kampeni, wapigiwe kura, washindi wakawalishe wananchi bila kujali kigezo cha jinsia. Hiyo ndio feminism yenyewe., sasa tukisema pale bungeni tuweke viti maalumu kwa ajiri ya wanawake tu hiyo sio feminism tena, isipokua ni gender descrimination.
You missed my whole point on this, nilikuwa najaribu kukwambia kuwa walioanzisha movements kama feminism au dini ni watu wenye akili sana, Maana yake ili movement yoyote ifanikiwe lazima uchanganye school of thought na mambo ambayo yanaonekana ni asili wakati in a real sense ni man made.

Nilikuwa najaribu kukosoa andiko lako kwa kukwambia you can do better, sababu movements zote zilizofanikiwa haziendeshwi kwa facts (kama ulivyofanya kwenye hili bandiko) Zinaendeshwa kwa manipulations….! Facts ni ngumu, manipulation ni rahisi… do you remember my suggestion earlier?

Otherwise it’s your parade ngoja nikuachie uwanja wako.
 
Mimi sifanyi movement yoyote. Am just talking the facts.
 
Wanaozeshwa mapema, wanapewa kazi nyingi za nyumbani, wanaonewa kidogo mkuu.
Ila bado naona kama wengi hawana uthubutu.
Natafuta Ajira umepewa point nzuri hapo juu 👆 , umeziruka kwa sababu hazitoi favor kwenye hoja yako ukaenda kujibu kwa mfano wa kitoto wa shule za bweni.

Mgawanyo wa majukumu ya nyumbani na mila zetu hazimpi nafasi sawa mtoto wa kike na hivyo kuwa na ulazima wa kumsaidia, mfano kimasomo ili kulazimisha usawa ambao bado haupo kwenye jamii.

Kwenye nchi za Ulaya ambapo kwa kiwango kikubwa wameondokana na mfumo dume, wasichana wanamaliza highschool na vyuo vikuu kwa viwango vikubwa vya idadi na ufaulu wa juu kuliko wavulana proving kwamba competence haiko tied to jinsia. Na huko wanawake hawahitaji misaada, mifumo rasmi ya usaidizi wa kijamii iko sawa kwa wanaume na wanawake.

Tukirudi kwenye mada: Saidia mtu ambaye ana uhitaji bila kujali jinsia yake.
Unaendesha gari wakati wa mvua na umewaona mwanaume na mwanamke kando ya barabara wananyeshewa mvua wakati katika gari yako imebaki siti moja tu, mpe lifti mwanaume.

Kwa sababu mwanamke hatosimama hapo kando ya barabara kwa muda mrefu. Huyo mwanamke atapata lifti, comfort na msaada mwingine sio kwa sababu anastahili zaidi ya mwanaume ila ni kwa sababu ya jinsia yake. Thousands of simp men are waiting to play hero just to earn a smile of fake validation.

Upande wa mwanaume sasa usipompa hiyo lifti kuna uwezekano akaendelea kusimama hapo mvuani kwa masaa mengi sana na asipate msaada wowote huku wanaopita na magari yao hapo barabarani wakimpuuza tu.

Hakuna atakaejali kama anapigwa na baridi, ana njaa au kachoka. Hakuna atakaeona maumivu yake kwa sababu jamii inatarajia aweze kukabiliana na kila kitu. Being a man is both curse and crown. You get no sympathy, but you get strength.
Ukiwa na gari, ni uamuzi wako nani wa kumpa lift.

Kwangu nitampa mwanamke kwa sababu kuna possibility anasubiriwa kuhudumia watoto nyumbani hata baada ya kutoka kazini au kwenye majukumu mengine au hata hapo alipo, inawezekana amebeba mtoto tumboni kwake na sijui.

In addition; kuna uwezekano mkubwa zaidi wa mwanaume kunidhuru, sababu wengi wenu mna nguvu za mwili kutuzidi, na baadhi yenu ni sexual predators, kukusaidia lazima nijihakikishie kwanza kama nitakua salama!
 
