Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Katibu mkuu hajaeleza hayo unayoeleza wewe, na ningetegemea kuwa anao uwezo mzuri kabisa wa kuelezea hayo kwa ufasaha mkubwa na akaeleweka.

Kuna shida gani kwa serikali hii iliyopo sasa kukaa chini na kuchambua miradi yote hiyo na kuona uwezo uliopo na kinachowezekana kufanyika halafu wakaelezea hali halisi ilivyo kwa wananchi!

Lakini ngoja nikuache na hili wazo: pamoja na 'ukichaa' mwingi aliokuwa nao Magufuli, upande ambao unabaki kuwa sifa kubwa kwake ni hiyo 'daring', hata kama ilikuwa ni ya pupa bila kutumia akili. Na nadhani, huku kuliliwa na wengi licha ya tabia zake mbaya inatokana na huo uthubutu wake.

Kuna kosa gani hata kama ni kukopa kukamilisha mradi muhimu kabisa kama Bwawa la Mwalimu Nyerere!

Haya yote wanayofanya hawa waliopo sasa ni kinyume kabisa, na ni dhahiri sasa wanategeshea kuingiza upigaji kwenye miradi mingi. Kazi kubwa inayokuja ni kutafuta na kuwatumia wapigaji tu waje hapa kutunyonga, hiyo ndiyo mikakati yao wanayoiweka mbelke.

Umezungumzia Dodoma mahali..., hiyo ni aina ya uthubutu ambayo imempambanua huyu kichaa aliyetokea kuwepo wakati huo, na hili kiukweli kalimaliza. Hutegemei tena serikali kurudi Dares Salaam hata wafanye nini hawa mashetani waliopo sasa hivi.
Kweli una hasira sana. Kunywa maji upumzike
 
Hongera sana Bw. Felchesmi Mramba... Kumbe wenye akili kubwa bado wapo.

Kujenga a mega project kama JNHP kwa kasi waitakayo wananchi na wanasiasa ni kujitegea time bombs.

Sijui wengine akili wanaziweka wapi wanapojadili masuala nyeti, muhimu na hatari kwa maendeleo na uhai. Ndiyo tunahitaji umeme wa uhakika lakini tujue kuwa miradi ya mabwawa ya umeme ni hatarishi. Inahitaji muda na umakini!

Pamoja na mambo mengine... nchini Ethiopia Grand Ethiopian Renaissance Dam ujenzi ulianza 2011 na kukamilika 2020. GERD imeanza kazi 2022.

Tujiandae kisaikolojia. JNHP itachukua muda mrefu zaidi.

La ethipia sidhani kama project nzima imeisha .. nafikiri ndo kwanza wamejaza maji awamu ya kwanza na inaweza chukua zaidi ya 3 yrs . Hizi project si mchezo. Kujaza maji tu ni miaka achana na kujanga
 
Ali go big kwenye nini sasa...miaka yake 5 alikamilisha nini ambacho tutasema kweli hiki kimebadili maisha ya watz kwa deni la trilioni 78 aliloacha?
Trillion 78? Sio kweli
Kuna vitu vingi tunaweza kumdiscredit na vipo wazi tu. Ila Kuna vingine naona tunakwepesha maana.
Hakuacha deni la trillion 78.
Kuna mtu nilimuambiaa humu siku flani, kuwa kila raisi atayekuja atakopa sana kwa sababu miakaa inavyozidi kwenda inflation ndio inaongezeka na hivyo tutahitajk pesa zaidi.
Kama mwaka 2005 tulihitaji mil 5 kujenga darasa moja, mwaka 2017 tukahitaji mil 15, mwaka 2021 tukahitaji mil 20 ,basi mwaka 2030 tutahitaji mil 40 kwa darasa moja. Hivyo raisi atayekuja huko atakopaa Sana kuliko Hawa waliotangulia.
Solution ni nchi kuzalisha sana na kupata pesa kitu ambacho tumeshindwa kabisa
 
