Force Account inawamaliza mabosi wa Serikali, Waziri Mkuu anashuhudia madudu ya kutisha

Hebu tupatie composition ya hizi "kamati ya mradi".
Tuanzie hapo ili tuung'oe mzizi wa fitna.
 
Acha kuingiza uharo wako wa kisiasa katika mamba ya kitaalam.
Ujuzi mdogo ulio nao utumie kwa akilina hekima.
Construction philosophy, systems, methods na management zime evolve over hundreds of years na hazikuanza ninyi kupata videgree vya vyuo feki.
Leo nikikutaka utueleze kwa nini miradi ya SGR, Nyerere Hydropower-Stiegkers na mingine haijengwi ka Force Account, utabwabwaja hadi mtondogoo!
Level of thinking ikiishia kwenye bei ya kitasa, basi ujijue huna nafasi kichwani kufikiria construction methods and system.

Ni wale watu wajunga wajinga tu huwa wanafikiri mkandarasi is an end into construction methods and systems.
Huwa hamjui kuwa katika ujenzi vile vile kuna Designers/Architects, Quantity Surveyors, Design Engineers na katika usimamizi kuna Supervision Resident Engineers au Clerk of Works.
Hawa wote wanafanya azi ya kumsuoervise Mkandarasi.

Sasa mtu mjinga mjinga anaondoa hao wote anakuja na fundi Maiko na eti Kamati ya Mradi....!

Huu ujinga utaisha lini, ona sasa Waziri Mkuu inabidi tembelea miradi na TAKUKURU!
Tanzania is falling into stupidity before our eyes!
 
Asante sana kwa ufafanuzi.
Nchi hii itapona pale tu pale kitengo cha manunuzi na ugavi, procurement and supply unit, kitakaporejeshwa kwenye mikono safi ya wananchi.

Hiki kitengo, kinaitafuna nchi.
 
Kweli mkuu mbona hizi nyumba zetu zinajengwa na hao hao anaowaita fundi maiko na zina viwango. Ikiwa unampa fundi material za kiwango duni unategemea afanye miujiza jengo lipate ubora wa hali ya juu. Maana katika hali ya kawaida, hao maafisa hawawezi kuokota tu mtu mtaani ambaye hajui lolote kuhusu ujenzi akafanye ujenzi kwenye jengo la umma na bila kuwa na ukaguzi na usimamizi wowote, tuongee mambo in a balanced way. Inawezekana nyie makandarasi mliisababishia serikali changamoto ndo maana ikaanza kutumia hizi njia za force account ili mambo yaende haraka na kwa wakati badala ya kubaki na urasimu na upigaji wa wakandarasi huku miradi ikiwa haifanyiki au inachelewa kukamilika.​
 
We kweli bolizozo.
Hizo ni kamati za kisiasa au za kitaalam?
Na tuekele hasa, kamati ya miradi imesajiliwa na Bodi ipi ya kitaalam?
 
Kila kitu kipo kwenye BOQ, upigaji hapo labda wa 10% , mfano siment, bati, tofali, nondo, rangi, gypsum, tiles, bei zake zinajulikana kabisa hapo mtu anapigaje nje ya bei?
 

Kitendo cha CCM kupora chaguzi na kuua nguvu yaa wananchi kuhoji, haya ndio matokeo yake. Kwa sasa unakuta waziri mkuu anatembelea miradi anakuta Madudu, anachukua hatua yeye wakati taasisi zote za usimamizi zipo. Na watu wanamchora tu maana wanajua hata yeye yuko madarakani kwa wizi wa kura. Viongozi wakianza kuingia madarakani kwa njia halali, wengine wa chini watafuata sheria na kuwa waadilifu.
 
We kweli bolizozo.
Hizo ni kamati za kisiasa au za kitaalam?
Na tuekele hasa, kamati ya miradi imesajiliwa na Bodi ipi ya kitaalam?
Hujitambui...

Kamati ya Ujenzi katibu wake ni ENGINEER na kama ni NGAZI ya vituo vya kutolea huduma basi ENGINEER ni mshauri na anawaongoza!!!

Manunuzi kadhalika!!!!

