Fisi aliyeuawa kwa risasi 49, wananchi wagawana nyama

Mkuu huku usukumani fisi akiuawa wanagawana hadi ngozi, ni kawaida yao.

Kuna siku fisi alionekana kwenye chemba za mtaro katikati ya manispaa ya kahama,wakaitwa maafisa wanyama wakampiga risasi
Nilishangaa watu wanavyomgawana kipande kipande.

Nahisi wanafanyia uganga/ushirikina fulani, maana hata mtu akipata kakipande ka ngozi anasepa nako.
 
Wanabodi,

Tarehe 25/07/2021 imeripotiwa tukio la fisi kushambulia na kuua mtoto wa mwaka mmoja na nusu.

Tukio hilo limetokea karibu na Hifadhi ya Lugoya huko Kaliua...
Huyo alikuwa commando, nyie mnatuna kuluta kumpiga risasi commandoo mnategemea nini sasa😜!?
 
Kwa wasioweza kufungua video.
Fungueni na chrome.

Hawa askari wa serikali ya CCM wawajibishwe, wanashindwa kuua fisi mpaka risasi 49 watamuweza mtu ?🤣👇
 
kwa hiyo kwa akili zenu mnaamini mmemuua? roho huwa inauawa? fisi mtu ni spirit ya kishetani ambayo inaweza kujibadilisha kuwa chochote na haifi. kuna siku ataabuka tena huyo.
 
Fisi huyo aliyeua mtoto wa mwaka mmoja na nusu baada ya kuvamia nyumba katika Kijiji cha Kangeme wilayani Kaliua alijeruhi pia watu watatu ambao inaelezwa wanaendelea vizuri.

Diwani wa kata ya Zugimlole, Ramadhan Balikeka amesema kuwa wananchi waligawana nyama na haelewi walienda kufanya nini.

"Watu baada ya fisi kuuawa walidai watamshughulikia na kuchukua nyama huenda walienda kuila,"amesema.
Balikeka amesema kuwa tukio la fisi huyo na namna alivyokuwa mahiri kukwepa risasi, limehusishwa na imani za kishirikina, wananchi wakidai ni fisi wa aina yake.

Katika taarifa yake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo alisema kuwa fisi huyo alivamia kwenye nyumba katika kijiji hicho na kuua mtoto wa mwaka mmoja na nusu na kujeruhi watu watatu.

Pia aliongeza kuwa polisi na askari wanyamapori walimuua baada ya kutumia risasi arobaini na tisa.

Kwa mujibu wa Diwani Balikeka, tukio hilo la fisi ni la kwanza mwaka huu katika kata yake.

Chanzo: Mwananchi

View attachment 1871249
Watu baada ya fisi kuuawa walidai watamshughulikia na kuchukua nyama huenda walienda kuila,"amesema.
Balikeka amesema kuwa tukio la fisi huyo na namna alivyokuwa mahiri kukwepa risasi, limehusishwa na imani za kishirikina, wananchi wakidai ni fisi wa aina yake.

NAHITAJI SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA MENO YAKE TAFADHALI
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom