EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Ukinunulia madem hiyo savannaj moja kwa 5000 inaathiri vipi watu wengine, au inaathiri vipi vitu vingine, ukipandisha bei ya mafuta unaleta mfumuko wa bei za bidhaa muhim. Nenda shule kaka nyny ndio wale mnaopelekwa kama makondoo!!
Shule alienda lakini kuuza visheti sio kusoma usimlaumu ...shule alienda na nilikuwa namuona anauza visheti na barafu.
 
Kama ulisikiliza kipindi cha kipima joto kuhusu kupanda kwa bei ya walishaelezea mwezi wa tano bei zitaongezeka.

Sababu zilizotolewa ni za msingi kwa mfumo wa manunuzi, mafuta yanayotumika leo yalinunuliwa wakati bei ipo juu kidogo mwezi wa tatu.

All in all mfumo wa ‘bulk procurement’ inabidi waufanyie assessment una mazuri yake kwa upande wa serikali kuhakikisha wana uwezo wa ku control supply ni swala muhimu kwa usalama wa uchumi.

Alikadhalika una mapungufu yake kwenye procurement strategies, kununua kwa mwezi kuna wanyima waagiza advantage za price hedging.

Ukiwa reliable buyer unaweza strike long term deals za miezi sita ata mwaka (depending na muuzaji) kupata mafuta kwa bei za price ‘ceiling and floor’ bei zikipanda na kushuka chini ya bei za soko.

Kwa sasa Bulk procurement inazuia advantages hizo pamoja na ushindani wa biashara.

mfanyabiashara inakuwa ngumu kutumia average costing za inventory ajipe advantage sokoni kupambana na ushindani au kutumia mbinu zingine za kujipa advantage.

Unaweza elewa kwanini serikali iliamua kwenda na Bulk procurement kutokana na masahiba ya huko nyuma kushindwa ku monitor reserves and supplies; but surely inahitajika amendments kwenye supply control baada ya kuwasikiliza na kuwaelewa umuhimu wake lakini huu mfumo unaondoa ubunifu pia wa ushindani na kupata good deals sokoni.

Kuna mambo ya taasisi kufanya overlapping works na zenyewe zinategemea tozo za mafuta, serikali kujitwika mzigo wa investment kwenye mabomba ya kupokea mafuta wakati port inatumiwa na rwanda, Burundi, congo, Zambia ata wao mafuta yao yakija meli zao zina wa-charge demmurage za siku. So kuna investments ambazo na wao wanaweza changia bure it’s in their interest too.

Hii nchi ina mambo mengi vitu vingine ukisikiliza unashindwa kuelewa baadhi ya watu hizo nafasi wamezipata vipi, ukiwasikiliza hawana majibu kabisa ya changamoto za sector zao zaidi ya kuongelea mambo ya kukariri.
Kwamba mafuta yalikuwa ya importation ya march bei zikiwa juu LAKINI ndani tukauziwa bei nafuu..ila sasa duniani bei zimeshuka LAKINI ndani bei zimepanda !!?? Na diesel imekuwa bei zaidi ya Petrol!!? Umetumia principle Gani au theory Gani ya uchumi kuelezea haya!!??
 
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258

View attachment 2210381

Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022

Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.

Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa Dar, na kwa Tanga watanunua kwa Tsh. 3,264. Mtwara watauziwa kwa Tsh. 3,309 kwa lita.

Mafuta ya taa hayako nyuma ambapo bei ya lita kwa Dar itakuwa Tsh 3,112. Mikoa mingine itakuwa na bei kutokana na hesabu zitakvyofanyika.

EWURA wamesema mabadiliko ya bei katika soko la dunia yamesababisha 93% ya mabadiliko ya bei

Bei za Jumla
Port Petrol
(TZS/Litre)
Diesel
(TZS/Litre)
Kerosene
(TZS/Litre)
DAR ES SALAAM 3,015.88 3,125.18 2,980.56
TANGA 3,028.72 3,131.39 --
MTWARA 3,044.88 3,176.87 --

View attachment 2210436

View attachment 2210437

View attachment 2210438

View attachment 2210439

View attachment 2210440
Hii ndo kazi wanayoiweza iwera kutangaza bei mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258

View attachment 2210381

Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022

Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.

Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa Dar, na kwa Tanga watanunua kwa Tsh. 3,264. Mtwara watauziwa kwa Tsh. 3,309 kwa lita.

Mafuta ya taa hayako nyuma ambapo bei ya lita kwa Dar itakuwa Tsh 3,112. Mikoa mingine itakuwa na bei kutokana na hesabu zitakvyofanyika.

EWURA wamesema mabadiliko ya bei katika soko la dunia yamesababisha 93% ya mabadiliko ya bei

Bei za Jumla
PortPetrol
(TZS/Litre)
Diesel
(TZS/Litre)
Kerosene
(TZS/Litre)
DAR ES SALAAM3,015.883,125.182,980.56
TANGA3,028.723,131.39--
MTWARA3,044.883,176.87--

View attachment 2210436

View attachment 2210437

View attachment 2210438

View attachment 2210439

View attachment 2210440
Ndio bei kwenye soko WENDA ipo juu ila kwetu inakua juu Mara dufu kisa mitozo ya kijinga,

Hali ni mbaya Sana tuendako
 
January Makamba nakuita kwa jina lako futa hiyo bulk system ya uagizaji mafuta inachangia kwa kiasi fulani ni kama tuko enzi za ujamaa hapa acha watu washindane huwezi kuagiza kitu kimoja kwa bei moja utegemee soko liwe la ushindani. Mtaangamiza nchi ni hatari. Ni wakati wa kukaa na kujiangalia. Haya matangazo ya usiku mnaogopa nini?
 
Kazi ipo.

Yaani ndani ya mwezi mmoja bei imeongezeka kwa zaidi ya shilingi 800.

Huyu mama hana mbinu yoyote ya kukabiliana na mfumo wa bei, bando bei ghali, mafuta bei ghali, mshahara haiongezeki miaka 7.

Hii nchi sijui nani alituroga.
Alafu utawasikia wakisifia , ujinga ujinga tu
 
Mimi sitaki kutumia mihemuko katika hili, ni kweli mafuta yamepanda duniani jana ilikuwa karibia 106$ kwa pipa ni kweli lakini kuna mambo pia yanachangia katika hili. Moja huyo anayeshinda Bulk tender anakuwa kashinda kwa bei maalumu kwa maana aliyeshinda leo tender atasambaza miezi 3 iinayokuja sasa swali kwanini kusiwe na notice ya miezi mitatu kuwa aliyeshinda kwa sasa mafuta ya mwezi wa sita yatakuwa bei hii sababu nasema hivi mtu akija ku tender huku anakuwa kishiingia makubaliano ya supply ya miezi mitatu iweje tangazo lije usiku tu kesho yanapanda. Haya yaliyopanda ni lini yaliletwa? kuna rushwa kubwa katika mfumo wa uagizaji mafuta wa pamoja, Nilidhani kama kipindi kile wa kusema baada ya miezi mitatu bei itashuka kwa kiasi hiki sababu aliyeshinda tender kampuni ya TPDC wame tender bei ya chini sasa iweje jana usiku linakuja tangazo? Ni muhimu sasa kujuwa hizi tender wanashindaje? navyojuwa huwezi kushinda tender halafu ukaja kubadili bei njiani inakuwa tender yote batili. ulishinda kwa bei hii huwezi kubadili. Makamba lazima aje hadharani aelezee imekaaje hii.
 
Tunalipia madhara ya vita!!...

Halafu kuna watu wanasifia Urusi kuvamia nchi nyingine....
Mkuu Sasa wewe mbona kutosifia urusi kwako hakujapelekea Vita kukoma? Kwa akili zako unaamini kuisifia urusi ndo kunapekelea mafuta kupanda Bei,?
 
Back
Top Bottom