Hawa watu wamesajiliwa na bodi zao
 
Reactions: Cyb
Sahihi kabisa!!!

Leo tuna miradi mingapi ilijengwa na WAKANDARASI na haina kiwango??? Au gharama zake ni za juu sana?

Uhakika ni kuwa ipo mingi sana...
 
Reactions: Cyb

Issue ni UNAONGEA kishabiki....

ndiyo maana watu kama wewe hujiona wasomi kumbe practically umebeba THEORIES ambazo huwezi kuzitumia kwenye UHALISIA!!!

KASOME mwongozo wa UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA NJIA YA FORCE ACCOUNT WA PPRA...

Utaelewa ili PROCURING ENTITY IWE QUALIFIED KUTEKELEZA MIRADI KWA NJIA YA FORCE ACCOUNT inatakiwa kuwa na sifa ZIPI???

Tujifunze kusoma kabla ya kubwabwaja. UKISHASOMA HUO MWONGOZO NDIYO UJE UTOE HOJA HAPA
 
Hujitambui...

Kamati ya Ujenzi katibu wake ni ENGINEER na kama ni NGAZI ya vituo vya kutolea huduma basi ENGINEER ni mshauri na anawaongoza!!!

Manunuzi kadhalika!!!!

Hawa watu wamesajiliwa na bodi zao
Kawaida yenu kuingiza wanasiasa kwenye miradi ili mpate uhalali wa kupora.
Katibu wa kamati ya Miradi ni Enginee? au siyo.
Una maana wale ma Engineer wa Halmashauri ambao ni clerical engineer?
Kwa taarifa yako hakuna maengineer wanaodharaulika katika fani hii ya ujenzi kama hao clerical engineers wa Halmashauri, wanao endeshwa na madiwani kwa faida ya ulaji.

Inaelekea hata swali langu hukulielewa maana yake.
Kwa hiyo kwenye hiyo Kamati ya Mradi, hawa ma Clerical Engineers wenu wanasajiliwa kama Engineers wa mradi?
Kama ni muelewa wa miradi utalijibu hili kwa ufasaha.
Halafu baada ya hapo tupe majukumu ya rchitect na Design ngineers hapo wanaingiaje.
 
 
Nyie manguini mnamatatizo sana.
Force Account ni kwa ajili ya miradi midogo sana na mainly repair na maintainance oriented.
Mmeamua kula fedha za wananchi na kumwaga fedha kwa mabilioni ati kumtumia fundi Maiko.
Umeulizwa hapo nyuma kuwa hiyo system yenu Force Acccount inayotumiwa kijinga, mbona hamuitumii kujenga SGR?
 
Nchi hii ina tatizo la usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya serikali.

Tatizo la msingi ni viongozi na watendaji tulionao katika nafasi mbalimbali za umma .

Tabia ya kupeana vyeo, na ajira kiudugu na kimchongo na kuwapa ujira mdogo huku ukiwapa wajibu wa kusimamia miradi ya mamilioni ya pesa . Hapa ndo anguko la taifa linaanzia.

Njaa ni Kali sana kwa maofisa na watendaji wa serikali - hivyo inakua ngumu sana sana kukwepa mtego wa rushwa na wizi.

Ili tufike mbali Iko haja ya kubadiri mfumo wa utumishi wa umma na taratibu za usimamizi miradi ya umma
 
Nakuunga mkono mkuu. Kama tukiwa wazalendo kweli huu mfumo ni mzuri na unatufaa sana kama siasa ikiwekwa kando na uzalendo kutangulizwa. Pia kufanyia mayoress vitu vidogo vidogo
 
Halafu anatokea mtu mjinga wa kiasi, anatetea miradi kusimamiwa na wanasiasa.
Inakera.
By the way mbona Bodi za serikali, zenye watu weledi ziko kimya juu ya hili swala.
Kuna NCC -National Construction Council
ERB -Engineers Registration Board
AQRB -Architects and Quantity Surveyors Registration Board
CRB -Contractors Registration Board

Wizara ya Ujenzi na Bodi hizi ziko kimya utafikiri hazipo.
Kazi ya TAKUKURU ilipaswa ifanywe na Bodi hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…