Fixed Deposits Account, UTT-Amis ni njia nzuri za kutunza pesa LAKINI SIYO uwekezaji abadani

Tatizo unalinganisha vitu viwili vinavyoonekana kama vinafanana ila ni tofauti.
 
Mkuu hapo kwenye namba 6. Umesema kwa monthly payment ya 1.1M unaweza kupata mkopo wa zaidi ya 40M.

Naomba kuuliza:-
1. Ni bank gani wanatoa mkopo huo?
2. Huo mkopo utakuwa ni wa muda gani (Miaka mingapi)?

Asante.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Asante
Asante Sana

Jibu ni kama ifuatavyo:-

1#. Bank zote za Bongo
2#. kuanzia miaka 4

Karibu tena kwa ufafanuzi zaidi
 
Asante

Asante Sana

Jibu ni kama ifuatavyo:-

1#. Bank zote za Bongo
2#. kuanzia miaka 4

Karibu tena kwa ufafanuzi zaidi
Naomba niiweke kwenye hesabu:

Ukichukua mkopo wa 40M, bank (NMB) itataka ulipe 13% (Mkopo wa biashara) hii ina maana kwa mwaka utalipa 45.2M (40M * 1.13) . Ambayo ni sawa na 3,766,667M kwa mwezi.

Hiyo hiyo 40M kwa miaka 4 utatakiwa kulipa Approx 60M, ambayo ni sawa na 1.3M kwa mwezi.

Kwa payment ya 1.1M monthly hii bado haiwezi kucover mkopo wa 40M, ndio maana nikawa nimeuliza ni Bank gani unaweza kupata mkopo wa zaidi ya 40M?

N.B
Mwaka huu nilienda NMB wakaniambia Mkopo wa biashara huwa unakopeshwa kwa muda wa Maximum miaka 2. Kwa maana hiyo kwa mkopo wa 40M itatakiwa kurudisha 50.4M, ambayo ni sawa na 2.1M kwa mwezi.

Kama kuna sehemu nakosea naomba unieleweshe mkuu.

Asante

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Great thinker! Heko sana. Humu hua tunalishana matango pori sana. Ukiambiwa kitu ni vema kwenda kufanya research kwanza. Kuna mtu naona amelalamika mahali mwaka flan aliunguza mtaji wake zaidi ya 15m sababu tu ya kuchukua na kufanya business idea iliyowekwa humu kwa mahesabu yale ya kuvutia ya kupata faida.
 
Tunarudi palepale kwamba watanzania wengi hawajui tofauti ya business na investment so mtoa mada akajifunze utofauti kwanza ndio aje kuandika fikra zake hapa
 
Hapa kwenye ku-unlock code ndipo kisanga kilipo. Lakini ukivuka huo mtego unajikuta unateleza tu.
 
Shida kubwa watu mnalinganisha "active income" na "passive income"

UTT, fixed deposit, bonds, etc ni namna ya kupata passive income inayoongezea kwenye main income yako/active income.

Kwa mfano una business inayokuingizia faida kubwa mnazozitaja, lakini inakufanya uwe busy kiasi kwamba huwezi tena kuwa na business kubwa nyingine. Ile faida unayopata unaweka kwenye passive investments badala ya savings account.
 
dunia na sayansi na technology follow up ya business na monitoring imerahisishwa sana

You just need right investment and business codes . Huhitaji kutumia mabavu.
 
Tunarudi palepale kwamba watanzania wengi hawajui tofauti ya business na investment so mtoa mada akajifunze utofauti kwanza ndio aje kuandika fikra zake hapa

Sijajua taarifa zako unazipata wapi? Hivi unapata kwa wenye kufanya hizi biashara au unazipata vijiweni ?

Nakuambia tena kupitia bank unaweza kopa hadi miaka 7 kwa kutumia montly gawio la UTT hizi taarifa nakupa kwasababu mm ni mfanyaji hizi mambo so nakuomba endelea kufanya utafiti bank ya CRDB NA NMB hakikisha unakutana wahusika wa vitengo vya mikopo sio wale wa reception hawana shule wale na info zao sio za uhakika.

Kuna vitu sio vigumu ila mnavitia ugumu kwa uvivu wa kutafuta taarifa au mnakutana na watoa taarifa sio sahihi.

Karibu tena ndugu
 
Mkuu, hizo data nilizotoa ni data za mikopo ya NMB tena ukiwa unachukua mkopo wa biashara inakuaje unasema naleta story za vijiweni?.

Riba ya mkopo wa biashara wa NMB 13% kwa mwaka.

Je ukikopa 40M unatakiwa kurudisha bei gani?.

Ndio maana nikakuuliza ni bank gani ambayo unaweza kukopa zaidi ya 40M kwa kuwa na return ya 1.1M kwa mwezi?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Nakuunga mkono ndugu mtu anapata 1.1M net profit bila jasho tena umelala mguu juu halafu anakwambia ni hela kdg are serious???
 
Nar
Nenda CRDB urudi na mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…