Album ya men's first, iko tayari 🔥.

List of tracks
  • me first
  • sina ya kutuma na ya kutolea.
  • 50/50 kuna deal ya zege twende
  • you don't want a broke man, I also don't need a broke woman.
  • cheat on me, you make a 50m pay as damage.
  • prenuptial marriage agreement.
That is exactly gender equality women demands, but guess what? They can't bearing it. Women don't want gender equality, the want selective equality. They want to choose when and how to be equal with men.
 
Natafuta Ajira umepewa point nzuri hapo juu 👆 , umeziruka kwa sababu hazitoi favor kwenye hoja yako ukaenda kujibu kwa mfano wa shule za bweni.

Mgawanyo wa majukumu ya nyumbani na mila zetu hazimpi nafasi sawa mtoto wa kike na hivyo kuwa na ulazima wa kumsaidia, mfano kimasomo ili kulazimisha usawa ambao bado haupo kwenye jamii.

Kwenye nchi za Ulaya ambapo kwa kiwango kikubwa wameondokana na mfumo dume, wasichana wanamaliza highschool na vyuo vikuu kwa viwango vikubwa vya idadi na ufaulu wa juu kuliko wavulana proving kwamba competence haiko tied to jinsia. Na huko wanawake hawahitaji misaada, mifumo rasmi ya usaidizi wa kijamii iko sawa kwa wanaume na wanawake.
Let get rid of gender equality illusion. With no malice to anyone, ukiwaweka mwanaume na mwanamke wa daraja moja kwenye fair competing ground, competence ya mwanamke ipo chini. Namba hazidanganyi angalia top elites kwenye kila nyanja mfano matajiri, wanasayansi, madaktari bingwa n.k utaona ni jinsia gani.
Tukirudi kwenye mada: Saidia mtu ambaye ana uhitaji bila kujali jinsia yake.

Ukiwa na gari, ni uamuzi wako nani wa kumpa lift.

Kwangu nitampa mwanamke kwa sababu kuna uwezekano mkubwa anasubiriwa kuhudumia watoto nyumbani hata baada ya kutoka kazini au kwenye majukumu mengine au hata hapo alipo, inawezekana amebeba mtoto tumboni kwake na sijui.

Pia kuna uwezekano wa mwanaume kunidhuru sababu wengi wenu mna nguvu za mwili kutuzidi, kwahiyo kumsaidia lazima nijihakikishie kwanza kama nitakua salama!
Kwanza mfano wa lifti niliutumia tu kujumuisha vikwazo tunavyokutana navyo kila siku. Ulichoongea ni sawa kwa mtazamo wako, lakini lazima tukubaliane kwamba suala la kumpa kipaumbele mwanamke halafu kumbebesha majikumu mwanaume halina mtililiko wa kimantiki. Kuna point tutafika huyo mwanaume aliepuuzwa atashindwa kubeba majukumu na mwanamke aliepewa kipaumbele atakataa kubeba hayo majukumu maana social constraints zimemuaminisha sio wajibu wake. Kwahiyo tuchague moja, ni either tutoe usawa wa kijinsia na majukumu yabebwe kwa usawa pia au anaepewa kipaumbele abebeshwe majukumu makubwa zaidi.
 
Shida ni ukijibiwa kwa hoja unaruka viunzi. Haya tujipambanue kwenye jibu lako.
Let get rid of gender equality illusion.
Why is gender equality an illusion?
With no malice to anyone, ukiwaweka mwanaume na mwanamke wa daraja moja kwenye fair competing ground, competence ya mwanamke ipo chini.
Ni lini na wapi wanawake na wanaume wamewekwa kwenye daraja moja na ikadhihirika competence ya mwanamke iko chini? Naomba hizo data na takwimu.

