Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Ndoto za mkosaji hizi.
 
Tafuta mwanasheria makini akupe elimu ili uelewe kitu ambacho hukijui mpaka dakika hii.

IGA haina maana iwapo HGA itaharibika kwa namna moja au nyingine. Kumbuka kuwa HGA zinaanzishwa kwa kufuata sheria na kanuni za Tanzania.

Mkuu denooJ wanasheria wabobezi wameujadili kifungu kwa kifungu ndani ya ukumbi wa bunge na wengine walikwenda mpaka huko Dubai wakajadiliana na DPW kwa kina.

Punguza mbwembwe na huu ujuaji wa mitandaoni.
 
Haya ndio matatizo ya kuwa na kiongozi aliyefeli shule.
 
Mkuu nchi ya laana hii hasa polisi ni kazi ya laana kuna mmoja naish kwake polisi mstaafu adi chakula ananiomba mim hua namnyoosha sana na nataka nihame kimy kimy nkakae nyumba za maana mbwa hawa
Huwa wanaishi kwa rushwa, wakistaafu wanapewa mafao kuanzia milioni kumi na saba kwa nini wasiwe mabwege.
 
Umejibu Tu kama mimi kuwa termination clause ipo isipokuwa wewe umeona "the worst case scenario"...
Sisi wengine hatuamini watumishi watafanya makosa hayo unayosema..
Bottom line termination clause ipo..
Wewe umeona mapungufu ya termination clause...sio Sawa na kusema "hakuna termination clause"
 
Tatizo lenu mnadhani mkataba ni wa wanasheria. Maudhui ya mkataba siku zote si ya wanasheria. Wanasheria kazi yao ni drafting tu. Wataalam wa Bandari, Uchumi, na Uwekezaji ndio wanaojua nini wanataka kwenye huo mkataba.
Hebu nieleze kwenye huo mkataba hao "watu" uliosema wanataka nini. Eleza vitu ambavyo Taifa litapata, siyo hao "watu". Haya nieleze kwa mujibu wa mkataba nini kama taifa tutapata, hao DP WORLD watapata nini kwa kuwekeza nini na kwa mchanganuo upi. Usipende kukimbilia statement za jumla kwamba "tatizo lenu".
 
Huyu Mama ngoja aendelee kudannganywa na hao machawa wake!
Hata Waziri Mkuu wetu uwezo/upeo wake una walakini kwenye mambo makubwa na ya msingi kwa Taifa!
 

Tuseme tu walio kubali mkataba wa mwanzo hawakua makini. Ni kweli mkataba unaendelea kujadiliwa. Lakini kukubali mapendekezo ya awali ya DP world yakiwa na makosa kiasi icho sio sahihi kabisa. Au tuseme tunachosoma kwa sasa ni mapendekezo ya DPworld. Na serikali ina mapendekezo yake. Na kama ni hivyo wanashindwa nini kutuambia wananchi mapendekezo ya serikali ni yapi? Na je unazani serikali wanaweza kukataa huo mkataba wakishindwa kuafikiana? The boss umeusoma mkataba wa awali Je ni kati ya serikali ya UAE na Tanzania au DPworld na Tanzania?
 
Hawasomi. Wanaishia kulalamika eti anasalitiwa au anabaguliwa.
Na kuokoteza maneno ya Mbarawa wanayabeba vichwani mwao, hawajui yule ni mwanasiasa, hiyo IGA inajieleza wazi kabisa, baada ya kusainiwa October 2022, mwarabu yuko huru kuanza shughuli zake, ndio maana ya hizi kelele za sasa, sio vinginevyo.

Wao wanakuja na utetezi wa uongo tusubiri HGA, watuambie basi, wapi IGA imetuambia tusubiri kwanza makubaliano ya HGA ndio utekelezaji wa mkataba uanze, watupe kifungu.

Kwasababu hapo nimeshawapa kifungu kinachosema makubaliano ya IGA ni legally binding, kusema tusubiri HGA hiyo ni janja ya kisiasa tu, kwanza wanapoteza muda kufunika kombe... lakini pia, wanajua watauficha huo mkataba wa hovyo hatutauona tena!.
 
Unaponiambia nitafute mwanasheria ina maana wewe hujui unachoandika hapa, unabisha tu; terms za IGA zinajieleza zenyewe, tatizo wewe hata kuzisoma naamini hujazisoma.

Ningetegemea kama unauelewa wa haya mambo kama unavyodai, wewe ndie uwe wa kwanza kunielewesha, ajabu unaniambia nitafute mwanasheria!.
 
Kwani umeambiwa IGA ni risiti kwamba itakuonyesha alichotoa na kupokea muuzaji na alichopokea na kulipa mnunuaji? Kwahiyo na wewe ndiyo miongoni mwa wabobezi wa sheria wanaotuchambulia mkataba wetu au?😆
 

Hatari sana. Ingebidi kupitia mikataba ya nchi nyingine zote zilizoingia na DP-World ili kuangalia makosa waliyoyafanya na kuyazuia kwenye nchi yetu.

Mikataba mizuri tuige hayo mazuri, kuepuka vipengele vitavyotuangamiza.
 
Tatizo hujui kazi ya IGA nini na kazi ya hizo HGA ni nini na kazi ya Projects activities ni nini? By the way usitake wewe ni nani? Yaani Serikali isifanye lake kwa kusikiliza wapuuzi wasiojua wanachobisha?
Ongeza uelewa. Soma hii article hapa chini.

 
Kwani umeambiwa IGA ni risiti kwamba itakuonyesha alichotoa na kupokea muuzaji na alichopokea na kulipa mnunuaji? Kwahiyo na wewe ndiyo miongoni mwa wabobezi wa sheria wanaotuchambulia mkataba wetu au?😆
Tunataka majibu kutoka kwa wahusika, sio porojo.
1. Kwa nini apewe bandari zote za bahari na maziwa?!

2. Kwa nini apewe kipaumbele yeye hata kwa projects ambazo hazijaanza?!

3. Kwa nini haikutangazwa tender ya wazi ili washindane wote duniani tupate aliyebora?!

Jibuni maswali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…