Ezekiel Kamwaga: Cuba mtungi wa gesi unaanzia laki moja na nusu mpaka laki tatu

Ezekiel Kamwaga: Cuba mtungi wa gesi unaanzia laki moja na nusu mpaka laki tatu

1756635860463.png
Kilaza SLUG hajui hata kudanganya!
😅 :peepoSpeed:
NB: 1. Kwa bei ya Polepole ya gesi,Cuba, nchi hiyo ingekuwa kimbilio la 'wanyonge' wote Duniani!
2. Hata kwa 'psychology' ya kiwango cha chini kabisa, ukiangalia tu macho yake na unyevunyevu wake, anapowasilisha 'story' zake nyingi, utaona kabisa huyu mtu ni muongo na nafsi inamsuta!
3. Wakati shujaa wetu, JPM, anatutoka, hivi viumbe vilivamia BOT na kuchota humo vilivyoweza kuchota! ... dhahabu yetu, pesa zetu za madafu na za kigeni ndizo sasa zinaendesha hizi harakati za akina polepole! WOTE WEZI TU!
 
Kwa hiyo mkweli ni Polepole aliyesema ni Tsh 2000?
Sasa hiyo elfu elfu mbili na nyingine malaki ipi ipo karibu na dola sita?

Pia mabalozi wabanunua bidhaa mara nyingi bila kodi kwenye maduka yao ya serikali kwa nchi kama Cuba. Hata TZ ilikuwa hivyo enzi za Nyerere
 
Bei ya Gesi ya Kupikia (LPG) Duniani

1. Mambo yanayoathiri bei ya LPG duniani
  • Vita vya Ukraine na Russia (2022) vimesababisha ongezeko la gharama za uagizaji na changamoto za usambazaji
  • Mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji wa fedha huathiri gharama za ndani
  • Hata nchi zinazotoa ruzuku hupata ongezeko la bei

2. Bei ya mtungi wa kilo 20 katika nchi mbalimbali
  • Mexico/Colombia: USD 15–25 (TZS 40,500–67,500)
  • Algeria (ruzuku): bado bei hupanda kutokana na changamoto za kiuchumi
  • Makadirio ya kimataifa: USD 10–20 (TZS 27,000–54,000) hata kwa ruzuku

3. Cuba na mfumo wa ruzuku
  • Uchumi wa Cuba unadhibitiwa na serikali, na LPG huuzwa kwa ruzuku
  • Hata hivyo, bei ya TZS 2,000 kwa mtungi wa kilo 20 ni ya chini kupita kiasi
  • Ruzuku ya kiwango hicho (95–98%) ni nadra hata kwa Cuba

4. Tathmini ya kauli ya Humphrey Polepole
  • Ina uwezekano mkubwa wa kutokuwa sahihi
  • Huenda alimaanisha saizi ndogo ya mtungi (kilo 1 au 2) au bei ya zamani
 
Haya sasa, kuna watu walidhani taarifa za Cuba hazipatikani. Uongo mkubwa umedhihiri. Tanzania ya sasa ni ya wasaka taarifaView attachment 3459625
Sasa anambishia mtu aliyeishi huko huko Cuba? Hawa machawa ni wajuaji sana si ndio huwa wanajilinganisha hadi na USA eti wanakopa kuliko Tanzania!! Hivyo tupo vizuri zaidi yao
 
Sasa hiyo elfu elfu mbili na nyingine malaki ipi ipo karibu na dola sita?

Pia mabalozi wabanunua bidhaa mara nyingi bila kodi kwenye maduka yao ya serikali kwa nchi kama Cuba. Hata TZ ilikuwa hivyo enzi za Nyerere
Huna unachojua na umeshachagua kuamini alichosema Polepole. Baki na huo msimamo hadi akuaminishe kuwa kinyesi ni chakula.
 
