Forex: Sandile Shezi kutoka South Africa kawapiga na kitu kizito wanafunzi wake yeye huyo Asia

Mwaka 2017 May ni mdau niliye shawishika sana kujiunga na jamii forum, kabla ya hapo nilikuwa nasoma tu na kupita hivi na sikuwa member. Ikaja thread moja kutoka kwa kijana machachali ontario kuhusu forex nikasoma na nikashawishika sana, kwa kipindi hicho nilikuwa mwa watatu chuo so kuna course moja tulio soma BAF inaitwa international trade ndani yake kuna forex, so haikuwa ngumu kwangu haikuwa ngumu sana kuelewana na ONTARIO.

Moja ya mifano aliyoitajija Ontario ni kijana huyu sandile shezi kutika south africa nikamfuatilia sana, nikaona interview zake alivyo acha chuo nakujiunga na forex na kutoboa kichwani mwangu moto uliwaka zaidi nikaona maisha si haya naenda kuyapatia

Nikajikita kusoma na kufungua demo account kama njia ya kujifunza pia nikawa mdau sana wakusoma vitabu vya kiyosaki, trump n.k hivi na soma hadi leo. Nikajiunga na magroup ya whatsapp na telegram nikawa member wa Ontario si unajua tena pesa ndugu zangu. Sikuwai kufungua real account cos nilikuwa na maisha yakuunga unga sana baada ya kumaliza chuo nikaona ngoja nijipe muda, nikaanza kuona wadau wanaanza kulia kuhusu Ontario kengere ikagonga kichwani nikabidi niwe ndugu mtazamaji tu. Nikaja jifunza kwa Robert kiyosaki usingie kwenye biashara ambayo hauwezi ku-control mtaji wako hasa forex hata kama biashara ina uhalisia ukiona hauwezi control capital tako achana nayo kupoteza ni dakika sifuli toka hapo nikapiga chini.

Sasa kijana huyu kutoka south anatafutwa na polisi na inasemakana ameitelekiza familia yake na hajulikani alipo na amekimbia na pesa za watu.

Ndugu zangu wana chuo hakuna pesa ya haraka haraka maisha ni mapambano leo ni mwaka sita toka nimalize chuo hata tobo bado sijalipata na BAF yangu, sio kwamba kichwani ni mweupe kwenye caree yangu najua sana cos huwa na zifungia kampuni binafsi mahesabu na kuwasaidi kwenye masula ya kodi TRA

NOTE: Vijana someni someni shule ndo mkombozi achana na forex japokuwa ni biashara halali ila usijingize kuendesha maisha yako itakuletea matatizo , muda unatumia kujifunza forex kajifunze kutengeza bajaji/ pikipiki na carpenter huku unasubilia ajira kutoka kwa government

Kuna ka kikundi kingine kama mr kuku, best capital, tapaia vyote hivyo ni vikundi vya matapeli. Ukiona mtu anafikiria kuwafanya wanachuo watajirike au watu wa kawaida watajirike huyo ni tapeli, kazi/ubunifu ndiyo huleta maisha mazuri
 
Forex is gambling
Huw na waambia watu hvyo

Mwaka jana imeumiz $700+[emoji35][emoji35][emoji856][emoji48][emoji81][emoji81]
Sio kweli, ila wewe ndio ulikuwa unafanya kama gamling na hakutaka kujifunza kupitia hiyo loss..

Nimekuwa kwenye forex zaidi ya 7 years najifunza kila siku makosa yangu , kila position nayofungua kwangu ni darasa.. nimepata loss nyingi sana na nimejifunza sana..

Mtu anacheza forex badala ya trading forex 😅😅😅😅 lazima upasuke
 
Forex haitaki vilaza. Ukiwa kilaza, vilaza waliochangamka watakutumia kama fursa yao ya kutoboa kimaisha.

Forex inataka watu wenye akili. Na watu wanaojishughulisha kwa bidii. Inataka watu ambao watalala masaa yasiozidi matano. Inataka watu ambao wataachana na mambo ya kufuatilia umbea, kuangalia tamthilia na vitu vyote ambavyo sio muhimu na huo muda autumie kwenye hiyo biashara ya forex.

Sasa mtu genge tu unashindwa kuliendesha mtaji unakufa halafu unataka ufanye forex?

Masaa yote upo insta umbea, ukitoka unaingia tiktok, ukitoka unakuja Jf ukimaliza hapo unaenda whatsap kupost memes halafu ukishachoka ndio unaenda sasa kuangalia
Candlesticks?

Kifupi uwe mtumwa sio? There's more to life than utumwa. Unaweza weka muda wako wote kwenye forex na most likely bado utaliwa kichwa. Yuko wapi ONTARIO au huyu Shonzi, unadhani hawakuweka muda enough kwenye forex?

Forex ni kamari na 'the house wins almost always' if you know what I mean.

Nakusanua, wote wanaotoboa kwenye forex hawapati hela kwa kufanya forex trading bali kwa kwa kufanya training au kuwalaghai maboya kwamba watafanya trading on their behalf.

Mwisho, biashara yeyote ambayo unaambiwa utapata return zaidi ya 10% kwa mwaka jua fika ni uongo. Either sio halali au wanakutengenezea mazingira wakupige.
 
Kwanini unaita utumwa?
Ili uwe daktari inabidi uingie darasani na usome miaka 4 au mitano right? Na ili ufanye vizuri inabidi usome hadi ukose muda wa kulala (hapa inategemea na wepesi wako wa kuelewa). Utapata muda wa kushinda mitandaoni kupiga umbea? No. Huo muda utatumia kutafuta useful materials kwa ajili ya unachokipigania.

