EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta zinazoanza kutumika Juni Mosi

Yaani nashangaa watu hawaelewi nn hapo,ni kwamba inonekana bei inazidi kupanda na mwezi huu ingekua Tshs 3000 kwa dar,lkn ruzuku imeishusha na kua Tsh 2994.
Mbona hesabu rahisi iyo mnakwama wapi kuelewa??
Ni ruzuku ya Tshs 300
 
Hi
Hiyo ela ya ruzuku bora wangenipa tu nifanyie mambo yangu maana sioni cha maana hapo.
 
Siyo kwa Tanzania aseee, leo kuna binti kalipa nauli 2000 alipanda kituo A akashuka kituo D konda kamrudishia 1000 binti kadai 500 konda hakumjibu kagonga gari ikaondoka, abilia wengine wakapotezea.
😂
Nasikia hiyo ndo nauli 'halali' ya kutokea Kawe kukanyaga mafuta!
 
Hiyo ruzuku kwa mafuta ya Tanga haijafanya maajabu.
 
Hizi ni ngonjera flani hivi.
Walijua watatoa ruzuku kwa nini wapaishe nauli?

Leo wamepunguza bei issue ya nauli inasimamia wapi?.
Gharama za maisha zilipanda
 
Tengeneza tatizo, tatua tatizo, pata ujiko
 
Zanzibar bei zipoje?
Kwa Znz huwa hakuna sarakasi nyingi kwenye bei za mafuta.. Tofauti na Tanganyika ambapo kila Lita 1 ya mafuta ina utitiri wa Kodi na tozo mbali mbali zaidi ya 20🤔🙄 Wakati Bara bei ikiwa zaidi ya 3,000, Znz ilikuwa 2,600.
Kama nao wamepewa hiyo 'ruzuku' basi bei yao itakuwa poa!
 
Mikoa yenye bandari ndio bei imeshuka kwenye petroli ipo chini ya 3000 lakini Mikoa mingine petroli ni kuanzia 3000 kwenda juu.
Ukiangalia kwenye chati sehemu ambayo petroli inauzwa chini kabisa ni muheza Lita moja inauzwa 2990
Sehemu nyingine bado maumivu ni yaleyale
 
Nilitegemea hili!

Hakuna lolote la maana kwa watumiaji wa mwisho!
 
Ni
Ni hivi, kusingekuwa na ruzuku bei mpya ingekuwa 3300. Hakuna aliyedanganya hapo
Basi tufanye kua wameshusha shiling 500, maana kusingekua na Ruzuku bei mpya ingekua 3500!! Number ukizijua rahaa sana,unacheza nazo unavyotaka!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Zanzibar ambayo haijaweka hata ruzuku ila bei zao zipo chini kuliko sisi.

Rais afanye ziara Zanzibar akajifunze kutoka kwa Mwinyi juu ya hili.
Kule ni kwao hataki kuwaumiza ndugu zake yeye adui zake ni wabara
 
Mimi huwa najiuliza haya makato sijui ya EWURA na TBS ni ya nini? pesa hizi wanazifanyia nini? hawa ni watumishi wa serikali wako kwenye payroll hata kama wamelala hawana kazi.

Hizi pesa huwa wanazifanyia nini? kwa kazi gani? ku regulate bei tu? huwa najiuliza sipati jibu kama kuna mtu anajuwa hebu atueleze wanakusanya za nini? mishahara yao? hata mishahara mbona pesa ndefu inakusanywa inaenda kwenye matumizi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…