Familia ya Freeman Aikaeli Mbowe yathibitisha mwanafamilia kuwa na Corona

Familia ya Freeman Aikaeli Mbowe yathibitisha mwanafamilia kuwa na Corona

Makonda anayoyafanya siyo kwamba hajui anakosea ila anafanya ili awe anazungumzwa na kutrend kwenye social media, hizi taarifa zake ambazo mtu mwenye akili timamu huona hazina maana ingekuwa zinaachwa ingemsaidia sana kumrekebisha kuzungumza mambo ya msingi ila kuzipublish hivi ndiyo matokeo yake haya kila siku ni vihoja

ha ha ha, wakati mwingine ili watu wa mtaani masela wa kijiweni waamini uwepo wa kitu cha hatari basi ni lazima kugusa na kuchoma sindano za moto kwa baadhi ya familia ‘kubwa’, japo mkubwa ni Mungu tu alieleta adui Corona asieshikika mkononi akupigae nawe huwezi kulipiza kisasi! nani angemfunga paka kengele sasa , mi kwangu naona hakukosea kumtaja mgonjwa this is public health issue kwanini DJ afiche ili mtoto akichepuka mtaani kula fegi awaambukize masela manake si hawakutaka ajulikane? mbona watu wengine wamejitangaza na kuwekwa lock up aka karantini!
 
Ikumbukwe kabla ya ugonjwa wa Corona haujafika Tanzania, Bavicha na chadema kwa ujumla walikuwa wakikesha mitandaoni wakiombea Corona ije ili wamkomoe na kumcheka rais Magufuli!.

Mwana jamii forum anayeitwa technically alileta Uzi humu akiombea na kushangaa kwa nini Corona haifiki haraka Tanzania!, Naam kama ilivyoandikwa aombacho mtu ndiyo hupewa, kama alivyoomba technically Corona imekuja Tanzania na hatua ya kwanza imeshambulia familia ya boss wake Freeman Mbowe!, nadhani sasa technically atakuwa anarukaruka kwa furaha sana huko aliko

Tuwaonye tu vijana wa chadema kuwa Mungu hana mchezo, mahaba yenu kwa Mbowe yasiwatoe ufahamu na kuanza kuiombea mabaya nchi mkidhani mnamkomoa rais Magufuli.
Sasa hivi mnamkejeli Makonda kwa kusema ni tasa mnasahau kuwa HalimaMdee ana miaka 45 na hana mtoto wala kutundikwa mimba.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi nyie mashetani kwanininaleta mambo yenu ya siasa kwenye issue ya life and death hivi mnaona kama kamchezo vile au?

Yani unafuraha una take pride kabisa mwanadamu mwengine kuwa mgonjwa what kind of an animal are you ???

Mnafanya the whole black race tuonekane wapuuzi,wasio na akili,washenzi tuliokosa ustaarabu.Hivi jambonla corona ni LA kuleta fun mbele za watu !!!

Italy huko sana record more than seven hindered death in a day, hivi unadhani ikija kuspread Tanzania na hali yetu ya kiuchumi itakuwaje mbona ham contemplate??
Unajuaje next utaumwa wewe? ,mkeo? Watoto wako? Au wazazi wako ?? Do you think its funny making politics in serious pandemics like this ???

Shame on you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi kati mwamba Technically aka kamanda wa Chadema alianzisha uzi hapa akiombea Corona iingie nchini.. Sasa imeingia imeanza na ndugu wa chama chake..😀😆😀hapa ndo hua najiuliza chadema amebaki nani mzima upstairs
 
Mtoto wa Mbowe anaeitwa James Mbowe amesema kuwa ugonjwa wa korona ni janga la kitaifa na halipaswi kufanyiwa mchezo wala mzaha.

Amesema kitendo cha Mh. Makonda ni kitendo cha kushangaza kwa kuwa amejivika usemaji wa familia ya Mbowe kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ugonjwa wa korona umepiga hodi kwenye familia ya Mbowe.

Amesema kuwa kwenye vita dhidi ya korona hatutakiwi kuweka itikadi za vyama bali tulitangulize Taia mbele katika vita dhidi ya korona.

Amesema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho kwa kuwa ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari anaemuhudumia. Hivyo aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kutumia ugonjwa wa korona.




TAARIFA YA FAMILIA YA FREEMAN AIKAELI MBOWE KWA UMMA WA WATANZANIA NA DUNIA.

KORONA NI JANGA KUBWA KULIKO VIONGOZI NA WATANZANIA WENGI TUNAVYODHANI:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, leo asubuhi ametangazia dunia kuwa mmoja wa Wanafamilia wangu (mtoto) amebainika kuwa na virusi vya Corona na pamoja na mambo mengine anamshukuru Mungu kwa janga hili kutokea kwa familia yangu.

