Forex: Sandile Shezi kutoka South Africa kawapiga na kitu kizito wanafunzi wake yeye huyo Asia

Forex haitaki vilaza. Ukiwa kilaza, vilaza waliochangamka watakutumia kama fursa yao ya kutoboa kimaisha.

Forex inataka watu wenye akili. Na watu wanaojishughulisha kwa bidii. Inataka watu ambao watalala masaa yasiozidi matano. Inataka watu ambao wataachana na mambo ya kufuatilia umbea, kuangalia tamthilia na vitu vyote ambavyo sio muhimu na huo muda autumie kwenye hiyo biashara ya forex.

Sasa mtu genge tu unashindwa kuliendesha mtaji unakufa halafu unataka ufanye forex?

Masaa yote upo insta umbea, ukitoka unaingia tiktok, ukitoka unakuja Jf ukimaliza hapo unaenda whatsap kupost memes halafu ukishachoka ndio unaenda sasa kuangalia
Candlesticks?
 
Kuna Mtu alinishawishiii mweee....ila MUNGU tu nikachomoa juu Kwa juu..kwanza sikua na Hela ya mchezo miye!!!
Mimi mwenyewe kuna mshkaj wangu alishawahi nipanga kuwa ana maisha na nyumba ameshajenga kwa sababu ya forex, kumbe anaishi kwa kaka ake chumba kimoja na kazi yake kubwa ni utapeli ukijichanganya tu umeliwa.
 
Sikiliza, hapa Duniani hakuna mtu aliyetoboa bila kufanya biashara, ila zisiwe hizo za kudownload pesa, kama wewe si tajiri wa Kutupwa basi Achana nazo, ssbabu ukipotea ndio umekwisha.

Soma kupata title tu, ila mwishowe fungua biashara.
 
Kumbe ndo huyu Ontario wa South Africa?
 
Sawa Genious tajiri.
 
Sikiliza, hapa Duniani hakuna mtu aliyetoboa bila kufanya biashara, ila zisiwe hizo za kudownload pesa, kama wewe si tajiri wa Kutupwa basi Achana nazo, ssbabu ukipotea ndio umekwisha.

Soma kupata title tu, ila mwishowe fungua biashara.
Lakini kufuanya Biashara huwezi kufuanya bila mtaji inabidi uutafute kwanza huo mtaji MO tiali anao vijana hawana hizo ndio njia wanazofanya kutafuta huo mtaji
 
Damn what a reply!
Hannah do you do any kind of investment? I mean digital investment
 
forex aisee ipo njema tu kwasababu nina jamaa yangu amefanikiwa mpaka sasa japo nae ana ups and down nyingi najua ndio maisha kuna mda anaishiwa kabisa japo kuna mda anapiga pesa sana niliwai kuwekeza kwake 2.5M na ikarudi na faida japo nilivumilia vingi sana
 
Sikiliza, hapa Duniani hakuna mtu aliyetoboa bila kufanya biashara, ila zisiwe hizo za kudownload pesa, kama wewe si tajiri wa Kutupwa basi Achana nazo, ssbabu ukipotea ndio umekwisha.

Soma kupata title tu, ila mwishowe fungua biashara.
Ndomaana nimewaasa vijana wafanye biashara ambayo wanaweza control mitaji yao ila sio forex
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…