Fanya hivi ukikutana na wanyama hawa porini

Ukimkimbilia simba umtishe nayeye akakukimbilia mkuu hapo unafanya nini?

Unamkimbilia huku unalia au unageuza unatafuta uelekeo wa wanyama wengine wa mwituni wanaoutafutaga?
😀
 
Nakumbuka mwaka juzi tulikutana na chui mwenye watoto ilikuwa usiku wa saa sita porini kilichotusaidia tulikuwa na mbwa kiherehere cha mbwa kwenda kuvamia watoto wa chui kumbe mama kajificha alichofanywa yule mbwa ilikuwa pona yetu. Yule mbwa alikuwa mtemi ila alibahatika kutoka kwenye mikono ya chui alirudi na donda lilomuachia kovu mpak kesho na alishinda ndan analia kutwa km mtoto.
 
Wanyama wote wakorofi wakiwa na njaa,kasoro Tembo,.
Nyoka anatumia hisia,ukimuona simama hatajua upo wapi ukipiga hatua tu anakufuata.
Katika wote siwapendi fisi kwakua wanakutafuna ukiwa mzima,wao hawaui kwanza
 
Ahsante kwa maarifa, ila hao wanyama ni wale kitendo Cha kusema Yesu kabla hujamaliza na Maria tayari usha rest in peace...


Cc: Mahondaw
 
Wanyama ambao sijawahi kukutana nao ni mbwa mwitu,mamba na chui.
 
Nitawapanga hao wanyama kwa jinsi walivyo hatari;
1. Simba
2. Kundi la mbwa mwitu
3. Mamba akiwa majini.
4. Chui
5. Faru
6. Chatu
7. Nyati
9. Nyoka
10. Fisi
Nyati ndo mnyama hatari
Yeye laZima akitangulize mbinguni
 
Kuna Siku Niko Na Braza Wangu Maeneo Ya Tandahimba Usiku Tuko Kwenye Gari Ghafla Tukagonga Mnyama Tukarudi Nyuma Tukawasha Full Braza Akanimbia Tushuke Tukamcheki Ni Mnyama Gani ?

Tukashuka Hamadi Kucheki Ni Mtoto Wa Chui Tukarudi Fasta Kwenye Gari Tukaondoka Basi Siku Ya Pili Kuanzia Saa 12 Mpaka Saa 4 Hajakatiza Mtu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]vichwa viwili na jicho lenye nywere na shingo hamna daaaah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]*****
 
Huyo mbwa mlimtibu?
 
Kwenye tembo tembea na filimbi hawapendi kelele so ukipiga filimbi anakimbia na wewe kabisa ila kuna tembo wakorofi sana hawa ni wale walio tengwa na familia zao

Nyati akiwa mmoja huna ujanja sanasana hapo ukikimbia lala chini uwe una kroo au kuloli kwa walio pitia jeshi wanaelewa ila wakiwa wengi huwa wao ndio wanakimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…