Mimi nimekupa mfano wa nchi za EU ambapo miaka ya karibuni equality ya gender imeadvance kidogo na wasichana wanaongoza kumaliza elimu ya juu ya sekondari, elimu ya vyuo vikuu na ajira mpya makazini.

Screenshot 2026-02-02 at 16.45.33.png

Source 1 > Source 2

Namba hazidanganyi angalia top elites kwenye kila nyanja mfano matajiri, wanasayansi, madaktari bingwa n.k utaona ni jinsia gani.
Top elites wa sasa ni zao la mfumo wa miaka ya nyuma ambao wanawake hawakuwa na haki sawa wala fursa kama wanaume.

Tuchukulie mfano wa nchi inayozalisha matajiri wengi duniani - Marekani, mwanamke hakuweza kuchukua mkopo wake binafsi wa kukuza wala kuanzisha biashara bila saini ya mwanaume mpaka mwaka 1974. Vyuo vikuu bora vya Ivy league vilivyotoa wabobezi na wavumbuzi wengi wa kisayansi havikuanza kuruhusu wanawake kusoma mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Wewe ukiangalia elites waliofanikiwa na kuwalinganisha kijinsia huwa unatumia vigezo gani?
Kwanza mfano wa lifti niliutumia tu kujumuisha vikwazo tunavyokutana navyo kila siku. Ulichoongea ni sawa kwa mtazamo wako, lakini lazima tukubaliane kwamba suala la kumpa kipaumbele mwanamke halafu kumbebesha majikumu mwanaume halina mtililiko wa kimantiki. Kuna point tutafika huyo mwanaume aliepuuzwa atashindwa kubeba majukumu na mwanamke aliepewa kipaumbele atakataa kubeba hayo majukumu maana social constraints zimemuaminisha sio wajibu wake.
Sijaona kipaumbele chochote anachopewa mwanamke ambacho hakipo kwa sababu za kimazingira au kisheria. Kama hicho kipaumbele kipo naomba uniainishie.

Kwenye mahusiano;
watu wafanye wanavyoona, kama unataka patriarchal system, ishi humo, kama unataka equality na kusaidiana basi fanya hivyo.
Kwahiyo tuchague moja, ni either tutoe usawa wa kijinsia na majukumu yabebwe kwa usawa pia au anaepewa kipaumbele abebeshwe majukumu makubwa zaidi.

Tukisema usawa, basi pande zote zisiwe selective.
  1. Mwanamke abebe majukumu yake ya kiuchumi na achangie kwa usawa gharama za matumizi ya familia na kimaendeleo.
  2. Mwanaume abebe majukumu yote ya malezi ya watoto na kazi zote za nyumbani na zile za kijamii kwa usawa.

Shida huwa inaanza pale pande zote mbili zinapotaka kuchagua majukumu na wajibu ule unaowapendeza tu na mengine kuyaacha.
 
Shida ni ukijibiwa kwa hoja unaruka viunzi. Haya tujipambanue kwenye jibu lako.

Why is gender equality an illusion?
Mwanaume na mwanamke wametofautiana kibailojia, saikokojia, physique mpaka expectations za jamii kwaiyo outcome yao haiwezi kuwa sawa. Gender equality is an illusion.
Ni lini na wapi wanawake na wanaume wamewekwa kwenye daraja moja na ikadhihirika competence ya mwanamke iko chini? Naomba hizo data na takwimu.
Nimekupa kazi ya kuangalia top elites kwenye kila eneo uone ni jinsia gani. Mchukue mfano Mark Zuckerberg na Alon Musk hawa wana madada. Jiulize kwanini dada zao hswakufika viwango vyao wakati wote wamelelewa kwenye daraja moja la kimaisha?
Mimi nimekupa mfano wa nchi za EU ambapo miaka ya karibuni equality ya gender imeadvance kidogo na wasichana wanaongoza kumaliza elimu ya juu ya sekondari, elimu ya vyuo vikuu na ajira mpya makazini.

