Ewe kijana/baba/mzee, kama una nafasi moja ya kutoa msaada. Msaidie mwanaume

Mleta mada una tatizo sehemu pole sana. Anyway wanawake sio chanzo cha matatizo yako bali destiny na fate havipo upande wako.
Kwa average ya maisha ya vijana kibongo bongo naweza nikasema nipo kwenye uelekeo mzuri kwenye karibu maeneo yote.

Suala la elimu tangu primary nilikua nashika namba za juu darasani. Sekondary olevel ninesoma azania sekondary pale magomeni na alevel ninesoma mzumbe morogoro uko kote tayari nishakichafua sana. Chuo nime-graduate kazi ya economics and finance sio kwa kupata first class tu, but first class with honors.

Suala la mahusiano nipo njema. Nimeoa. Mimi na mke wangu tuna mtoto mmoja wa kiume ambae kwa sasa ana mwaka mmoja na miezi miwili. Hakuna migogoro nyumbani kwangu.

Nikiwapa vijana miongozo ya standard za kuzingatia wakati wa ku-settle na mwanamke haimaanishi kwamba kwangu kunawaka moto. Najaribu tu kuwapa muongozo kwa sababu mimi kama mmoja wa kijana ambae nime-dedicate maisha yangu kuwainua vijana wenzangu naona changamoto wanazopitia na wengi washakuja kuniomba msaada, kwa mantiki najiona nawajibika kuwaongoza ambao bado hawajayatimba

Suala la kipato nipo njema pia. Nilishafanya kazi moja ya benki kubwa hapa bongo kama business banking officer.

Niliacha kazi benki baada ya kupata ofa nzuri zaidi Delloite kama statistic analyst officer.

Niliacha kazi Delloite pia baada ya kupata ofa nzuri zaidi USAIDS kama financial suporvisor. Nikafungua kampuni yangu ya masuala ya auditing na baadae nikacha kazi USAID'S ili nielekeze mkazo zaidi kwenye kamouni yangu.

Kampuni inafanya vyema na nimeajiri vijana kadhaa. Kwahiyo sipo katika phase ya kuhitaji msaada wa kuinuliwa kimaisha. Nawaongelea madogo na vijana waliokwamba. Mimi mwenyewe nipo njema.
 

Nakuomba data, takwimu na vifungu vya sheria vya unayoyazungumza naona unaruka ruka. Utakapokuja na facts tutaendelea, ngoja nikuache na mambo mawili!
  1. Ukiona huu mfumo uliotengenezwa na wanaume wenzako haukunufaishi au unakukandamiza, basi fanyia kazi kuubadilisha. Sisi wengine tulishaanza jitihada za kuachana nao kitambo sana.

  2. ZINGATIA: In evolutionary science kuna rule kwamba "species or animals that are not well adapted to their environment are less likely to survive and reproduce". Ni suala la muda tu, iwe ni mwanamke au mwanaume, ukishindwa kuadapt na uhalisia wa mazingira yanayokuzunguka, kizazi chako au kundi lako litaangamia.

    Tuishi humo kwa sasa!
 
Kusaidiana ni jambo muhimu Sana ila pia kuna viwango vya kusaidia

Kwa mfano Natafuta Ajira nikuulize ikitokea Leo nimemsaidia mwanaume halafu Kesho nikakutana na mwanamke mwenye tatizo kama lile alikuwa nalo mwanaume niliyemsaidia Jana,je nikimsaidia huyo mwanamke nitakuwa nimekosea kweli?

Mi nadhani kama mtu upo katika nafasi ya kutoa Masada kwa wenye uhitaji saidia tu bila kujali jinsia zao
 
Unataka data gani sasa. Nikwambie tofauti za kibailojia baina ya mwanamke na mwanaume ambazo haiwezekani wakawa sawa? Unataka data kwenye mambo ambayo yanaonekana? Angalia divorce inawaumiza jinsia gani? Angalia top elites kwenye kila nyanja ni jinsia gani? Unataka data gani sasa hapo.

Shida yenu wanawake mnapenda sana kudanganywa ndio maana inakua rahisi feminism kuwauzia illusions. Baada ya kujiuliza "what is this?" nyie mnataka kulazimisha iwe "what this should be"
 
Nimesema kama una nafasi moja mpe kipaumbele mwanaume. Sio vibaya kumsaidia yoyote lakini utilization ya msaada wako itakua kubwa zaidi kama ukimsaidia mwanaume kwa maana mwanaume akisimama ndie anabebeshwa majukumu na hata yeye mwenyewe anakubali kuyabeba bila shida. Tofauti na mwanamke akisimama yeye ni mbinafsi kidogo chake ni chake, cha mwanaume ni cha wote.