Polepole mmoja anajibiwa na wanasi-hasa, maaskofu, mashehe, machwa, vibwetere, vibwengo, vijizi, majizi n.k
Kila kukicha kuna Jukwaa jipya,,, Mpaka elf 2 ya Gesi imetengenezewa jukwaa...
Hata shetani anashambuliwa na watu wengi sana. Polepole ni shetani
 
Kwa taarifa, jana nilibandiko hili:

S.M.P2503 said:
Si sahihi kusema “gesi ya kupikia Cuba inauzwa TZS 2,000.” Kisheria, bei ya mtungi wa 10 kg nchini Cuba ni 225 CUP; ukibadilisha fedha: ni takriban TZS 1,350–4,620 kutegemea kiwango cha kubadilisha fedha unachotumia. Lakini kiuhalisia, kutokana na uhaba na soko la walanguzi, wengi hulipa TZS ~78,000–168,000 kwa ujazo huohuo—kwa hiyo madai ya “TZS 2,000” yanapotosha muktadha. (cubadebate.cu, Cubatrámite, elTOQUE, Bank of Tanzania, Directorio Cubano)

Ushahidi wa takwimu na makadirio (Cuba na Tanzania)

  • Bei rasmi Cuba (mtungi 10 kg): 225 CUP kuanzia 1 Machi 2024. (cubadebate.cu, Cubatrámite)
  • Ubadilishaji → TZS (30 Agosti 2025):
    • Kiwango cha soko lisilo rasmi (elTOQUE): 1 USD ≈ 410 CUP ⇒ 225 CUP ≈ USD 0.549 ⇒ kwa BoT 1 USD ≈ TZS 2,463 ⇒ ≈ TZS 1,351. (elTOQUE, Bank of Tanzania)
    • Kiwango cha benki/CADECA (karibu 120 CUP/USD) ⇒ 225 CUP ≈ USD 1.875 ⇒ ≈ TZS 4,619. (Kiwango cha 120 CUP/USD ni cha rasmi; thamani ya TZS inatumia BoT ya leo). (Cuba Unbound, Bank of Tanzania)
  • Uhalisia sokoni Cuba (2025): uhaba ulisababisha balita kuuzwa 13,000–18,000 CUP (ujazo tu) na hadi 28,000 CUP (mtungi umejazwa)—sawa na takriban TZS ~78,000–108,000 (ujazo) na ~TZS 168,000 (mtungi umejazwa) kwa kutumia 410 CUP/USD na BoT. (Directorio Cubano)
  • Mlinganisho na Tanzania: rejareja za kawaida (Dar n.k.) ni takriban TZS 21,500–22,700 kwa 6 kg na TZS ~47,000 kwa 13 kg ⇒ ~TZS 36,000 kwa 10 kg (ukipima kwa bei/kilo). (TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, superstore.co.tz)
Mwisho:
  • Ndiyo, kinadharia ukiangalia bei rasmi ya Cuba na ukitumia kiwango cha soko lisilo rasmi, 10 kg “hutafsiriwa” karibu TZS 1,350—chini ya TZS 2,000.
  • Lakini, kwa vitendo wananchi wengi hawapati hiyo bei kwa sababu ya mgao/uhaba; wanaishia sokoni ambako 10 kg hufikia mara 2–5 ya bei ya Tanzania. Kwa hivyo kauli “Cuba ni TZS 2,000” haina uhalisia wa soko na inahitaji kuwekwa wazi kuwa ni hesabu ya ubadilishaji wa fedha, si bei unayolipa mteja kawaida. (Directorio Cubano)
(reference/Marejeo: Taarifa za bei rasmi za Cuba, viwango vya kubadilisha fedha vya sasa, na bei za rejareja Tanzania zimeorodheshwa kwenye vyanzo vilivyonukuliwa hapo juu.)

Pamoja na hayo yote hapo juu, swali la msingi linabaki, ni kwa nini Watanzania walipishwe hadi Tsh 55000 kwa mtungi (sio Msajili wa vyma vya siasa) ikiwa Gesi tunayo toka huko Lindi/Mtwara? Au ni mpaka bibi wa mtwara apigwe biti ili aruhusu gesi itolewe Bure?
Mimi sikugusia bei ya gesi Tanzania kuwa ghali, hoja yangu ilikuwa kukataa bei ya mtungi wa gesi 20kg kuwa 2,000 kule nchini Cuba.

Na bei ya vichochoroni au bei isiyo halisi haiwezi tumika kama standard. Haya mambo yalikuwepo sana nchi za Kikomunisti ikiwepo Cuba yenyewe.