Hivi mkuu unajua Bunge la Ujerumani lilikaa session kibao kuzungumza na kupinga mradi wa Nyerere Dam eti unaharibu mazingira hebu fikiria umbali uliopo kati ya Tanzania na Germany wao inawaharibia mazingira gani? Lini sisi bunge letu limekaa kujadili mambo ya miradi ya nchi ingine? Magufuli will always remain a hero.
Kwa nini Ujerumani isikae session kujadili mradi ulioko Selous wakati wao wanatoa mamilioni ya dolari kusupport uhifadhi wa hiyo mbuga? Hiyo ndiyo tafauti baina yao na sisi. Watz tumefadhili mradi gani nje ya nchi yetu?

Yanatushinda ya kwetu tunasubiri kikombe tugaiwe ndiyo tufanye conservation - Selous, Ngorongoro, Tarangire..... endelea.
 
Lakini hufahamu hasara na adha waliyopata waliohamia Dodoma bila maandalizi ya kutosha. Kwanza vifaa vingi vya ofisi viliharibika wakati wa usafirishaji. Pili ofisi hazikuwepo na kujibanza UDOM na baadhi ya Wizara kwenye majengo mengine ya kupanga. Tatu ofisi za muda zilizojengwa Mtumba ni ndogo mno ofisi inayotakiwa kukaa afisa 1 kuna maafisa 4 . Chumba cha maafisa 6 wanakaa hadi 15!! Utadhani darasa!!!

Kati ya 2018 hadi sasa baadhi ya ofisi zilikuwa hazijahama. Kulikuwa na movement kubwa sana kati ya Dar na Dodoma kupeleka majalada na kuyarudisha. Gharama za kuitisha mikutano Dodoma maafisa kutoka Dar ni lazima waende. Kwa ufupi Gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa. Si ajabu bado zipo.

Mwisho hakuzingatia social aspect ya kuhamisha watu bila maandalizi. Ndoa nyingi sana ziliyumba. Kwa hiyo kusifu kuwa aliweza kuhamisha sana but with a lot of consequences. Angehamisha lakini kwa utaratibu maalum.
Ongezea na gharama kubwa sana za kuhamisha maofisa na maofisi ambazo hazikuwepo kwenye mpango wa miaka mitano wa maendeleo.
 
Kwa nini Ujerumani isikae session kujadili mradi ulioko Selous wakati wao wanatoa mamilioni ya dolari kusupport uhifadhi wa hiyo mbuga? Hiyo ndiyo tafauti baina yao na sisi. Watz tumefadhili mradi gani nje ya nchi yetu?

Yanatushinda ya kwetu tunasubiri kikombe tugaiwe ndiyo tufanye conservation - Selous, Ngorongoro, Tarangire..... endelea.
waondoe ufadhili wao sababu Bwawa ni bora kwetu kuliko mbuga ambazo tunazo nyingi mno!!
 
Nani kasema aliuawawa?
Unataka kusema hujawahi kusikia kwenye mitandao hadi You tube huko watu wanaongelea hayo? Hata SSH mwenyewe aliwahi kulisemea hili akasema walio na ushahidi wapeleke vyombo vya usalama vifanyie kazi la sivyo wakae kimya. Au mwenzetu unaishi nje ya TZ?
 
Unataka kusema hujawahi kusikia kwenye mitandao hadi You tube huko watu wanaongelea hayo? Hata SSH mwenyewe aliwahi kulisemea hili akasema walio na ushahidi wapeleke vyombo vya usalama vifanyie kazi la sivyo wakae kimya. Au mwenzetu unaishi nje ya TZ?
ok, umeshinda mkuu maelezo mazuri! hata mimi naamini hivyo
 
