GE2025 Faris Buruhani: Maandamano ya Oktoba 29 yaishie Mitandaoni, Bukoba UVCCM hatutawaachia Polisi, tutashughulika nao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Watu hata wakiandamana mwezi mmoja kabla ya uchaguzi watapigwa, watajeruhiwa na kuuwawa tu. Kwanza wengi wamaepigwa, kujeruhiwa na kuuwawa kwa madogo zaidi ya hili.
 
You sound like you have a do-nothing strategy. Hii posture wangekuwa nayo kina Mandela, South Africa mpaka leo ingekuwa bado iko kwenye apartheid system. The same can be said of America and slavery system. Kama hivyo ndivyo unavyotaka, basi afadhali uwaache wahangaikaji wahangaike!

Tanzania itarudishwa kwenye mstari na Watanzania ambao wako tayari kuifia. Obviously, wengi watakufa kabla haijarudi kwenye mstari. That’s Okay because repressive regimes don’t usually go down without firing a shot.
 
Watu hata wakiandamana mwezi mmoja kabla ya uchaguzi watapigwa, watajeruhiwa na kuuwawa tu. Kwanza wengi wamaepigwa, kujeruhiwa na kuuwawa kwa madogo zaidi ya hili.
Sasa wakiandamana wanapigwa, wanauawa.

Halafu hakuna kinachobadilika.

Deus Soka kahimiza maandamano, kaandamana, kauawa.

Kaswahili kaandamana, kauawa.

Hamuoni kuandamana tu bila mpango mwingine ni ujinga?

You are becoming sitting ducks for killers to shoot you down.

Mnaandamana ili iweje? Muuawe?

Zaidi ya kuandamana mnafanya nini?
 
Ukishaanza habari na "you sound like" hata wewe mwenyewe huna uhakika na hoja yako.

Umemtaja Mandela.

Mandela hakuandamana bila strategy.

Aliunda "Umkotho we Sizwe" watu wakapigana kuikomboa nchi yake.

Wewe "Umkontho we Sizwe" yako iko wapi?

Alijipanga kukomboa nchi mpaka akatumia passport ya Tanzania kusafiri nje ya Afrika ya Kusini kujenga mtandao wa nje kuwabana makaburu.

Wewe mtandao wako wa nje uko wapi? Nani anauongoza?

Mandela aliweka strategy ya kimataifa kuibana serikali ya makaburu.

Wewe unafanya nini zaidi ya kuandamana tu na kujifanya target ya kupigwa na kuuawa na polisi wa CCM?

Ukitoka juandamana siku ya uchaguzi utapigwa, watu watauawa kama walivyouawa Pemba na Mkapa.

Samia kashasema hakuna nyinywinywi wala nywanywanywa, uchaguzi utafanyika.

Maana yake mkitoka kuandamana mtapigwa virungu na risasi. Watu watakufa. For what? What will you achieve?

Halafu serikali itasema hawa wahuni walikuwa wanataka kuharibu uchaguzi tumewashughulikia. Tumelinda haki za kikatiba za Watanzania wanaopenda amani kufanya uchaguzi bila bughudha.

Na watu tunaotetea haki ya watu kuandamana tutapata tabu kutetea maandamano yanayongoja siku ya uchaguzi wakati kuna siku nyingine 364 za kuandamana.

Kuandamana kutawasaidia nini?
 
Wapinzani wa Tanzania mko performative sana.

Yani mnaweza ku act hata kama hakuna audience.
 
Siwezi kujua for sure strategy unayosimamia kwasababu hujaibainisha, lakini unaonekana kama mtu ambaye unasimama na do-nothing strategy. Kama unasimama na strategy tofauti na hiyo, basi iseme tuijue. Otherwise, waache wahangaikaji wahangaike. They’re ready to die for their cause. BTW, katika historia ya mwanadamu, hakuna ukombozi uliowahi kupatikana overnight. Ni perennial exercise. Wapambanaji wengi hufa bila kufaidi matunda ya struggles zao, lakini hilo haliwasumbui. That’s just the nature of the beast!

Mimi sio mmoja wa wale wanaoratibu maandamano, lakini sipingi wanachopanga kufanya kwasababu (1) I have nothing better to offer, ukizingatia mazingira ya kisiasa waliyomo (2) I am not privy to their strategy.

Armed struggle ya kina Mandela (through MK) haikuwepo from the beginning. Ilikuwa phase II ya struggle yao. Hiyo haina maana kwamba hawakufanya civil disobedience mpaka walipoanzisha MK. Waliandamana sana na watu wengi waliuawa na vyombo vya dola vya makaburu. That didn’t stop them from protesting! It’s an honor kwa mtu kufa akipigania haki kubwa kama hiyo. That’s what keeps wapigania ukombozi going!
 