Unafikiri ni kwanini mwanamke na mwanaume wenye kipato cha milioni 2 inakua ni rahisi kwa mwanaume kuoa lakini ni ngumu sana kwa mwanamke kuolewa? ni kwa sababu mwanaume hana tatizo kuoa mwanamke mwenye kipato kidogo zaid yake au ambae hana kipato kabisa, na kuna maelfu ya wanawake hao mtaani. Upande wa mwanamke kuolewa na mwanaume mwenye kipato cha chini au ambae hana kipato kabisa ni bora abaki kuwa single. Atataka mwanaume mwenye kipato cha milioni 3 na kuendelea na vijana wa kiume wenye vioato vya milioni 3+ ni wachache sana miongoni mwa vijana.

Tukisema tuangalie hoja kimantiki tutaona kumpa kipaumbele mwanaume kuna mtililiko wa kimantiki kwa sababu ndie atabebeshwa majukumu, lakini 50/50 au kumpa kipaumbele mwanamke hakuna mtililiko wa kimantiki coz at the end a woman will be looking for a man to offload her financial and living responsibility to. What a reason to empower a woman to be able to make maney like a man if at the end a man should pay all bills? poor utilization if fund and opportunity.
 
Story ya mvua hapo juu imenikumbusha Mabibo wakati fulani way back 2003 huko kipindi kile Dar daladala vi-Hiace walipanda mwanamke mjamzito na jamaa mmoja ana magongo amevaa P.O.P means mguu ulivunjika.

Kuna jamaa aliamua asimame mgonjwa (mwanaume) akae but yeye akajisogeza na magongo yake akimuashiria yule mwanamke akae,wakati mwengine kuna vitu vya hovyo kabisa tunavifanya wanaume havina hata mana hii mada ndiyo imenipa wasaa wa kutafakari lile tukio kwamba kwanini mule kwenye gari hakusimama mwanamke mwenzake na yule mwenye mimba ampishe kwa sababu na yeye anaujua uchungu wa kubeba mimba?
 
Na hii ndo inasababisha wanaume wengi kujizira na kujikana na kuamua kuwa mashoga ili kurahisha wepesi wa maisha

Maana mwanaume akishakuwa shoga tyari kawa mwanamke Kila huduma anayotaka atapata kirahisi maana atakuwa amevaa sketi, gauni na kujipodoa kama wa kike, Kwa maana hiyo basi atakae jaa kwenye mfumo atamchukua shoga na kumlipia huduma zote akijua ni mwanamke kumbe dume

Mwisho wa siku na huyo shoga atakuwa ametimiza malengo ya kupata vya mserereko kama mwanamke kweli kumbe dume

Na Kwa mtindo huu ushoga ndo unaongezeka na hautakaa uishe, Yani idadi kubwa ya wanawake inazidi kuongezeka.
 
Tumeamua kupuuza magumu anayopitia boy child sio kwa sababu hatuwezi au hatuoni mantiki ya kumsaidia, isipokua ni kwa sababu yeye ni mwanaume.

Halafu scenerio uliyoiongelea inaonyesha kwamba hata wanawake hawapo tayari kusaidia wenyewe kwa wenyewe. Mwanamke mwenzao akikutana na changamoto wazo lao la kwanza ni kwamba atasaidiwana mwanaume. Hii kitu ni kweli ipo kwenye jamii.
 
Ushoga ni topic nyingine inayohitaji tafakuri yake binafsi. Zipo sababu nyingi za kumfanya kijana wa kiume kuwa shoga mfano hitilafu kwenye mfumo wa homoni, makuzi especially shule za bweni, kufuata mkumbe, childhood trauma n.k. Steve Jobs, ambae ni founder wa kampuni inayotengeneza bidhaa za apple kama simu, komputa n.k alikua shoga usiniambie huyu alikua mvivu au masikini ndio maana akawa shoga kupata shortcut ya maisha.

Ngoja nikueleze mkasa wangu mmoja hivi takribani miaka miwili iliyopita. Kuna wakati nikioanga katika nyumba ambayo nje ya geti kuna kibalaza. Siku moja narudi home usiku wa majira ya saa kumi nikamwona mtu kalala kwenye kibaraza pale nje ya geti. Nikafikiri labda ni mlevi kaangushia gari hapo nikasema akiamka asubuihi ataondoka nikaingia zangu mdani.

Kesho yake usiku majira ya muda ule ule narudi nyumbani kwenye kutoka kwenye pilika pilika za wikiend namwona tena yule jamaa kalala nje. Safari hii nikamuamsha nikamuuliza kwanini analala hapo na nimemuona tangu jana.

Maelezo aliyonipa ni kwamba hana makazi ya kuishi. Ndani kwangu kuna chumba kidogo nje ambacho akitumiki. Hakina umeme na kitasa mlangoni lakini dirisha lina nyavu kibishi bishi mtu yoyote anaweza akalala tu. Nikampa pamoja na godoro na shuka mbili nikampa kipindi cha miezi mitatu alale hapo wakati anatafuta kibarua chochote cha kumwezesha kupata sehemu ya kuishi.