View attachment 3538025
Source 1 > Source 2
Kuna favouritism au qualifications downgrading huwa inafanyika upande wa mwanamke ili ku-stabilize uwiano wa namba baina yake na mwanaume. Proffesional yangu inahusiana na masuala ya takwimu najua kuna invisible factors huwa haziwekwi kwenye takwimu kwaiyo sometimes takwimu zinaweza zisihakisi uhalisia uliopo ground.
Top elites wa sasa ni zao la mfumo wa miaka ya nyuma ambao wanawake hawakuwa na haki sawa wala fursa kama wanaume.

Tuchukulie mfano wa nchi inayozalisha matajiri wengi duniani - Marekani, mwanamke hakuweza kuchukua mkopo wake binafsi wa kukuza wala kuanzisha biashara bila saini ya mwanaume mpaka mwaka 1974. Vyuo vikuu bora vya Ivy league vilivyotoa wabobezi na wavumbuzi wengi wa kisayansi havikuanza kuruhusu wanawake kusoma mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1960.
Mwaka 1974 mpaka kufikia mwaka 2026 ni gap ya miaka 52. Hata ukienda na age group hiyo bado wanawake wapo chini
Wewe ukiangalia elites waliofanikiwa na kuwalinganisha kijinsia huwa unatumia vigezo gani?
Umri pamoja na uwiano wa daraja la kimaisha walilotoka. Maana hauwezi kumfananisha fetma dewji na vunjabei. Offcourse fetma atampita vunjabei kwa sababu ya class za familia walizotoka.
Sijaona kipaumbele chochote anachopewa mwanamke ambacho hakipo kwa sababu za kimazingira au kisheria. Kama hicho kipaumbele kipo naomba uniainishie.
Viti maalumu kwa ajiri ya wanawake bungeni, sheria ya ndoa na talaka ambayo inamlinda zaidi mwanamke n.k
Kwenye mahusiano; watu wafanye wanavyoona, kama unataka patriarchal system, ishi humo, kama unataka equality na kusaidiana basi fanya hivyo.viti

Tukisema usawa, basi pande zote zisiwe selective.
  1. Mwanamke abebe majukumu yake ya kiuchumi na achangie kwa usawa gharama za matumizi ya familia na kimaendeleo.
  2. Mwanaume abebe majukumu yote ya malezi ya watoto na kazi zote za nyumbani na zile za kijamii kwa usawa.

Shida huwa inaanza pale pande zote mbili zinapotaka kuchagua majukumu na wajibu ule unaowapendeza tu na mengine kuyaacha.
Majukumu ya mwanaume yapo wazi ambayo ni provision and protection na hayajabadilika tangu enzi na enzi, ni wanawake wa kisasa ndio hamjui mnataka nini. Mnataka kuwa complimentor au competitor wa mwanaume? . Huwa mnabadilika badilika kimsimamo kwa kuangalia masilahi yapo upande upi kati ya patriarch au 50/50
 
Reply ndefu, hakuna data wala takwimu hata moja, ni opinions tu!
Anyway, ngoja niende na wewe mdogo mdogo.
Mwanaume na mwanamke wametofautiana kibailojia, saikokojia, physique mpaka expectations za jamii kwaiyo outcome yao haiwezi kuwa sawa. Gender equality is an illusion.
Gender equality ni fursa na usawa wa haki si kwamba mwanamke na mwanaume wanalingana kwa kila kitu.
Nimekupa kazi ya kuangalia top elites kwenye kila eneo uone ni jinsia gani. Mchukue mfano Mark Zuckerberg na Alon Musk hawa wana madada. Jiulize kwanini dada zao hswakufika viwango vyao wakati wote wamelelewa kwenye daraja moja la kimaisha?
Wana kaka pia, wana school mates, wana friends ambao ni wanaume, kwanini nao hawakufika kwenye viwango vyao na kuwa billionaires?

