Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Naona Fatuma Karime amejitahidi kumlisha Dogo nondo za kujitetea CAS. Ila nadhani Dogo anapoteza mda tu.

Kwanza, toka alipojua mkataba umeongezwa Miaka, alichukua hatua mara Moja au aliendelea nao kwa Miaka kadhaa ndipo akafanya maamuzi hayo?

Pili, Mama ya Fei anatambuliwa katika huo mkataba Hadi awe analumbana na Yanga. Is/was She privy to the contract.

Tatu, Sheria za FIFA zinasemaje kuhusu kuvunja mikataba?

Huyo Shangazi Fatuma anachofanya ni kitu wanasheria wanaita "ku-test the law", ila hapa wanacheza bahati nasibu.
 
Chuki za kishamba hizi,
Huyu dogo Kuna watu wanampotosha kwa maslahi Yao BINAFSI[emoji3525]
Kama hakuikimbia yanga kipindi cha njaa basi asikilizwe vizuri hata kama hajui kujieleza, kitu cha msingi hakuna maelewano maziluri kati ya raisi wa klabu na mchezaji, huku raisi akitoa lugha ambazo ni za kibaguzi kitu ambacho pia ni kosa kwenye michezo, na ni muda sahihi sasa kwa wachezaji kuwa na management na wanasheria.
 
Yani Hersi atume watu wamtukane Feisail na Mama?!

Nitakua wa mwisho kuamini hii. Kuhusu mkataba naweza kuamini, Bongo magumashi mengi.

Tusubiri upande wa pili kama wataona inafaa kujibu.
Kwanini isiwezekane? Kwani Malaika?

Huyu si aliita mashabiki wa Yanga wala mihogo, huyu si aliwapigia Video call Kisinda na Razak wakiwa Berkane kuwa wakija Dar atawasaidia kuwapa mbinu ya Simba.
 
Haya wana Yanga SC mnaomtaka Feisal Salum 'Feitoto' muondoeni upesi Uongozini Rais wenu Injinia Hersi Said ili arejee hata leo.

Chanzo Taarifa: Jemedari Said Bin Kazumari akiongea Mubashara muda mfupi uliopita katika Kipindi cha Michezo cha EFM cha Sports Headquarters.

Kazi ipo....!!
Huyu binti Kazumari na Fei mtoto itakuwa wanagonga kizamuzamu, wote machoko fresh.
 
Mara Manyanyaso,Ghalib kamsema vibaya,Mara Hersi. Yaani tumtoe Hersi kisa ww urudi yaani unajiona ww Yanga ndio kila kitu.Wewe kama umeamua kuendesha mambo kihuni, Yanga inaendesha mambo kisheria,endelea kuchangisha hela tutakutana CAS.
Screenshot_20230601_093020_Instagram.jpg

Tumtoe Hersi mmoja wa aliyefanya Yanga ipate msimu bora wa mafanikio kuliko misimu yote kisa utoto wako.
 
Kuna interview moja Feisal alifanya na Azam, akasema Simba walienda na dau dogo akakataa leo anasema Simba walitoa 25 Yanga akatoa 10, ni vile tuu hawa watangazaji wetu hua hawana taarifa za kutosha,
Ile interview ya leo Clouds walipaswa wawe na mtu wa michezo pia
Watu wa michezo wameshaingia sasa... hata mada zimeanza kueleweka
 
Inawezekana upo sawa ila Dogo ameshasema tangu anasaini mkataba alisaini kwa kumuamini Hersi, hata mkataba hakuchukua Kumbe Hersi walichozungumza sicho alichokiandika kwenye mkataba.

Hili ni tatizo ambalo kisheria atashindwa ila ni wazi kuwa kuna kiongozi anafanya maisha ya Fei hapo Yanga kuwa magumu. Kama ni sahihi, Katika mazingira haya mchezaji anaweza kuamua potelea mbali,IMETOSHA ngoja nijaribu nikishindwa nitakaa mtaani.
Katika hali ya kawaida ukifikiria utagundua kuwa hiyo miaka ilyoandikwa kwenye mkataba aliijua na aliridhika nayo. Nasema hivyo kwasababu baada ya Feisal kusaini mkataba wa kuongeza miaka Yanga, vyombo vya habari vikaripoti kuwa Feisal asaini miaka mitatu Yanga. Ina maana Feisal sio mfuatilia wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kiasi kwamba asijue kumbe maandishi yameenda kinyume na tulivyoongea mdomoni? Kwanini alilikalia kimya swala la muda wa mkataba kipindi chote hiko?
 
Mara Manyanyaso,Ghalib kamsema vibaya,Mara Hersi. Yaani tumtoe Hersi kisa ww urudi yaani unajiona ww Yanga ndio kila kitu.Wewe kama umeamua kuendesha mambo kihuni, Yanga inaendesha mambo kisheria,endelea kuchangisha hela tutakutana CAS.
View attachment 2642150
Tumtoe Hersi mmoja wa aliyefanya Yanga ipate msimu bora wa mafanikio kuliko misimu yote kisa utoto wako.
Yani kwa kifupi anasema waondoke GSM yeye ndio arudi Yanga.

Yani mtoto wa kiume akishaanza kuinamishwa basi kichwani kunabaki empty.

Hivi hii Kenge yeye ndio angekuwa Mayele ingekuwaje?
 
Hili ni funzo kwa TFF, wachezaji, na timu.

1. TFF wazibane timu kuandaa mikataba kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wachezaji wa Kitanzania wasiojua Kiingereza.

2. Wachezaji wawatumie mawakala pamoja na wanasheria kutafsiri mikataba.

3. Ziache ubabaishaji wa kutaka mchezaji mzuri kwa bei ndogo.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo maana watu husaini mbele ya kamera na kutaja miaka waliyosaini. Kama hana ushahidi wa hilo afanye kazi yake, akubali hali.
 
Back
Top Bottom