Fixed Deposits Account, UTT-Amis ni njia nzuri za kutunza pesa LAKINI SIYO uwekezaji abadani

Unakuja na kutoka.

Mil 12 kwa mwezi unapata how much UTT?
Kwa riba ya 12 % unapata like 1.4M kwa mwaka. Hizo pesa labda uwe umefungulia watoto kwa matumizi ya baadae otherwise Kama unataka kutoboa kwa UTT, unatoboa ukiwa dead already


hakuna tajiri aliyetajirika kwa kuweka pesa UTT au bank . Matajiri wote wanaenda kuchukua hizo pesa zenu na kuingiza kwenye mzunguko

Tatizo kubwa ni ngozi nyeusi haina nature ya biashara. Huwa tunalazimisha. Elimu ya biashara unaipata nyumbani kama ilivo kwa wahindi na wasomali. Why wanaweza ?
Ndio mana ngozi nyeusi tunachoma hela tukiingia kwa business. Business is for few not for many.

Kama umeajiriwa focus na ajira yako, business achana nayo tunza pesa yako

Business inahitaji guidance from the parents au uwe ni natural born business personal . But tambua biashara ndio inaleta matajiri dunian kote

Shida ni kujua codes , sometimes kujua codes inakuja na kupoteza hela then ndio unakuja kuelewa business ethics. Watoto wa kihindi na wasomali hizi codes wanazipata home ndio maana unaona kuna continuity .
 
Yaani uwe na uwezo wa kuweka fixed deposit au unayo 150 million halafu uanze kuendesha spacio kusomba abiria? Stupid. Why can't you find another lucrative business? Sasa dereva wa uber anakuwa afanye nininambaye hana hata mia?
 
Naomba na mm niweke neno kdg km nitaeleweka:-

1#. Fixed account and UTT amis ni vitu viwili tofauti na utofauti wake upo hapa fixed account haikuwi kithamani lkn UTT inakuwa kithaman kwa kupitia vipande maana bei za vipande zinaongezeka mfano ukinunua vipande vya 100M baada ya miaka mi3 hutauza kwa m100 itakuwa zaidi lakni bank fixed deposit km umeweka M100 utakuta hiyo hiyo 100M.

2#. Business and investment ni vitu viwili tofauti na kote unaweza kutoboa kutegemea na kiwango chako cha elimu ya fedha,uzoefu na risk appetite yako. Nije kwa mfano wako wa gari kupitia UTT gawio lako la mwezi unaweza kuchukua mkopo wa 15M kwa riba ya 13% kwa miaka mitatu makato hayazidi 500K montly hiyo ndio ufanyie izo mishe zako za abiria na utapiga hela vizur tu na sio kuchukua cash yako kununua gari (PROTECT YOUR CASH). Hapa narudia kusema biashara na investment zote zinalipa swali je ww ni muekezaji na mfanyabiashara mzuri?? Binafsi kuna investment nimefanya since 2016 niliweka 7M now nina more than 30M na zinazidi kukua so ni ww na financial inteligence yako.

3#.Kuna mdau mmoja kazungumza vizur sana katika uwekezaji wako hakikisha unatrade with protection tena hasa hasa capital protection kitendo cha kuweka hela UTT basi umeprotect mtaji wako na utaendelea kuwa nao siku zote, risk faida yako na sio mtaji wako.

4#. Mambo ya gari sijui itapigwa mzinga hizo ni mentality za kimasikini biashara yoyote hakikisha inakuwa full protected kupitia BIMA na mambo mengine ili kujilinda na majanga kama hayo.

5#. Bank kuna opportunity kibao na za maana zaidi ya fixed deposit cha msingi ni kuwa curious katika kutafuta maarifa na elimu nikupe mfano mambo ya mortgage kama unataka kujenga apartment zenye thamani ya 200M ww ukiweka 10% liqudity cash or collateral equivalent pamoja na kukamilisha requirements zengine Bank wanalend rest amount ambayo ni 90% ya 200M.

6#. Net profit ya 1.1M ni hela nyingi sana bila ya jasho tena nasema ni hela nyingi mno hasa ukijua kumaximuze hiyo hela hiyo hela unapata more than 40M loan ambayo unalipa kupitia montly payment yako.

7#. 1.1M net profit (Passive income) = 0.73% Montly gaining ya 150M WHILE Tsh elf 40 daily ni = 6.4% Monthly gaining ya 15M lakini sio NET PROFIT.

8#. Know your self ni mtu wa aina gani

Mwisho Sema hivi:-
fixed deposit and UTT amis ni njia nzur na kuhifadhi pesa lakini SIO UWEKEZAJI ABADAN KWANGU MIMI.

MCHAWI CALCULATOR (KIKOKOTOO)

Samahanini kwa usumbufu ingawaje nina mengi itoshe kuwasilisha hayo

Naomba na nipo tayari kurekebishwa na kupata maarifa zaidi
 
Nenda UTT

Ukiwa na hela nyingi like 100M ukaweka UTT utapata, 12 M kwa mwaka that is fine Kama unahifadhia watoto. Yaani mtoto anazaliwa leo then unamfungulia Ac ya UTT kwa principal ya 100M , by the time anafika 15 years anakuwa na (12M mara 15 years ) . Hii mbinu wanatumia wahindi sana ndio maana mtoto unasoma nae Udaktari mkimaliza anakuajiri au hukutani nae kwenye kuhangaika na Bahasha.

Muhindi au Msomali anasoma aje kukabhiwa ofisi, blacks tunasoma kuja kupambana na utumishi matokeo yake unafika 50 bado hujapata maisha.

Aidha kwenye Investment, kuweka hela UTT , it is the worst idea unless hujui anything about business .

