Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Ta
Tatizo kubwa ni mawasiliano ya hiyo bodi ya korosho na jinsi ya kuandaa shamba.
 
Wasiliana na bodi ya korosho watakwambia wapi utapata miche, ila kwa wastani ekari moja inaingia miche 39 hivi.
 
Habari wajasiriamali.

Ni kijana mwenzenu ambaye ni mkulima wa korosho mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba. Kesho naenda kutembelea na kufanya farmer works na kurudi home.

Nitawajulisha nikifika.
Inshaaalah

great thinker
Wanauza ngapi ufuta mtwara
 
Habari wana JF.

Naomba mwenye uzoefu au utaalamu wa zao la korosho anisaidie kujua mahitaji ya kuanzisha kilimo hiki. Nataka nitafute shamba(virgin land) kwa kilimo hiki, napenda nijue maeneo ambayo zao hili hustawi sana, mbegu bora ya muda mfupi, gharama za kuhudumia hadi kuanza kuvuna ikiwa ni pamoja na madawa, mbolea kama itahitajika na masuala mengineyo.

 
Kwa kuwa unataka kuanza kupanda habari ya madawa sitakueleza.Tafuta shamba maeneo ya kusini mwa Tanzania(Lindi, Mtwara, Tunduru). Miche tunapanda kipindi cha mvua ambapo halmashauri husika wanagawa niche kupitia serikali za vijiji. Kumbuka mbegu wanayotoa ni ya miaka mitatu,ila mavuno yanaongezeka kadri ya umri wa mti unavyoongezeka.

Uzoefu unaonyesha kuwa mashamba mengi yanamilikiwa na Wazee, hivyo kuna umuhimu wa vijana kuanza kupanda miti mipya kwenye maeneo mapya ili kutransfer uchumi uje kwetu. Kwa wale wanaonunua mashamba yenye miti iliyozeeka wanachofanya no kupanda niche mipya na kukata ya zamani pale mipya inapoanzaa kuzalisha.
 
Asante mkuu
 
Nenda serikali ya kijiji ambapo shamba lako lipo watakupa utaratibu, mm nilipata mwaka jana miche ya bure.
Ni kweli Serikali ya kijiji wanatoa miche ya bure! Ila inagharama zake, mfano mimi mwaka huu niliomba miche wakaahidi kunipa.

kilichotokea nimekuja kupewa miche mwishoni mwa msimu wa Mvua matokea yake miche mingi imekufa kutokana na kutopata maji ya kutosha!

Nimejipanga mwakani nitanunua tu miche! Bure ni Ghali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…