Sidhani kama kila mtu anaweza inventor na tajiri kama hao uliwataja.
Kuna favouritism au qualifications downgrading huwa inafanyika upande wa mwanamke ili ku-stabilize uwiano wa namba baina yake na mwanaume. Proffesional yangu inahusiana na masuala ya takwimu najua kuna invisible factors huwa haziwekwi kwenye takwimu kwaiyo sometimes takwimu zinaweza zisihakisi uhalisia uliopo ground.
Care for some proof? (kwa kuzingatia mfano wangu wa EU)
Mwaka 1974 mpaka kufikia mwaka 2026 ni gap ya miaka 52. Hata ukienda na age group hiyo bado wanawake wapo chini
Sheria zilibadilika ila mifumo ya kijamii huchukua muda kubadilika, je kuna significant progress ya wanawake toka 1974 au bado unaona wako vile vile?

Na inakuwaje ukawashindanisha wanawake waliopata haki zao 52 years ago na wanaume ambao walishakusanya wealth na kujenga structures kwa mamia ya miaka?
Umri pamoja na uwiano wa daraja la kimaisha walilotoka. Maana hauwezi kumfananisha fetma dewji na vunjabei. Offcourse fetma atampita vunjabei kwa sababu ya class za familia walizotoka.
Hizo ni individual cases, nimeuliza kijamii. Unalinganisha mafanikio ya jumla ya wanawake na wanaume kwa kwa lens ya kijinsia kwa kutumia vigezo gani?
Viti maalumu kwa ajiri ya wanawake bungeni, sheria ya ndoa na talaka ambayo inamlinda zaidi mwanamke n.k
Ulishafuatilia kujua kwanini tuna sheria inayoruhusu nafasi maalum kwa wanawake? Unafahamu ni kwanini ipo?
Sheria ya talaka na ndoa inawalinda wanandoa wote, toa mfano wa vifungu na kanuni zinazomfavor mwanamke!
Majukumu ya mwanaume yapo wazi ambayo ni provision and protection na hayajabadilika tangu enzi na enzi, ni wanawake wa kisasa ndio hamjui mnataka nini. Mnataka kuwa complimentor au competitor wa mwanaume? .
Mazingira yamebadilika, hatuhitaji protection kwa sababu hatuishi misituni kwenye wanyama wakali anymore. Tunaweza kuprovide sababu ya elimu na ajira, maisha yanataka tuevolve na kwa kawaida kundi ninaloshindwa kuendana na mabadiliko ya evolution, nature huwa inalitupilia mbali.

Mimi siamini kwenye competition ya kijinsia, naamini kwenye cooperation, kwamba tutashirikiana na kusaidia kulingana na strength na weakness zetu.
Huwa mnabadilika badilika kimsimamo kwa kuangalia masilahi yapo upande upi kati ya patriarch au 50/50
Nimetoa mfano wa usawa na majukumu, je mkitaka wanawake walipe kodi za nyumba na ada za watoto kwa sababu wana kipato kupitia makazini, na nyie mko tayari kufua nguo na kupika?
 
Gender equality ni fursa na usawa wa haki si kwamba mwanamke na mwanaume wanalingana kwa kila kitu.
Ndio illusion ninayoiongelea hiyo. Kimantiki hauwezi kuwaweka kwenye identical standard watu waliotofautiana almost kila kitu. Tumia busara kwa kuangalia nani anastahili zaidi wapi. Pamoja na hiyo haki sawa bado wanawake hawapelekwi vitani frontline, unafikiri ni kwanini? Mwanamke na mwanaume wapewe haki sawa kwenye elimu na ajira halafu jukumu la kulipa bill na kuboresha maisha ya mwenzake libebwe na mwanaume unaona kuna mzani wa kimantiki hapo?
Wana kaka pia, wana school mates, wana friends ambao ni wanaume, kwanini nao hawakufika kwenye viwango vyao na kuwa billionaires?