Bila kujali Maadili na upotoshaji ulioambatana na taarifa hizo, ni kweli mwanangu Dudley amethibitika kupatikana na virusi vya Corona baada ya kupata homa za vipindi, kuumwa kichwa mfululizo na kukohoa kwa siku tano.

Mama yake, ambaye ni Daktari alipobaini hali hiyo alizitaarifu mamlaka za Serikali zinazoshughulikia Janga hili nazo zilimtaka kijana apelekwe Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kwenye vipimo zaidi ambapo ilithibitika rasmi kuwa ana virusi vya Corona.

Aidha, timu ya Serikali imeendelea kutoa ushirikiano na ufuatiliaji wa karibu kwa familia yote ikiwemo ushauri nasaha kwa wanafamilia na marafiki wengine waliokutana na Dudley katika mikusanyiko mbalimbali ikiwemo kuweka wengine in Isolation au karantini.

Familia yangu inakiri kupokea ushirikiano wa kiwango kilichowezekana kutoka kwa Mamlaka husika za Serikali wakiongozwa na Waziri Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wake, Mganga Mkuu wa Serikali na Wataalam wao wote nikimaanisha Madaktari, Wauguzi nk.

Hali ya Dudley sasa imeimarika. Homa zimekwisha. Kichwa kimepona. Bado anakohoa kiasi na yuko chini ya uangalizi maalum kwenye “isolation”.

Dudley hajasafiri nje ya nchi mwaka huu. Maambukizi haya kayapata ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Ugonjwa huu haupaswi kuwa siri japo kuna miiko inayoongoza utaji wa taarifa za wagonjwa. Tatizo ni kubwa kuliko tulivyojiandaa na tunavyojiandaa.

Wengi wameitafuta familia kutaka kujua ukweli na undani wa jambo hili. Pengine kupitia ushuhuda wangu, tutaweza kuokoa wengi katika nchi yetu. Hakika leo kila mmoja anastahili kujua janga hili
liko mlangoni mwake!

Nimekiri kupata ushirikiano “kwa kiwango kilichowezekana”. Sina uhakika ni wangapi watapata “bahati” hiyo. Nimejifunza mengi. Nazungumza kwa mamlaka ya kuwa mhanga na shuhuda wa hali halisi tuliyo nayo. Tuna mlima mrefu wa kupanda. Hakika Serikali inahitaji msaada. Mlipuko hauko mbali. Tuelezane ukweli tusijechelewa.

Njia mojawapo muhimu ya kulishinda tatizo ni kulikubali na kulikabili kwa nguvu zote na kwa Umoja wetu.

Hatustahili kuchefuliwa na kejeli za Paul Makonda kipindi hiki. Tusiiachie serikali pekee. Tutajuta. Tusiilaumu tu, tuishauri nayo iwe tayari kuupokea ushauri na ishirikishe. Ni janga la Dunia na hakika tutaumizwa kuliko tunavyowaza.

Rai kwa Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Magufuli: Unda timu ya kukusaidia na ushirikishe wadau wengine nje ya Serikali yako. Yako mengi ya kufanya nje ya mikakati ya kitabibu inayosimamiwa na Waziri Mkuu na Waziri Ummy Mwalimu.

Katika maisha maandalizi hayajawahi kuwa hasara, bali hasara iliyo
majuto ni kutokujiandaa na kupuuza yanayofanywa na walioyapitia kama
Ilivyo nchi za wenzetu zilizoendelea na hata nahitaji zetu!

Wengi wako tayari kukusaidia. Chadema tuko tayari kukusaidia na kulisaidia Taifa. Siyo wakati wa kulumbana huu.

Freeman Aikaeli Mbowe
Mkuu wa Familia na Shuhuda wa Janga

Makonda aache kuropoka kutoa taarifa zisizomhusu
 
Mbowe kafanya uzembe ambao utagharim watu wengi
Mbowe hakua na sababu ya kuita press conference ilihali anajua anamgonjwa wa korona nyumban kwake huu ni uzembe unatakiwa kupingwa kwann baada ya kufaham kua mwanae alikua na Corona hakujiweka karantin mpaka ametangazwa na Paul Makonda et leo ndio anasema amejitenga karantin yeye na wafanyakazi Wake
Wakati amesha fanya mizunguko mingi na hata kukutana na watu
MUNGU ainusuru Tanzania mungu atulinde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili ya mbowe na TL inafikiria kuchonganisha Taifa na mabeberu,sasa hao mabwana wao Leo tunaongea lugha moja inaitwa covid 19
 
Wanakuja hao
dd5417584e53a5cbdbcff4de420d3ee7.jpeg
View attachment 1399436
82285956926aa7f042b08097be896c3b.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtoa mada nimekuelewa mako anaropoka lakini kuropoka kwake sometime kunawashtua watu na majanga, imagine dogo kakohoa siku tano hajui ana shida gani, hapo baba yake kashamjulia hali ndugu mpaka marafiki wamemjulia hali, siku ya tano anakuna kujishtukia aisee ni hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom