Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Kweli una hasira sana. Kunywa maji upumzike
 

La ethipia sidhani kama project nzima imeisha .. nafikiri ndo kwanza wamejaza maji awamu ya kwanza na inaweza chukua zaidi ya 3 yrs . Hizi project si mchezo. Kujaza maji tu ni miaka achana na kujanga
 
Ali go big kwenye nini sasa...miaka yake 5 alikamilisha nini ambacho tutasema kweli hiki kimebadili maisha ya watz kwa deni la trilioni 78 aliloacha?
Trillion 78? Sio kweli
Kuna vitu vingi tunaweza kumdiscredit na vipo wazi tu. Ila Kuna vingine naona tunakwepesha maana.
Hakuacha deni la trillion 78.
Kuna mtu nilimuambiaa humu siku flani, kuwa kila raisi atayekuja atakopa sana kwa sababu miakaa inavyozidi kwenda inflation ndio inaongezeka na hivyo tutahitajk pesa zaidi.
Kama mwaka 2005 tulihitaji mil 5 kujenga darasa moja, mwaka 2017 tukahitaji mil 15, mwaka 2021 tukahitaji mil 20 ,basi mwaka 2030 tutahitaji mil 40 kwa darasa moja. Hivyo raisi atayekuja huko atakopaa Sana kuliko Hawa waliotangulia.
Solution ni nchi kuzalisha sana na kupata pesa kitu ambacho tumeshindwa kabisa
 
Kwa nini Ujerumani isikae session kujadili mradi ulioko Selous wakati wao wanatoa mamilioni ya dolari kusupport uhifadhi wa hiyo mbuga? Hiyo ndiyo tafauti baina yao na sisi. Watz tumefadhili mradi gani nje ya nchi yetu?

Yanatushinda ya kwetu tunasubiri kikombe tugaiwe ndiyo tufanye conservation - Selous, Ngorongoro, Tarangire..... endelea.
 
Ongezea na gharama kubwa sana za kuhamisha maofisa na maofisi ambazo hazikuwepo kwenye mpango wa miaka mitano wa maendeleo.
 
waondoe ufadhili wao sababu Bwawa ni bora kwetu kuliko mbuga ambazo tunazo nyingi mno!!
 
Nani kasema aliuawawa?
Unataka kusema hujawahi kusikia kwenye mitandao hadi You tube huko watu wanaongelea hayo? Hata SSH mwenyewe aliwahi kulisemea hili akasema walio na ushahidi wapeleke vyombo vya usalama vifanyie kazi la sivyo wakae kimya. Au mwenzetu unaishi nje ya TZ?
 
ok, umeshinda mkuu maelezo mazuri! hata mimi naamini hivyo
 
Kwani shida ni construction yenyewe au pesa?, swala sio ukubwa wa project ila ni makubaliano ya pande mbili ndo kuna shida, maana serikali inatoa requirements zake kwa wazabuni wanao omba tender pamoja na kuangalia uwezo wa kumpuni kujenga ( Technical & financial capabilities), pia wazabuni huandaa technical design ya mradi huo , layouts baada ya kutembelea eneo husika, baada ya hapo wana toa taarifa kwa wahusika, wana review kama kuna marekebisho utaenda kurekebisha, layouts ndo inaonyesha workload ya kazi yote na muda utaokaotumika katika kujenga huo mradi, baadaye wanakuja na project milestone kuanzia contract signing, payment yaani serikali kufaya malipo kwa mzabuni, mzabuni kuandaa vifaa baada ya kupokea malipo, manufacturing, shiping, clearance, office setup in Tz, site acquisition, site clearance,project inauguration /Kickoff meeting hadi kuanza site/project implementation na phase zake zote, hii duration yote huwa imekuwa reviewed by both two parties, agreed and compiled in contract and signed, lazima mjiridhishe kila kitu na kutambua matatizo yote ya mradi kwa pande zote mbili, watalaam wetu wote pande mbili wanajua na walikubaliana, kama ni three years basi ni miaka mitatu tu na kama kuna delay basi mzabuni hutoa taarifa na kuakaa kuzungumza, kwa hiyo sio sahihi kuja na kusema kwa kuwa mradi wa xxx mdogo ulijengwa kwa miaka 10 basi huu ni miaka 20 in which basis? , kwani katika mazungumzo ya awali , technical discussion hamkuona hilo? sasa kuna haja gani ya kuwa na watalaam wasio jua kitu hadi waanze kazi bila kujua na leo ndo wana kuja na blablabla?

In facts, ngoja tuseme ukweli, miradi mingi or breach of contracts nyingi chanzo kikubwa ni pesa, sijui agreements za serikali za mzabuni wa Nyerere hydropower project, but i'm sure kwa serikali hii, sijui kama inatekeleza makubaliano, ndo maana wana rukaruka, serikali hii ni broke, hawana pesa, katibu wa wizara hajengi bwawa, yeye ni facilitator tu na mpokeaji wa taarifa za ujenzi kutoka kwa mjenzi, hivi leo hii huyo Mzabuni baada ya kujenga phase 1 akakuambia unajua ujenzi huu sio wa miaka 20 huu unachukua miaka 40 katibu mkuu atakubali tena? thats what we agreed? ni lazima uwe na akili ya kulogic kwanini under evaluation stage hukusema kitu kama hicho? hiyo ni breach of contract, lakini i'm sure 100% serikali haitoi pesa , wanatufuta tu huruma kwa wananchi.
 
Mramba bana, JNHPP ni mara mbili tu ya mtera. Mara 10 sio kweli.
Ingekua Mara 10 tusingeweza, yaani tujenge 6000sqkm??? Ndio wataalamu wetu hao
Lkn ndiyo kasema hivyo mkuu. Tazama clip. Ndiyo kusema kadanganya umma??
 
Yule boss wa awamu ya 5 alikuwa na nia njema lakini uwezo wake wa kupangilia mambo ulikuwa mdogo Sana. Aliendeshwa na mihemko ya kutaka sifa.

Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa
Alikuwa anawaona watangulizi wake hawana akili na uzalendo, akajaribu Ku adopt tufunge mkanda kama Nyerere.
Kumbe wenzie walikuwa wanaona ni bora kwenda polepole huku wakisaidiana na sector binafsi, wakiwaongezea watumishi mishahara huku wakijenga barabara na madaraja taratibu, wakikaa mbali na manunuzi ye ndege Kwa keshi na hawakujenga airports makwao!

Sisi siyo matajiri kihivyo! Alivyoamini!
 
This guy ni kichwa.
 

Bwawa la JNHPP lisipo kamilika kabla ya 2025 CCM haina la kuwaambia watanzania.​

Hata ccm wasipokamilisha na wakakosa cha kuwaambia wananchi watafanywa nn? Na nani na kivipi?

Time, polisi, tiss na wakurugenzi wote ni wa ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…