Sidhani kama kila mtu anaweza inventor na tajiri kama hao uliwataja.
Tunaangalia top elites kijinsia, yaani mwanaume na mwanamke. Sheria zimeshabadilishwa kuwekwa usawa wa kijisnia almost miaka 60 iliyopita. Kwanini bado hakuna wanawake kwenye list za top elites?
Care for some proof? (kwa kuzingatia mfano wangu wa EU)

Sheria zilibadilika ila mifumo ya kijamii huchukua muda kubadilika, je kuna significant progress ya wanawake toka 1974 au bado unaona wako vile vile?

Na inakuwaje ukawashindanisha wanawake waliopata haki zao 52 years ago na wanaume ambao walishakusanya wealth na kujenga structures kwa mamia ya miaka?
Sio kweli kwamba matajiri tulio nao walikua tayari washajilimbikizia mali. Ukichukua list ya matajiri wote miaka 52 iliyopita hawakuwa matajiri. Bezos alikua bado fukara tu, bill gate alikua bado anasoma, mark zuckerberg nafikiri alikua bado hajazaliwa kabisa, musk alikua na miaka miwili tu. Wengi wao wamejenga himaya zao from scratch katika zama hizi hizi za usawa wa kijinsia. Ndipo hapo nikauliza mbona wanawake hawapo kwenye top elites wakati kuna fursa sawa kwa wote
Hizo ni individual cases, nimeuliza kijamii. Unalinganisha mafanikio ya jumla ya wanawake na wanaume kwa kwa lens ya kijinsia kwa kutumia vigezo gani?
-Top elites kwenye kila nyanja ni jinsia gani
-jinsia ipi inatatua changamoto za kijamii mfano kubuni na kutengeneza teknolojia za usafiri kama magari na ndege, kugundua chanjo na dawa za magonjwa n.k
Ulishafuatilia kujua kwanini tuna sheria inayoruhusu nafasi maalum kwa wanawake? Unafahamu ni kwanini ipo?
Unataka kuhalalisha mbeleko? Whatever it is, ukishapewa mbeleko that's means you didn't earn it.
Sheria ya talaka na ndoa inawalinda wanandoa wote, toa mfano wa vifungu na kanuni zinazomfavor mwanamke!
Mgao wa mali na divorce alimony in most cases huwa inamuumiza mwanaume kwa sababu ndie anakuaga mwenye uwezo mkubwa zaidi ya mwanamke. Sioni mantiki yoyote ya mgao wa mali na divorce alimony katika zama hizi za usawa wa kijinsia maana hapo ni kama mwanaume analipia gharama ya laziness/incompetence ya mwanamke. Umepewa fursa zote kama mwanaume ukashindwa kutafuta vyako how comes upewe alichotafuta mwanaume?
Mazingira yamebadilika, hatuhitaji protection kwa sababu hatuishi misituni kwenye wanyama wakali anymore. Tunaweza kuprovide sababu ya elimu na ajira, maisha yanataka tuevolve na kwa kawaida kundi ninaloshindwa kuendana na mabadiliko ya evolution, nature huwa inalitupilia mbali.
Ndio siasa zenu hizi feminists, ila mkikwama mnakua soft na kumkimbilia mwanaume awatatulie matatizo yenu. Women are aleays strong and independent until it comes a time to face accountability

Nimetoa mfano wa usawa na majukumu, je mkitaka wanawake walipe kodi za nyumba na ada za watoto kwa sababu wana kipato kupitia makazini, na nyie mko tayari kufua nguo na kupika?
Kama wote mnaenda kazini basi kwa kazi za nyumbani mnaweza kuajiri housegirl, lakini mwanamke uende kazini halafu usijumuishwe kwenye ulipaji bill, sasa kipato chako unakipeleka wapi.

Traditional roles kama kupika na kufua hautaweza kuzifanya kwa sababu unaenda kazini halafu bill usilipe kwa sababu wewe ni mwanamke, sasa utakua na output gani kwenye hiyo ndoa?

Umeluka luka weeeee hatimaye umekuja ku-expose ubinafsi wenu wanawake.
 
Back
Top Bottom