Ewe Mkristo, nani alikwambia kukusanyika kila Jumapili kwa ajili ya Ibada?

Kutokufungwa na SHERIA ndo kubadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada Kutoka Siku ya Saba ya juma (Jumamosi) kwenda siku ya Kwanza ya juma (jumapili)?
Mkuu,soma wakolosai2:16 utaelewa kuwa muhimu Ibada ifanywe kwa viwango vya Mungu haijalishi ni siku gani
 
Rabbon

Wakolosai 2:16-17

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
 
Rabbon

Wakolosai 2:16-17 SRUV​

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Ndiyo hivyo mkuu,halafu zile SHERIA za kushika sabato walipewa taifa la Israeli tu sio wakristo,mtoa mada aelewe wakristo walianza baada ya Yesu kubatizwa kuwa Kristo,lile taifa la Israeli hawakuwa wakristo
 
chalula kigumu hiki, tuanzishie uji mkuu.
 
Salam, Shalom!!

Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili kama siku kuu ya IBADA badala ya Jumamosi iliyovyokuwa awali?

Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,

Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.

Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.

Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili kama siku kuu ya ibada takatifu badala ya Jumamosi?

Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?

Ni nani aliyebadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada Kutoka Siku ya Saba ya juma, kwenda siku ya kwanza ya juma,jumapili?

Ni nani aliyekuagiza kusherehekea sikukuu ya Christmas tarehe 25 December?
Unalo andiko?

Ni maagizo ya Roho mtakatifu kufanya mambo hayo?

NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.

ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.

SOURCE: OLE... MNAOTETEA JOKA KUABUDU JUMAPILI- UTUBE VIDEO, UNYAKUO TV.

Karibuni.[emoji120]
Swali hili linawahusu Wakristo wa Iran, Iraq, na nchi nyingine za Kiarabu na Kiislam pia?

Vv
 
Rabbon

Wakolosai 2:16-17

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Umeangalia u tube video nilokutumia?
 
Ufunuo 1:10
"Nalikuwa katika roho, Siku ya Bwana"

Kuna Siku ya Bwana Yesu ( ya ufufuo), na Siku Musa (sabato), wakristo tumefanya maamuzi

Kwa kusema hivyo sipingi makusanyiko ya kila Siku, Ila kuna Siku ya kusanyiko kuu, Mfalme Daudi aliliita kusanyiko makini, kwa wakristo Ni Siku ya Bwana wao " Lord's day" ndio maana hata michango na kumega mkate kulifanyika Siku hiyo

Kwa wayahudi na wengine wanaomkataa Yesu sabato inaendelea huku wakimsubiri masihi!!!
 
Hiyo siku ya BWANA katika ufunuo mbona haikutajwa?

Unajua makusanyiko ya IBADA jumapili yameanza Karne ya 4?

Hujiulizi kwanini mitume wote hawakuwahi kubadili?
 
Yn 20:19
"Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu."

Unaweza kuonyesha na wewe wanafunzi wa Yesu walikutanika Siku ya sabato? Au Yesu akawatokea Siku ya sabato, au Siku ya sabato walimega mkate?

Hayo mambo ya Karne ya nne Ni hadithi za wasabato, mbona biblia Ipo wazi?
 
Yn 20:19
"Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu."

Unaweza kuonyesha na wewe wanafunzi wa Yesu walikutanika Siku ya sabato? Au Yesu akawatokea Siku ya sabato, au Siku ya sabato walimega mkate?
Rudi kwenye historia,

Mitume na manabii hawajawahi Badili Ibada Toka Jumamosi kwenda jumapili.

Hizo mambo wameanzisha watumishi Karne ya 4.
 
Achana na historia, rudi kwenye maandiko, Kama unaamini kwamba biblia ndio mamlaka pekee ya neno la Mungu, sio hizo hadithi za kizee zinazobadirika kila Siku kwa jina la historia
 
Rudi hapo juu, nimeweka Video Kutoka U-Tube Kuna ushuhuda wa maelekezo ya Mungu.
 
Angalieni Leo kusanyiko Takatifu la Agano Jipya.
Kawe kwa Mwamposa.

Nyie watakatifu Wasabato msubiri siku ya Jumamosi.
Siku ya Saba ya Juma.

"Vipofu wanaona, viwete wanatembea, heri yenu msio na mashaka nami"

Mathayo (Mat) 18:20
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

Roho Mtakatifu hapa alikosea
Angesema wakusanyikao siku ya kwanza ya Juma. Siku ya Jumamosi ndio nitakuwa katikati yao.

Luka 7
20 Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

21 Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.

22 Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.

23 Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.

Hapa Yesu alikosea, angesema wakusanyikao siku ya Jumamosi ndio nitakao waponya.

Luka 8
9 Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo?

10 Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.

Luka 7
31 Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini?

32 Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.

Nilisahu kumbe Roho Mtakatifu anasikia maombi ya Jumamosi tu.

Huyu anafanana na Allah, anayesikia lugha ya Kiarabu tu.

Tulia, Jitakari, chukua hatua Leo.
 
Alicho fanikiwa Bibi Ellen G. White ni kutengeneza kundi linalo wachukia wa Roman Kathori na wengine.

Waromani hawana chuki kabisa kwa Wasabato.
Ila Wasabato kila Jua likichomoza kazi Yao kuu ni kuwadhihaki Waroma.

Hawana habari na Dini ya Shetani, wala Freemasonry, wala Wahindu na Wabudha.

Hao wote ni watakatifu kwa Wasabato, Chuki ya Wasabato ni kwa Waroma tu Basi.

Wamesahau kutubu dhambi zao, wamesahau kujiona wenye dhambi,
Wamesahau kuhubiri Injiri ya Kristo.

Wao Kitabu chao ni cha Daniel tu, na Ufunuo wa Yohana.

Kwao wenye dhambi ni Wakatoriki tu Basi.
 
Yesu alishuka Duniani ili awaokoe Waroman Katoriki, kwakuwa ndio wenye dhambi kuu hapa Duniani.

Kungekuwa na Wasabato tu na Freemasonry na Wabudha na Wahindu na wa Ratafarian na Wamomoni, Yesu asingeshuka Duniani.
Hao wote ni watakatifu sana, Kanisa la Unyakuo

Nawatakia Safari Njema ya Mbinguni Wasabato.
Maana mmetakasika na hamna dhambi yoyote.
Na mmekuwa kundi pekee Takatifu lisilo na mawaa ya hii Dunia.

Endeleeni kuwadhihaki Waromani maana Wana dhambi nyingi sana.
Kama dhambi za Mtoza Ushuru.

Ufalme wa Mbingu ni wa Wasabato tu.
Wanaokusanyika siku ya kwanza ya Juma. Jumamosi
Na kuishika Sabato kwa kupumzika na kustarehe.
 
Ni Lini Yesu Kristo alikuagiza mkristo kukusanyika jumapili Kwa ajili ya IBADA Takatifu?
Utakuwa mgonjwa wa akili sio bure.
Ni wapi iliandikwa lazima iwe Jumspili?

Huu ni utaratibu tu na biblia inaruhusu mambo kufanyika kwa uzuri na utaratibu..
Rejea👇👇
Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

1 Wakorintho 14:40

Pili: sababu kuu ni kuwa Jumapili ni siku ya kwanza ya Juma.
Ni siku ya ushindi kwani Yesu alifufuka👇👇👇
Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.

Marko 16:9

Hitimisho; Sio lazima kusali Jumapili but ni utaratibu mzuri tu waliojiwekea wanadamu.

Mwisho; Siku haiwezi kukusaidia uende mbinguni bali matendo yako
 
Alicho fanikiwa Bibi Ellen G. White ni kutengeneza kundi linalo wachukia wa Roman Kathori na wengine.

Waromani hawana chuki kabisa kwa Wasabato.
Ila Wasabato kila Jua likichomoza kazi Yao kuu ni kuwadhihaki Waroma.

Hawana habari na Dini ya Shetani, wala Freemasonry, wala Wahindu na Wabudha.

Hao wote ni watakatifu kwa Wasabato, Chuki ya Wasabato ni kwa Waroma tu Basi.

Wamesahau kutubu dhambi zao, wamesahau kujiona wenye dhambi,
Wamesahau kuhubiri Injiri ya Kristo.

Wao Kitabu chao ni cha Daniel tu, na Ufunuo wa Yohana.

Kwao wenye dhambi ni Wakatoriki tu Basi.
Msabato ni mtumwa wa torati.
Ni watu wanalolitumikia andiko na sio Neno na kweli ya Mungu.

Andiko huua bali Neno la Mungu huponya
 
Salam, Shalom!!

Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili kama siku kuu ya IBADA badala ya Jumamosi iliyovyokuwa awali?

Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,

Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.

Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.

Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili kama siku kuu ya ibada takatifu badala ya Jumamosi?

Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?

Ni nani aliyebadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada Kutoka Siku ya Saba ya juma, kwenda siku ya kwanza ya juma,jumapili?

Ni nani aliyekuagiza kusherehekea sikukuu ya Christmas tarehe 25 December?
Unalo andiko?

Ni maagizo ya Roho mtakatifu kufanya mambo hayo?

NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.

ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.

SOURCE: OLE... MNAOTETEA JOKA KUABUDU JUMAPILI- UTUBE VIDEO, UNYAKUO TV.

Karibuni.🙏
Tumeamua na huna la kufanya. Tumekuwa tukifanya miaka yote ata kabla ya kahaba Ellen G White, na freemason Joseph Smith kupotosha. Sabato ya kristo sio sawa na sabato ya watesi wake wayahudi. Hamna akili. Karibu kitimoto roast na ndizi mbili, then Bata wa kushoto.
 
Back
Top Bottom