Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Nadhani hizo Sheria ipo kwa waliopo ndani ya na wale wanaojenga majengo makubwa au magorofa,lakini kwa walio nje ya mji ambaye amenunua eneo lilipopimwa na halmashauri na anajenga nyumba ya kawaida sidhani Kama ni tatizo

Mkuu utakuwa unaongelea zamani, sasa hivi bila kibali cha ujenzi utavunjiwa tuu, fuateni sheria msije kulia baadae, tena kama hujapima kiwanja chako fanya hima ukapime kabla kiwanja chako hakijageuka kuwa barabara
 
Unaweza kuwa ni mmoja kati ya 10 au 100 lakini professionals wengi ndiyo namba moja kukiuka sheria na kanuni eg joka la makengeza kwenye sakata la rada, ndugu yai alivyompiga na gongo mtia nia mwenzake, wale wengine wa escrow, walimu nao wanakula urefu wa kamba si kwamba hawajui sheria....
Nimecheka sana!
Watu mnajua kuweka kumbukizi nyie! Eti 'joka la makengeza na nduguyai'! Dah!
 
Wewe jàmaa ni njaaa Sana kumbe ni walewale Kama dalali tu kuzurura mitaani kutafuta Nani anaejenga Bila kibali alafu unakimbilia manisspa unakuja na wale afisa wa ujenzi mwenye njaa hadi kwenye kope.mwanaume wewe pambana kuijengea misingi familia yako acha kuangaika na watu wanaopambana kuwekea familia zao future.
Umetukosea sana heshima aisee sema sababu umejificha nyuma ya keyboard unaweza kuongea lolote katika thread hapo nadhani kilichotolewa ni elimu ili watu walitambue kuwa katika nchi unatakiwa kufuata sheria za ujenzi ili uwe huru na kuepukana na adhabu zisizo na msingi
 
Hivi kibali cha ujenzi mbali na kuogopa hizo faini zenu za kipuuzi kina faida gani katika ujenzi wa nyumba ya kawaida za kuishi ikiwa kiwanja kimepimwa. Mimi ninajenga nyumba buyuni ccm kuelekea chanika na sina hayo mavibali yenu ya uongo uongo na bureaucracies za kijinga.
Sasa hapo unaiambia serikali mana sisi kama kampuni tumekupa elimu bure tu
 
mimi najenga chumba na sebule,ngoja nifuate huu utaratibu,,ila mlolongo mbona mrefu sana?
 
Back
Top Bottom