Alitengeneza urafiki na vijana wenzake pale mtaani wakaanzisha kijiwe cha kuosha magari. Alikaa kwangu kwa takribani miezi miwili na nusu akaja kuniaga amepata geto mtaa wa pili. Je mimi kumsaidia yule kijana nitamu-influence vipi kuwa shoga?
 
Asili inamlinda sana mwanamke. Ndio maana ukiwa unaendesha Gari, Saa nane usiku, ukakutana na mwanamke anakuomba lifti. Unaweza kusimama ukampakia.

Lakini Saa nane usiku, umkute mwanaume mwenzako anakuomba lifti, Hata wewe mleta mada husimami ng'oo.

Tena ndio unaongeza speed kabisa.

Nature favors women.

Time favors men.

Muda hauna huruma kwa mwanamke. Ndio maana kuoa mwanamke wa miaka 30+ ni ngumu. Ila asili inamlinda mwanamke popote pale.

Asili haina huruma kwa mwanaume. Ndio maana huwezi kupewa lifti saa nane usiku. Utakomaa mwenyewe.
 
Kabisa naaipaswi wote tuwe sawa , na hapo wala hakuna mjanja zaidi ya mwingine ni aina ya maisha tu
Pamoja na kwamba tunatofautiana bado kuna umuhimu wa kuwekeana miongozo ili kuwepo na mzani katika interactions zetu. mfano, binadamu tumetofautiana physique sasa tukisema tuwaache mwenye nguvu na asie na nguvu wa-activate jungle mode zao katika kumaliza tofauti zao bila shaka yule asie na nguvu atapata tabu sana ndipo hapo unakuja umuhimu wa kuwawekea sheria za kuwaongoza.

Tukija kwenye mlengo wa nilichokiongea kwenye mada yangu. Sija-base kwenye usawa wa kijinsia, nime-base zaidi kwenye logic. Ukweli ni kwamba tunapigia chapuo usawa wa kijinsia lakini outcome ya mwanaume kunyanyuka ni tofauti na ile ya mwanamke.

Mwanaume akinyanyuka atasuluhisha matatizo, mwanamke hata akinyanyuka bado atatafuta mwanaume wa kumsuluhishia matatizo yake.
 
Ukimuinua mwanamke , umeinua dunia , kwa sasa wanawake walivyotelekezewa watoto na wanapambana mwenyewe, ukiwasaidia unasaidia kizazi kijacho.
 
Nalitambua hilo msingi wa hoja yangu ni kuitoa akili nje ya box. Sio kila situation mwanaume ataweza kui-defeat asili, sasa hapo ambapo anakwama kama unaona kuna kitu unaweza ukasaidia wewe saidia tu usilete complications nyingi
 
Ukimuinua mwanamke , umeinua dunia , kwa sasa wanawake walivyotelekezewa watoto na wanapambana mwenyewe, ukiwasaidia unasaidia kizazi kijacho.
Ukimuinua mwanaume automatically utapunguza namba ya hao fatherless kids from the first place. Single mother epidemic ya kwenye jamii ya sasa ni moja ya consequences za feminism.
 
Ukimuinua mwanaume automatically utapunguza namba ya hao fatherless kids from the first place. Single mother epidemic ya kwenye jamii ya sasa ni moja ya consequences za feminism.
Mwanaume ajiinue mwenyewe , hata maumbile yetu yapo katika muundo wa kujipambania mwenyewe kiasili kabisa
 
Mwanaume ajiinue mwenyewe , hata maumbile yetu yapo katika muundo wa kujipambania mwenyewe kiasili kabisa
Sio kweli kabisa, mwanaume pia anakutana na magumu na kukosa suluhisho. Binafsi kuna vijana wenzangu nishawasaidia sana.

Hapa jf kuna kijana kule kwenye jukwaa la biashara niliona anaomba partner wa biashara ataetoa hela ili kununua vifaa fulani hivi vya kuongeza uzalishaji. Vifaa alivyokua anahitaji then watagawana faida baada ya mauzo. Mimi nilikua navyo hivyo vifaa stoo kwa sababu kuna kipindi nilitaka kufanya ile biashara ila nikakosa muda. Nikamwambia yule kijana aandae hela ya usafiri aje nyumbani kuvichukua. Gharama ya vile vifaa ni milioni 1.8 lakini nilimpa bure kabisa bila kunilipa hata shilingi moja.

Wapo vijana ambao nishawasaidia makazi, hela ya kujikimu, chakula, ajira, mtaji, vifaa vya michezo, vyombo vya mziki na mengi ambayo nimeshasahau, na nitaendelea kuwasaidia zaidi kadili uwezo wangu unapoishia

Kama unaona ni sawa kumoa kipaumbele mwanamke ni it's ok haujavunja sheria yoyote. Ni matumaini yangu utakapokutana na changamoto wanawake pia watakukimbilia kukusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…