Bado unarudia non sequitur fallacy.

Maandamano siku ya uchaguzi si strategy.

Ni performance arts tu.

Mnajifurahisha wenyewe.
 
Kwa sababu na wao wanajifanyia wanachojisikia.

Hata wakiiba kura, kwa kanuni yako hiyo, itakuwa sawa tu

Dah

Huyo uvccm anaongea Kwa kujiamini kwamba polisi wapo kwaajiri yao
 
Ilifikia upinzani
Wanawachomea nyumba wana CCM kama wao walivyokuwa manachomea upinzani ofisini zao
Watapenda? Au jinai?!
Je na ndugu zao wakipotezwa na kutekwa watajisikiaje?!

Haki sawa Kwa wote
 
Sasa hapa kuna "falsafa" gani kama siyo kujiondoa akili kichwani mwenyewe!

Kwanza hiyo "falsafa" yako ingekuwezesha kujiuliza kama kweli huu ni uchaguzi au ni uchafuzi!

Hii falsafa yako inaona tu HAKI ya hao waytakaozuiwa kwenda kwenye "uchafuzi", lakini huoni HAKI ya wale ambao wamenyimwa kabisa hata kuwaendea wananchi na kuwaeleza kwa nini wachaguliwe wao badala ya haya majambazi unayotaka yakafanye najisi na kudai kuwa yamechaguliwa kwa kura feki.
 
Bado unarudia non sequitur fallacy.

Maandamano siku ya uchaguzi si strategy.

Ni performance arts tu.

Mnajifurahisha wenyewe.
Haki ya kikatiba ya watu kuandamana peacefully haikomi siku ya uchaguzi. Kama wamepanga kuandamana siku ya uchaguzi na iwe hivyo. And it makes sense kwasababu mchakato wa uchaguzi ndiyo kiini cha hayo maandamano.

The do-nothing strategy you embrace is capitulation at best!
 
Haki ya katiba ni mwanzo tu wa kuamua kitu, si mwisho.

Strategically utapata nini kuandamana siku ya uchaguzi?

Unatakiwa kufanya cost benefit analysis mathematics kujua kufanya mambo strategically, sio kuandamana kama nyumbu uuawe tu.

Hujaweza kujibu hili swali.

Far from advocating a do nothing strategy, you are the one who is advocating a do nothing non strategy.

Maandamano siku ya uchaguzi is just performative politics. That is not doing anything.

I am challenging you to do something instead of acting in this useless show.
 
Hii kauli ingetolewa na mwanachadema nadhani angekuwa ameshapotezwa
 
Unaishi sayari gani? Come down on earth… Hakuna siku ya maandamano dhidi ya watawala ambayo ni safe kwenye hii nchi. Ukiandamana hata leo utashughulikiwa just as ruthlessly. Kumbuka, kuna watu wamevunjwa miguu kwasababu tu wamekwenda mahakamani (open court) kuhudhuria kesi inayomkabili Lissu.

Tupe mathematical cost-benefit analysis uliyofanya ya kuandamana siku ambayo siyo ya uchaguzi.

Mwisho, tuambie nini kifanyike ili Tanzania irudi kwenye mstari. Kama huna jawabu, waache walio tayari kuifia nchi yao waifie.
 
Acha porojo zako hizo hiyo tareh 29 nayo ni siku kamae zingine
 
Kuna sehem kwenye katiba imeweka siku au tareh sahihi ya kunandamana?
Bado unarudia non sequitur fallacy.

Maandamano siku ya uchaguzi si strategy.

Ni performance arts tu.

Mnajifurahisha wenyewe.
Sasa kinachokuwashawasha nini kama wao wameamua kujifurahisha wenyewe
 
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera ndugu Faris Buruhani, amewasihi na kuendelea kuwaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kwenda kupiga kura nyingi kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi na kuachana na upotoshaji unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uvunjifu wa amani siku hiyo ya uchaguzi. Ndugu Faris amesema ubora, uweledi na umahiri wa wagombea walioletwa na CCM kwa wananchi, ni kielelezo tosha cha wananchi kuwapigia kura nyingi ili wakaisimamie Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 inayolenga kusogeza huduma kwa wananchi. Ndugu Faris ameyasema hayo Septemba 23, 2025 kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Injinia Johnston Mutasingwa uliofanyika kwenye kata ya Kibeta na kuhudhuriwa na wananchi wengi wa Kibeta na Bukoba mjini kwa ujumla.
 
Huyu si ndo alisema wakiwapoteza wapinzani, Polisi wasihangaike?
Au sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…