Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Ta
Mbegu huwa inagawanywa bure na bodi ya korosho baada ya kukuzwa na watu mbalimbali walioteuliwa. Kwa kawaida itaanza kugawanywa kati ya oktoba na desemba.

Muhimu ni kuandaa shamba na kutoa taarifa ya idadi ya mikorosho utakayohitaji toka bodi ya korosho.
Tatizo kubwa ni mawasiliano ya hiyo bodi ya korosho na jinsi ya kuandaa shamba.
 
Wasiliana na bodi ya korosho watakwambia wapi utapata miche, ila kwa wastani ekari moja inaingia miche 39 hivi.
 
Habari wajasiriamali.

Ni kijana mwenzenu ambaye ni mkulima wa korosho mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba. Kesho naenda kutembelea na kufanya farmer works na kurudi home.

Nitawajulisha nikifika.
Inshaaalah

great thinker
Wanauza ngapi ufuta mtwara
 
Habari wana JF.

Naomba mwenye uzoefu au utaalamu wa zao la korosho anisaidie kujua mahitaji ya kuanzisha kilimo hiki. Nataka nitafute shamba(virgin land) kwa kilimo hiki, napenda nijue maeneo ambayo zao hili hustawi sana, mbegu bora ya muda mfupi, gharama za kuhudumia hadi kuanza kuvuna ikiwa ni pamoja na madawa, mbolea kama itahitajika na masuala mengineyo.

HABARI,
"Mshuza2,

Kama unania hiyo wahi Mkuu ndani ya miaka 3 Kama ukitumia mbegu ya kubebesha na Kama mambo yote yatakwenda safi kwa upande wa ukuaji na kama utaweka lengo la miti Elfu moja na kundelea utakuwa na kipato cha uhakika sana na kikubwa kwa mwaka,Na hata kama ulikuwa na mawazo ya biashara nyingine ukakosa mtaji hapo kila mwaka unakuwa na mtaji tosha Huangaiki na Bank.

Kwa mti mmoja wa miaka 3 unaweza kuanza kuvuna mpaka kilo 2-3 ikifika miaka 5-10 ni zaidi kilo 30 Pale Dodoma kwenye wilaya ya mpwapwa kunagereza wanayo miti walipanda ya kubebesha ya miaka 10 kila mti unatoa kilo 40 kwa mwaka.Sasa kama ukivuna kilo 2 kwa kila mti kwa miti 1000 ni tani 2 na kwabei ya mwisho wa mwaka huu ilifika mpaka elfu 3800 kwa kilo maana ya sh. Milioni 3.8 kwa Tani ukiwa na tani 2 ni milioni 7.6 hiyo ni kwa kilo 2 kwa mti mmoja sasa piga hesabu ukivuna kilo 5-10 kwa mti utapata jibu Mkuu na hata kama bei ikiwa ni sh.2500 kwa kilo bado unahela nyingi.

Wataalam wakubwa wa mambo ya uchumi wanakwambia matajiri wengi wapya watakaokuja kwa sasa ukitoa mambo ya COMPUTER wengi watatokana na shuguli za kilimo hao ni wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi.
Usirudi nyuma Ndugu ifanyie kazi.

LUMUMBA
 
Kwa kuwa unataka kuanza kupanda habari ya madawa sitakueleza.Tafuta shamba maeneo ya kusini mwa Tanzania(Lindi, Mtwara, Tunduru). Miche tunapanda kipindi cha mvua ambapo halmashauri husika wanagawa niche kupitia serikali za vijiji. Kumbuka mbegu wanayotoa ni ya miaka mitatu,ila mavuno yanaongezeka kadri ya umri wa mti unavyoongezeka.

Uzoefu unaonyesha kuwa mashamba mengi yanamilikiwa na Wazee, hivyo kuna umuhimu wa vijana kuanza kupanda miti mipya kwenye maeneo mapya ili kutransfer uchumi uje kwetu. Kwa wale wanaonunua mashamba yenye miti iliyozeeka wanachofanya no kupanda niche mipya na kukata ya zamani pale mipya inapoanzaa kuzalisha.
 
Kwa kuwa unataka kuanza kupanda habari ya madawa sitakueleza. Tafuta shamba maeneo ya kusini mwa Tanzania (Lindi, Mtwara, Tunduru). Miche tunapanda kipindi cha mvua ambapo halmashauri husika wanagawa niche kupitia serikali za vijiji. Kumbuka mbegu wanayotoa ni ya miaka mitatu, ila mavuno yanaongezeka kadri ya umri wa mti unavyoongezeka.Uzoefu unaonyesha kuwa mashamba mengi yanamilikiwa na Wazee, hivyo kuna umuhimu wa vijana kuanza kupanda miti mipya kwenye maeneo mapya ili kutransfer uchumi uje kwetu.

Kwa wale wanaonunua mashamba yenye miti iliyozeeka wanachofanya no kupanda niche mipya na kukata ya zamani pale mipya inapoanzaa kuzalisha.
Asante mkuu
 
Nenda serikali ya kijiji ambapo shamba lako lipo watakupa utaratibu, mm nilipata mwaka jana miche ya bure.
Ni kweli Serikali ya kijiji wanatoa miche ya bure! Ila inagharama zake, mfano mimi mwaka huu niliomba miche wakaahidi kunipa.

kilichotokea nimekuja kupewa miche mwishoni mwa msimu wa Mvua matokea yake miche mingi imekufa kutokana na kutopata maji ya kutosha!

Nimejipanga mwakani nitanunua tu miche! Bure ni Ghali.
 
Back
Top Bottom