Kwani shida ni construction yenyewe au pesa?, swala sio ukubwa wa project ila ni makubaliano ya pande mbili ndo kuna shida, maana serikali inatoa requirements zake kwa wazabuni wanao omba tender pamoja na kuangalia uwezo wa kumpuni kujenga ( Technical & financial capabilities), pia wazabuni huandaa technical design ya mradi huo , layouts baada ya kutembelea eneo husika, baada ya hapo wana toa taarifa kwa wahusika, wana review kama kuna marekebisho utaenda kurekebisha, layouts ndo inaonyesha workload ya kazi yote na muda utaokaotumika katika kujenga huo mradi, baadaye wanakuja na project milestone kuanzia contract signing, payment yaani serikali kufaya malipo kwa mzabuni, mzabuni kuandaa vifaa baada ya kupokea malipo, manufacturing, shiping, clearance, office setup in Tz, site acquisition, site clearance,project inauguration /Kickoff meeting hadi kuanza site/project implementation na phase zake zote, hii duration yote huwa imekuwa reviewed by both two parties, agreed and compiled in contract and signed, lazima mjiridhishe kila kitu na kutambua matatizo yote ya mradi kwa pande zote mbili, watalaam wetu wote pande mbili wanajua na walikubaliana, kama ni three years basi ni miaka mitatu tu na kama kuna delay basi mzabuni hutoa taarifa na kuakaa kuzungumza, kwa hiyo sio sahihi kuja na kusema kwa kuwa mradi wa xxx mdogo ulijengwa kwa miaka 10 basi huu ni miaka 20 in which basis? , kwani katika mazungumzo ya awali , technical discussion hamkuona hilo? sasa kuna haja gani ya kuwa na watalaam wasio jua kitu hadi waanze kazi bila kujua na leo ndo wana kuja na blablabla?

In facts, ngoja tuseme ukweli, miradi mingi or breach of contracts nyingi chanzo kikubwa ni pesa, sijui agreements za serikali za mzabuni wa Nyerere hydropower project, but i'm sure kwa serikali hii, sijui kama inatekeleza makubaliano, ndo maana wana rukaruka, serikali hii ni broke, hawana pesa, katibu wa wizara hajengi bwawa, yeye ni facilitator tu na mpokeaji wa taarifa za ujenzi kutoka kwa mjenzi, hivi leo hii huyo Mzabuni baada ya kujenga phase 1 akakuambia unajua ujenzi huu sio wa miaka 20 huu unachukua miaka 40 katibu mkuu atakubali tena? thats what we agreed? ni lazima uwe na akili ya kulogic kwanini under evaluation stage hukusema kitu kama hicho? hiyo ni breach of contract, lakini i'm sure 100% serikali haitoi pesa , wanatufuta tu huruma kwa wananchi.
 
Mramba bana, JNHPP ni mara mbili tu ya mtera. Mara 10 sio kweli.
Ingekua Mara 10 tusingeweza, yaani tujenge 6000sqkm??? Ndio wataalamu wetu hao
Lkn ndiyo kasema hivyo mkuu. Tazama clip. Ndiyo kusema kadanganya umma??
 
Yule boss wa awamu ya 5 alikuwa na nia njema lakini uwezo wake wa kupangilia mambo ulikuwa mdogo Sana. Aliendeshwa na mihemko ya kutaka sifa.

Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa
Alikuwa anawaona watangulizi wake hawana akili na uzalendo, akajaribu Ku adopt tufunge mkanda kama Nyerere.
Kumbe wenzie walikuwa wanaona ni bora kwenda polepole huku wakisaidiana na sector binafsi, wakiwaongezea watumishi mishahara huku wakijenga barabara na madaraja taratibu, wakikaa mbali na manunuzi ye ndege Kwa keshi na hawakujenga airports makwao!

Sisi siyo matajiri kihivyo! Alivyoamini!
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2244046
This guy ni kichwa.
 

Bwawa la JNHPP lisipo kamilika kabla ya 2025 CCM haina la kuwaambia watanzania.​

Hata ccm wasipokamilisha na wakakosa cha kuwaambia wananchi watafanywa nn? Na nani na kivipi?

Time, polisi, tiss na wakurugenzi wote ni wa ccm.
 
Back
Top Bottom