You sound like you have a do-nothing strategy. Hii posture wangekuwa nayo kina Mandela, South Africa mpaka leo ingekuwa bado iko kwenye apartheid system. The same can be said of America and slavery system. Kama hivyo ndivyo unavyotaka, basi afadhali uwaache wahangaikaji wahangaike!
Tanzania itarudishwa kwenye mstari na Watanzania ambao wako tayari kuifia. Obviously, wengi watakufa kabla haijarudi kwenye mstari. That’s Okay because repressive regimes don’t usually go down without firing a shot.
Ukishaanza habari na "you sound like" hata wewe mwenyewe huna uhakika na hoja yako.
Umemtaja Mandela.
Mandela hakuandamana bila strategy.
Aliunda "Umkotho we Sizwe" watu wakapigana kuikomboa nchi yake.
Wewe "Umkontho we Sizwe" yako iko wapi?
Alijipanga kukomboa nchi mpaka akatumia passport ya Tanzania kusafiri nje ya Afrika ya Kusini kujenga mtandao wa nje kuwabana makaburu.
Wewe mtandao wako wa nje uko wapi? Nani anauongoza?
Mandela aliweka strategy ya kimataifa kuibana serikali ya makaburu.
Wewe unafanya nini zaidi ya kuandamana tu na kujifanya target ya kupigwa na kuuawa na polisi wa CCM?
Ukitoka juandamana siku ya uchaguzi utapigwa, watu watauawa kama walivyouawa Pemba na Mkapa.
Samia kashasema hakuna nyinywinywi wala nywanywanywa, uchaguzi utafanyika.
Maana yake mkitoka kuandamana mtapigwa virungu na risasi. Watu watakufa. For what? What will you achieve?
Halafu serikali itasema hawa wahuni walikuwa wanataka kuharibu uchaguzi tumewashughulikia. Tumelinda haki za kikatiba za Watanzania wanaopenda amani kufanya uchaguzi bila bughudha.
Na watu tunaotetea haki ya watu kuandamana tutapata tabu kutetea maandamano yanayongoja siku ya uchaguzi wakati kuna siku nyingine 364 za kuandamana.
Kuandamana kutawasaidia nini?