Serikali ya kijamaa ya Urusi ilikuwa kwenye makaratasi inadai magari ni bei nafuu kuliko Marekani na nchi za Ulaya, ila ukitaka kununua gari labda Lada Niva unachukua kuponi na unasubiri miezi zaidi ya 4 ndio upate gari hilohilo linalotengenezwa nchini kwako. Wakati gari za nje muda wowote zipo showrooms.
Toilet paper kwenye makaratasi ya serikali ni very cheap, ila haipo kwenye groceries afadhari ununue gazeti au daftari la kuandikia. Wakati kule kunakotajwa toilet paper zina bei kutokana na uchumi wa kibeberu, kila raia hata mlalahoi anaweza nunua hata akitaka kontena zima.

Au sometimes bidhaa zinapatikana Moscow na St. Petersburg pekee, kisha serikali inadai bei moja nchi nzima wakati uko kama Yekaterinburg hazipo. Kuna muda ndege ya kijeshi ya Urusi ilianguka ikiwa imebeba maofisa wa juu zaidi wa Soviet Navy baada ya mkutano wa kijeshi, kisa wamenunua personal items nyingi maana kambi walikotokea mbalimbali haina hizo bidhaa, ndege ikazidiwa uzito.
Kwa ulinganifu/ compare and contrast -Iran - tulisikia kwamba bei ya mafuta ni cheap sana kuliko bei ya maji- watanzania wanafunzi walihojiwa na chombo fulni cha habari (wakati ule Israel inaishambulia Iran)na wakasema hivyo... sisi tunashindwa nini kuwa kama wao? Na kama serikali na viongozi wao wameshindwa KUFANYA GHARAMA ZA MAISHA ZIWE CHINI KABISA, kwa nini wasikaribishe mawazo mubadara ili tuendelee kuijenga nchi yetu pamoja?
Iran bei ya mafuta iko chini sana sababu wanazalisha mafuta kwa siku mapipa milioni tatu na nusu, Iran bila OPEC+ kuweka quota hata kesho tu wanaweza zalisha pipa milioni 5 za mafuta kwa siku. Wewe Tanzania inazalisha pipa hata 1 kwa siku??

Na ndio maana maji wanayauza bei kuliko mafuta, vyanzo vyao vya maji ni vichache kuliko sisi.
 
Hata hela ya Cuba hajui inaitwaje halafu anapinga asichojua.
 
Mtungi wa gas Cuba ni dola kati ya sita na saba (180 pesa ya Cuba). Kutegemeana na wapi unabadili pesa yako maana Cuba kuna black market ya dola

Sasa dola sita kwa Tanzania ni kana elfu 15.
Akina Polepole ni mabalozi wanapata dola kwenye channels sahihi za serikali Kwahiyo inawezekana gas kununua hata chini ya hapo.
Dola 6 au 7 za Marekani ndio zinakupa shilingi 2,000 ya Kitanzania ambayo haifikii hata dola 1?

Bei ya balozi ndio bei ya soko, ndio ya mwananchi. Kwani Polepole alikuwa anataja bei kwa ajili ya mabalozi? Balozi wa Finland akija akala bure Serena Hotel, akienda kwao Helsinki aambie wananchi kuwa Tanzania kule 5 star hotel zinalisha watu bure?

Na ubaya zaidi unasema Cuba kuna black market ya dola. Unajua hiyo inaashiria nini kiuchumi? Tena sio ya dola tu, hata ya hiyo gesi, ya bidhaa muhimu. Nchi yenyewe huwa inakumbwa na mgawo wa umeme kisa mafuta hayatoshi ndio mnatwambia hapa mtungi wa gesi 20kg sawa na bei ya parachichi Kariakoo 😂

Yaani Cuba isiyo hata na gesi, haina LPG plant, haina LPG tanker hata moja ndio iwe na bei ndogo ya gesi kuliko nchi zenye gesi, LPG plant, mabomba na tankers za kuuza nje. Kwani gesi imekuwa ARVs?
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Ni Tanzania tu mtu anayeishi sehemu fulani anapingwa na mtu ambaye hajawahi hata kufika hiyo sehemu.

Yaaani tumsikilize hiyo Kamwaga ambaye hajawahi hata kufika Cuba alafu tuache kumsikiliza Polepole kama mwakilishi rasmi wa nchi nchini Cuba?
Kweli vichwa pumbu mko wengi..
Kwahiyo akisema kyuba kuna mti unazaa hela utaamini kwa kuwa yeye aliishi huko
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Back
Top Bottom