EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

We kweli hamnazo so unataka nani alaumiwe?! Kama anakubali kupangiwa tumlaumu JK AU!
 
Ila daah!! Hatujamaliza lile, ghafla linakuja hili la mafuta kupanda, sasa unadhani lile litakamilishwaje...
Linatakiwa kuanza kukamilishwa lililotangulia 😜😜

Wachana na mafuta, mwendokasi upo.
 
Rais wa Ukraine ni fala tu, kutojiunga kwake na NATO kunampunguzia nini? Wasweden na Wafini wame-enjoy amani na Urusi kwa miaka mingi kwa sababu ya kutojiingiza kwenye mafungamani na NATO, leo wako roho juu kwa sababu ya kujiingiza kwenye mgogoro wa Russia vs Ukraine kwa kupeleka silaha Ukraine au kutaka kujiunga na NATO. Kupanga matumizi kwa kipato ambacho jirani ameahidi kukusaidia ni ujinga. Hao Marekani na wenzao wanachofanya ni kupeleka silaha tu kwa Ukraine ili vita iendelee wakati wao wako pembeni wanasubiri kuwapelekea ankara ya gharama za silaha mara vita vikiisha.

Ukraine wameingia gharama kubwa sana kwenye vita hii, kama wangechagua kubaki na msimamo wa awali hii vita isingekuwepo. Itawagharimu sana kuijenga upya miundimbinu yao na hakuna gharama ya kufidia uhai wa watu wao.

Vv
Sorry nikurekebishe tu by record. Kwanza sweden na finland majuz tu wame request kujiunga NATO. As we speak wako kwenye mazungumzo

Lakini Bado hujajibu swali. Ukraine si taifa huru? Si lina right ya kujilinda? Si lina jeshi lake na bendera yake?
Kwann wakifanya maamuzi kama taifa huru wanaonekana wabaya..?
 
Mafuta kwenye soko la dunia hayajapanda bali yameshuka kidogo, Ila usiniulize kwa nini bongo yamepanda

Mkuu umesahau, bei uliyoiona leo sio iliyotumiwa kuyanunua mafuta yaliyopo sokoni leo. Pili, bei uliyoiona ni ya muuzaji kwenye refinery yake. Sio pamoja na export levy, freight, import levy na kodi nyingine.

Usisahau kila tukinunua tunanunua mafuta ya miezi kadhaa ya mbele na ndio maana mabadiliko ya bei soko la dunia kila siku hayana athari kwetu!

Ni kweli pia mifumo yetu ya kodi na aina zake si rafiki kwa mlaji wa ndani. Tusipodhibiti bei sa bidhaa hii muhimu tutashindwa kusonga!
 
Hiyo sukari 3500 unaopata wali wewe fala? Walipopamdisha uliona Magufuli alichukua hatua gani? Ongelea huyo bibi yako! Vitu vyote vimepanda bei hata kabla ya vita ya Ukraine!
Sijaribu kumtetea lakini sababu ya vitu kupanda kipindi hiki zinajulikana.
 
Kuna kipindi serikali ya mwendazake ilikua ianzishe petrol statns za serikali sijui ile plan iliishia wapi muda kama huu vingeweza kusaidia kupunguza makali kwa kuuzia wananchi kwa bei nafuu kidg
 
Zile za kukebehi vigari vidogo kama passo, vitz na IST ziendelee na sasa hivi.
 
Leo nimeenda kujaza mafuta ya dizeli kwenye gari langu nikitumaini kuwa bei niliyoizoea ni Tshs.2842 kwa lita hapa Mwanza. nilipotoa fedha ya lita 20 yaani Tshs.56,840 nikaitwa ili niongeze hela.

Nikawa mbogo nikaambiwa unatakiwa kulipia Tshs.68,040. Tofauti ya Tshs.11,200. Bado ninajiuliza kuwa juzi ndo Latra iliwaongezea wamiliki wa vyombo vya usafiri gharama zao za nauli, itakuwaje tena jana bei tena zimeongezeka. Je itabidi waongezewe bei tena?. Vile vile bei ya dizeli ndo imeongezeka kuliko hata petroli ni kwa sababu gani?.

Itakuwa vema kama Serikali ingekuwa inatoa elimu kwa wananchi kupitia luninga kwa vigezo ni kwa nini bei ya mafuta imepanda kwa kipindi husika. Tukiendelea hivi Serikali iliyo madarakani itaendelea kuchuchukiwa sana na wananchi.
 
Back
Top Bottom