Force Account inawamaliza mabosi wa Serikali, Waziri Mkuu anashuhudia madudu ya kutisha

Nakuunga mkono mkuu. Kama tukiwa wazalendo kweli huu mfumo ni mzuri na unatufaa sana kama siasa ikiwekwa kando na uzalendo kutangulizwa. Pia kufanyia mayoress vitu vidogo vidogo
I mean maboresho
 
Kuna mwamba mmoja alizungumza bungeni,kizazi chote hiki tokea kiko primary school kinawaza,nikimaliza masomo yangu tu nikaajiriwa lazima nipige hela,sasa ili uweze kushinda hili ni lazima utafute mbadala wa kufuta hii mindset,hapo ndio sijui wanafanyaje...
 
Yawezekana tatizo la wizi sio kubwa kama watu wanavyotaka kuliweka kuwa miradi inayotekelezwa na mfumo wa force account kuna wizi mkubwa kuliko mfumo wa kutumia wakandarasi.
Ukweli ni kwamba Force account imepunguza/imeokoa gharama kubwa za ujenzi, kabla ya force account hakuna mkandarasi aliyekuwa anajenga darasa moja kwa milioni ishirini, hakuna mkandarasi anayeweza jenga bweni kwa milioni sabin na tano.
Yawekana tatizo ni gharama za ujenzi kupanda kulinganisha na fedha zinazotolewa kukamilisha miradi, ni ngumu kukamilisha bweni kwa asilimia 100 kwa milioni sabin na tano. Mtu anayejenga Sumbawanga gharama zake haziwezi kuwa sawa na wa Kinondoni lakini fedha za ujenzi wa madarasa zinatolewa sawa.
 
Mkuu uelwa wako wa fani hii ya ujenzi, kama walivyo wanasiasa wengi, ni mdogo sana.
Kazi ya ujenzi si mkandarasi peke yake anayeweza kuathiri gharama za ujenzi.

Ni wale wasiojua tu ndio utawaona wakikazana kumtazama mkandarasi badala ya kuitazama Team nzima ya Client, Architect/Designer, Engineer, Quantity Surveyors, Supervision Staff na wataalam wengine.

Ndiyo maana watu kama ninyi mnaulizwa kwanini mstitekeleza miradi mikubwa kama ya SGR na Bwawa la Mwalimu Nyerere, mnaaza kuhesabu nyote za mbiguni!!
 
Hujaeleewa my point, najua kwenye ujenzi kuna QS , Architec etc.. ninacchokwambia tatizo la kutomalizika kwa miradi mingi iliyotekelezwa kwa njia ya force account kama madarasa, mabweni etc ni upungufu wa fedha zinazotolewa compared to BOQ. Hakuna QS anayeweza kutengeneza BOQ ya ujenzi wa bweni linalochukua wanafunzi 80 kwa shilingi milioni sabini na tano, hata angepewa nani hawezi.
 
Ulaji mwingine wamesogezewa hao wanaoambia KAMATA HAO
Yaani nchi inakatwa vipande vipande na haviungiki tu
 
Ulaji mwingine wamesogezewa hao wanaoambia KAMATA HAO
Yaani nchi inakatwa vipande vipande na haviungiki tu
Exactly.
Thats the point.
Force Account inaingia kwenye unregualted area kiusimamizi.
Kamati za Ulinzi na Usakama sasa zinasimamia ujenzi, na hizo kamati za Miradi sijui core function zake ni nini.

Badala ya usimamizi kufanya na wataalam waliosajiliwa, sasa kazi inasimamiwa na kamati za kisiasa, na hela inapigwa kihalali.
 
Hapo kwa kib
Asante sana kwa ufafanuzi.
Nchi hii itapona pale tu pale kitengo cha manunuzi na ugavi, procurement and supply unit, kitakaporejeshwa kwenye mikono safi ya wananchi.

Hiki kitengo, kinaitafuna nchi.
. Muu I mada mbili tofauti. Hapa tuna force account
 
. MKuu hakuna nafuu. Vitu vingi viko substandard, hapo ni hesabu ya materials na fundi tu. Key staff wote pamoja na cost za usafiri zinatoka serikalini/municipal. Hakuna kodi hapo (withholding tax) wala VAT.
So hakuna nafuu yoyote vs mkandarasi. Pia ina negative effects kwenye uchumi wa inchi kwani pesa inazunguka within a narrow circle.
 
Maria
Utaachaje kujadili Force Account bila kutaja Procuring entities alizotaja Ndugu Maria Nyedetse ? Hapa ni muhimu kuitazama mada kwa jicho la tatu Mkuu.

Karibu.
Maria analeta vitu tofauti. Hoja kubwa hapa ni force account imevuka malengo yake ya kuanzishwa
 
Force Account bila kuwa na system ya kufanya checks Ni kazi bure,kwanza majengo mengi hayakidhi viwango vya ubora..

Mwisho hasara kubwa ya force Account Serikali haipati Kodi
 
Unaonyesha tatizo kwa kusingia msingi wa tatizo na sio suluhisho la tatizo.... Yaani solution yako ni kubadilisha walaji na sio kuzuia ulaji
 
Hapo ndipo mleta mada anapohoji yaani darasa litakalojengwa Wilaya ya Tanganyika liwe na cost sawa na darasa litakalojengwa Mchikichini Wilaya ya Ilala? Nabado watetezi wa force account wanaona iko sawa tu
 
Force account sio mbaya mradi mingi imetekelezwa vizuri sana,wanakula ila sio sana kama nyie
 
Maria

Maria analeta vitu tofauti. Hoja kubwa hapa ni force account imevuka malengo yake ya kuanzishwa
Point ya Maria anasema Force Account haina matatizo, matatizo yapo kwenye procuring entities ambazo ni kiungo muhimu katika kusimamia account hiyo Pamoja na wasimamizi wanaotumia Force Account kutekeleza miradi.
Kwa muhitasari, nimemuelewa hivyo Maria.
 
Nyie vichwa wazi mnashauriwa mkajenge SGR kwa force akaunti, mnajishaua hapa.
 
Hii ni mbinu ilitengenezwa ya kuchepusha fedha za Serikali na viongozi wetu wakapelekewa uongo kwamba eti miradi inajengwa kwa gharama nafuuu kumbe ni chain ilitengenezwa ya ulaji na mwisho wa siku akosekane wa kuwajibika moja kwa moja kila mmoja anamsingizia mwenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…