Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Mi sijasema anatambulika kisheria, nimebainisha kuwa msimamo wa Feisal ndio kile alichokizungumza mzazi wake

Kwa hiyo kama mzazi ali demand kila kitu kiwekwe bayana that's means na Feisal anakubaliana na kitu hicho
mashudu
 
Naomba kuuliza
Kwenye mkataba si kuna kipengele cha kuvunja?? Na inatakiwa ifanyike hivi na hivi, sasa km mtu kavunja kwa kufuata matakwa shida iko wapi???
mkataba hauvunjwi kwa kipengele kimoja tu
 
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo tarehe 2 Machi, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Young Africans kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Young Africans.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi

Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali hivyo imetupilia mbali shauri hilo.

Sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo siku ya Jumatatu 6 Machi, 2023.

Nafananisha na suala la Halima Mdee na wenzake dhidi ya CHADEMA.
Ngoma itachezwa mpaka mkataba wake na Yanga utaisha rasmi.
 
Wee ndo unaetaka kudanganya watu hapaaa, as if shule uelewa unao pekee ako. Usituchoshee bhana wee.
Nenda kwenye nyuzi zako huku huna uelewa, mtu akae nyumbani asubiri mkataba uishe awe huru? Ingekua hivyo Fei si angekaa asubiri hio 2024 unadhani anakomaa sababu ya nini?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kwamba mzee wa Ugali na sukari ameangukia pua

Hii ni baada ya TFF kukosa msingi wa kisheria wa kubadili uamuzi wake wa awali

Sasa ni hiyari yake kusuka au kunyoa, bali nawaomba viongozi wa Yanga wamhurumie huyu kijana aende atakako, kumkomoa haitasaidia chochote.

Yanga Mshahara wenu mdogo sana, mwacheni huyo kijana akale Ugali na mboga sasa, milion zenu hizo 4 zinatosha unga, sukari na mkaa tu.

b16c33a3-3c34-402c-b775-292ddb8d8762-jpeg.2535203
Kwani yanga ipo pale kuhurumia watu?Yani ikihijumiwa yanga sio tatizo,waliompotosha ndio wamhurumie
 
Huu ni mfano namna watanzania tusivyopendana.
 
Back
Top Bottom