Huu uzi umenikumbusha kisa changu na mwanamke mmoja hivi kati ya 2008 mpaka 2012.
Ni mwanamke wangu wa kwanza kwenye mahusiano, nililazimika kukaa nae geto kipindi hicho kwa sababu ya shida zake binafsi na nyumbani kwao. Alikuwa amefukuzwa kwao.
Kipindi hiko 2008 ndiyo na miezi kama 5 hivi tokea nipange na kujitegemea hata sikua nimefika mbali kiivile.ndio nilikua naanza maisha hapo hapo na mke juu, na alikua mwanamke wangu wa kwanza.
Nilikua na maisha magumu kwa kiasi kikubwa sana, yule binti aliumwa wa kulala kitandani kama mwaka na nusu hivi, maisha yangu na yule msichana yalikua magumu sana siku pata msaada popote pale iwe nje ama ndani, nilikomaa naye mpaka akapona na mimi nilirudi nyuma kiuchumi kwa kiasi kikubwa .
Ilibidi nimtafutie biashara eneo fulani lenye pilikapilika sana, haikupita miezi mitatu akaniambia amenivumilia sana anaona bora aondoke amepata bwana mwingine mimi ni maskini sana.
Alisahau mimi nilimvumilia mwaka na nusu wa kuugua kwake hata sex ilikuwa no.
Mwishowe akaondoka na vyombo ingawa nilinunua tukiwa nae lakini alibeba vyote akaondoka huku namungalia kwa machozi, kibaya zaidi huko aliko enda olewa na huyo bwana alikuja kumchukua mlangoni kwangu kabisaa.
Ingawa niliumia sana,nilirudi nyuma sana, lakini nilipoona yale maumivu.
Mwanamke huwa inapofika wakati wa kufanya lile linalo mfaa kwa wakati huo huwa haifikirii jana wala kesho, hana huruma hata kama wewe ni nani, hajali machozi ya mtu.
Kwa namna hio wanaume wengi kwa namna moja ama nyingine wameumizwa sana tena sio mara moja au mbili wala tatu, ndio maana kilio na malalamiko yamekua mengi mno.
Mwanamke ni mtu mzuri sana akiwa mama, na binti yako, akitoka hapo haki ya Mungu ishi nao kwa tahadhari sana.