Kama una Mil 100, unaenda kuwekeza UTT, I think unatakiwa kujitafakari, maana 100M kwa mwezi unapata 1.2 M plus na kodi unaweza Baki na 1M , hiyo ni ndogo sana kwa investment ya 100M .

Investment ya 100M kwa mwezi as profit unatakiwa usikose 7to 10M on monthly basis.

Shida kubwa kwa sisi black tunafanya business kwa kusoma articles na mitandao, unaenda ku invest hela.

Business ina codes zake na wala haihitaji mambo ya shule, just codes . Ndio maana hata layperson can do better in business akisha uncode
The codes .
Siwezi kumshauri mtu fanya business fulan kwa sababu business ni CODES and codes varies . The same business iliyokushinda mwingine inamlipa.

Mtu ana 30M za mkopo anenda kufungua business , in 12 months biashara imeshakufa na hela hizo kuja kuzipata tena ni ishu….. dhambi ya umasikini inatambaa

CODES . ndio mpango mzima

Hakuna tajiri anaetoboa kwa kuchimbia pesa chini au kuiweka FIX . By the time hiyo pesa inakupa faida, you will be dead already .asilimia kubwa wanaoweka pesa UTT ni wasataafu au watumishi; a bright mind and business oriented hawezi kulaza pesa UTT unless ni saving ya watoto.
 
Mkuu nimependa maelezo yako. Yana vitu vya kujifunza.

Unaweza kushare na sisi hiyo Investment uliyoifanya 2016 kwa 7M?
 
Nakubaliana na ww 100% kuhusu CODES maana kuna codes fulani nilipewa kuhusu biashara ya mchele nikaifanya tena kwa kujifunza nikaweka 2M now nina 4+m within a month tena trip moja tu nimefanya now ndio nataka nizame mazima
 
Mkuu usipangie watu maisha kila mtu ana motives zake mwingine peace of mind ndio mpango mzima na hizo pesa kwake anazopata riba kwa mwezi zinakidhi mahitaji yake na unaongelea matajiri unless hujui maana ya utajiri..., kwa mtu binafsi ambaye haishi maisha ya kupangiwa au kuangalia fulani anafanya nini....

Utajiri = Mahitaji yako yote bila kujinyima + Savings

To each their own....
 
Haya ndio naita kutaka kuweka mawazo yako kwenye maisha ya watu..., Kwahio kwa logic yako wote tukienda China then What ? (Nadhani wewe ndio unahitaji kujua msemo wa let your money work for you); Katika ulimwengu wote risk takers hawazidi 10% kwahio for their sake, safety na ustawi wa jamii low risk investments kwao ndio mpango mzima..., Waweze ku sustain their day to day life...,

Jamii yoyote iliyoshiba inahitaji middle incomes wengi wenye disposable income kuwa na matajiri wachache na masikini wa kutupa ndio unapata watu desparate kila wakipata senti wanatafuta high returns ndio wanaishia kudanganywa na Desi au na mtu kama wewe kwamba waende China na kuleta mzigo wa maana (badala kama taifa kuangalia ni lini wachina watakuja hapa kuchukua mzigo wa maana) Ni muendelezo wa kuwa wachuuzi na madalali from viongozi mpaka wananchi na sio practically tu bali mpaka mentally
 
Japo sikubaliani na kila ulilosema LAKINI bila doubt yoyote niseme wewe UNA AKILI KUBWA SANA. Nashukuru kwa mchango wako Captain.
 
Lengo ni kueleweshana na kipeana madini hebu twende kipengele kwa kipengele ili nijifunze zaidi wapi hukubalian ?? Ili tuelekekezane
Hapo #1. Utt inakuwa wakati FDA haikui. Labda ungepitia aina zote za mifuko ya UTT ungetambua kwamba mifuko hii inatofautiana na hivyo suala la kukua kwa vipande inategemea na aina ya mfuko. Kuna mifuko ambayo inaathiriwa na DSE na ile ambayo ni independent yaani haiathiriwi na DSE upande wa kukua positively au kukua negatively. Ukumbuke vipande vinaweza kupanda thamani au kushuka thamani kama mfuko unaathiriwa na DSE. Natumaini nitakuwa nimeeleweka.
 
Haya mawazo yako ya owoga wa maisha. Wewe Ni Mtanzania halisi, siyo risk taker. Ukweli unabaki pale pale kuweka hela fixed deposit siyo uwekezaji bali saving tu. Ukitaka uwekezaji hela lazima uizungushe ikiingize faida.
 
Umemaliza kila kitu hapo
 
Hapo ulikuwa unailinda hela yako na inflation ila sio uwekezaji huo chief...inflation kwa mwaka hii ha karibuni inaweza kuwa hata 15% hasa baada ya haya mambo ya Covid na vita za huko Duniani...mfano Mafuta yaliyokuwa yanauzwa 2200 sasa yanauzwa 3200

So milioni yako 150 unaeeza kuona imekuzalishia milioni 15 kwa mwaka kumbe ukiweka na inflation no hujapata kitu

Mimi biashara yangu ukiwekeza milioni 50 kwa mwaka unaondoka na million 100 au 150 mambo yakiwa vizuri, japokuwa risk za kuipoteza hats yote pia IPO kama usipokuwa makini
 
Yes nakubaliana na ww vipande vinapanda na kushuka but as investor angalia overall trend ni up or down jibu ni UP so if ni up why unawaza down while down inakuwa partial down then inaendelea up but all in all you are smart enough ukijpa muda zaidi na kujifunza zaidi naona your 150M soon will be worth of 1B within 15 years
 
M Mkuu sikupingi ,umefafanua vizuri
 
[emoji23][emoji23][emoji23] jamii forums projects business ideas...on paper
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…