EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Ukinunulia madem hiyo savannaj moja kwa 5000 inaathiri vipi watu wengine, au inaathiri vipi vitu vingine, ukipandisha bei ya mafuta unaleta mfumuko wa bei za bidhaa muhim. Nenda shule kaka nyny ndio wale mnaopelekwa kama makondoo!!
Shule alienda lakini kuuza visheti sio kusoma usimlaumu ...shule alienda na nilikuwa namuona anauza visheti na barafu.
 
Kwamba mafuta yalikuwa ya importation ya march bei zikiwa juu LAKINI ndani tukauziwa bei nafuu..ila sasa duniani bei zimeshuka LAKINI ndani bei zimepanda !!?? Na diesel imekuwa bei zaidi ya Petrol!!? Umetumia principle Gani au theory Gani ya uchumi kuelezea haya!!??
 
Huu upumbavu sasa 😟😟😟😟
 
Hii ndo kazi wanayoiweza iwera kutangaza bei mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio bei kwenye soko WENDA ipo juu ila kwetu inakua juu Mara dufu kisa mitozo ya kijinga,

Hali ni mbaya Sana tuendako
 
January Makamba nakuita kwa jina lako futa hiyo bulk system ya uagizaji mafuta inachangia kwa kiasi fulani ni kama tuko enzi za ujamaa hapa acha watu washindane huwezi kuagiza kitu kimoja kwa bei moja utegemee soko liwe la ushindani. Mtaangamiza nchi ni hatari. Ni wakati wa kukaa na kujiangalia. Haya matangazo ya usiku mnaogopa nini?
 
Anaupiga mwingi
Hizi dalili za mfumko wa bei na wa ajabu tuliona mapema Sana ,tukauliza hum jf , wakaja wachumi uchwara na kuanza kuleta shule zao uchwara wanazoamini kupitia vyeti, Sasa kiko wapi , KWa speed hii lt itaenda fika elf 5000
 
Kazi ipo.

Yaani ndani ya mwezi mmoja bei imeongezeka kwa zaidi ya shilingi 800.

Huyu mama hana mbinu yoyote ya kukabiliana na mfumo wa bei, bando bei ghali, mafuta bei ghali, mshahara haiongezeki miaka 7.

Hii nchi sijui nani alituroga.
Alafu utawasikia wakisifia , ujinga ujinga tu
 
Mimi sitaki kutumia mihemuko katika hili, ni kweli mafuta yamepanda duniani jana ilikuwa karibia 106$ kwa pipa ni kweli lakini kuna mambo pia yanachangia katika hili. Moja huyo anayeshinda Bulk tender anakuwa kashinda kwa bei maalumu kwa maana aliyeshinda leo tender atasambaza miezi 3 iinayokuja sasa swali kwanini kusiwe na notice ya miezi mitatu kuwa aliyeshinda kwa sasa mafuta ya mwezi wa sita yatakuwa bei hii sababu nasema hivi mtu akija ku tender huku anakuwa kishiingia makubaliano ya supply ya miezi mitatu iweje tangazo lije usiku tu kesho yanapanda. Haya yaliyopanda ni lini yaliletwa? kuna rushwa kubwa katika mfumo wa uagizaji mafuta wa pamoja, Nilidhani kama kipindi kile wa kusema baada ya miezi mitatu bei itashuka kwa kiasi hiki sababu aliyeshinda tender kampuni ya TPDC wame tender bei ya chini sasa iweje jana usiku linakuja tangazo? Ni muhimu sasa kujuwa hizi tender wanashindaje? navyojuwa huwezi kushinda tender halafu ukaja kubadili bei njiani inakuwa tender yote batili. ulishinda kwa bei hii huwezi kubadili. Makamba lazima aje hadharani aelezee imekaaje hii.
 
Tunalipia madhara ya vita!!...

Halafu kuna watu wanasifia Urusi kuvamia nchi nyingine....
Mkuu Sasa wewe mbona kutosifia urusi kwako hakujapelekea Vita kukoma? Kwa akili zako unaamini kuisifia urusi ndo kunapekelea mafuta kupanda Bei,?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…