Ili uwe mhasibu inabidi pia uingie darasani usome na ujinyime, uwekeze muda wako huko kwa miaka kadhaa ufanye na mitihani ufaulu au ufeli urudie ndio uwe mhasibu!

Sasa kwa nini ikija kwenye forex ukiambiwa wekeza muda wako soma unaona ni utumwa?

Ni biashara gani ambayo aihitaji kuwekeza muda wako? Kufuga mbuzi? Hapa napo bado inabidi uwekeze muda wako usome ufugaji na changamoto zake.

Pili. Unaposema kutoboa kwenye forex unamaanisha mtu kuwa tajiri? Kama ni hivo badili huo mtazamo kwa sababu sio kila biashara anayofanya mtu anakuwa tajiri. Utapata hela ya kukuendeshea maisha yako ya kila siku ila ukiwa umebahatika zaidi unaweza kuwa tajiri.

Usifanye biashara yoyote kwa lengo la kutoboa kimaisha wewe fanya kwa lengo la kuendesha maisha yako.

Mfano vunjabei. Ni biashara ngapi zinafanana na zake na wanaozifanya sio matajiri wala hawana majina? Lakini kafanya vunjabei kapata jina. Sasa ina maana hao wanaofanya biashara za hivo na hawajatoboa hizo biashara ni scam?
 
wasouth weusi wote nilishawadharau huwa naona kama ni failures kwenye maisha, tangu waonekane wavivu na kuua waafrica wenzao waliowapigania, hata mtu akijifanya kufanikiwa au nikisikia kiingereza cha south tu mtu huyo huwa namweka kapu moja na failures kwenye maisha na watu wasio na shukran.
 
Kwanini unaita utumwa?
Ili uwe daktari inabidi uingie darasani na usome miaka 4 au mitano right? Na ili ufanye vizuri inabidi usome hadi ukose muda wa kulala (hapa inategemea na wepesi wako wa kuelewa). Utapata muda wa kushinda mitandaoni kupiga umbea? No. Huo muda utatumia kutafuta useful materials kwa ajili ya unachokipigania.

Ili uwe mhasibu inabidi pia uingie darasani usome na ujinyime, uwekeze muda wako huko kwa miaka kadhaa ufanye na mitihani ufaulu au ufeli urudie ndio uwe mhasibu!

Sasa kwa nini ikija kwenye forex ukiambiwa wekeza muda wako soma unaona ni utumwa?

Ni biashara gani ambayo aihitaji kuwekeza muda wako? Kufuga mbuzi? Hapa napo bado inabidi uwekeze muda wako usome ufugaji na changamoto zake.

Pili. Unaposema kutoboa kwenye forex unamaanisha mtu kuwa tajiri? Kama ni hivo badili huo mtazamo kwa sababu sio kila biashara anayofanya mtu anakuwa tajiri. Utapata hela ya kukuendeshea maisha yako ya kila siku ila ukiwa umebahatika zaidi unaweza kuwa tajiri.

Usifanye biashara yoyote kwa lengo la kutoboa kimaisha wewe fanya kwa lengo la kuendesha maisha yako.

Mfano vunjabei. Ni biashara ngapi zinafanana na zake na wanaozifanya sio matajiri wala hawana majina? Lakini kafanya vunjabei kapata jina. Sasa ina maana hao wanaofanya biashara za hivo na hawajatoboa hizo biashara ni scam?

Mkuu, there's a big difference kati ya professions kama udaktari, uuzaji duka na forex. Udaktari au kada zingine ukiweka juhudi na maarifa utafanikiwa tu.

Forex trading, on the other hand, is a get-rich-quick scheme. Hiii ndo ahadi ya forex. Weka hela kuwa billionaire overnight. Jambo ambalo haliwezekani.

Unlike kada zingine, unaweza weka muda na maarifa yako yote kwenye forex na bado ukafeli. Hivi unajua 95% ya watu wanaofanya forex trading duniani wanapoteza hela? That's a fact. Ni kada gani ina failure rate kubwa kiasi hicho? Unataka kusema hao wote hawajui nini wanafanya? Case in point, ONTARIO muasisi wa forex bongo, kaishia wapi? where did he go wrong kwa mtazamo wako?

Jisomee mwenyewe hapa chini na links nimeweka:

A well-known figure in the Forex world is that 90% of Forex retail traders do not succeed. Some publications quote failure rates as high as 95%.

Statistics show that most aspiring forex traders fail, and some even lose large amounts of money.

Ndio maana nakwambia hizo data wanazosema juu ya forex kuhusu kufanikiwa ni mtu kuwa tajiri”. Kutajirika kupitia forex.

Lakini sio lazima uwe tajiri ukiweza kupata ya kukuendeshea maisha yako ya kila siku inatosha. Duniani si kila mtu anatakiwa awe tajiri.

Na hiyo asilimia 5 au 10 ya wanaofanikiwa kuwa matajiri bado ni ushahidi kwamba inawezekana ukiweka enegy and that has to be you.

Watu waelewa wameshaachana na dhana ya kuwa matajiri kupitia forex. Wanafanya kuendesha maisha yao kama biashara nyingine.

Kuhusu Ontario sijui lakini failure ya muasisi haimaanishi kwamba hicho kitu hakifanyi vizuri. Yeye ni binadamu tu.
 
Hiyo ni figure ya watu wanaofeli kabisa sio kuwa matajiri. 95% wanapoteza kabisa hela zao sio kuwa matajiri au kuendesha maisha yani hawapati kitu wanapoteza hata kile walichoweka.
 
Ukiweza kuishinda tamaa na kubali kuingiza asilimia ndogo utafurahi kwenye forex.

Njee ya hapo hata usome vitabu zaidi ya million 1 na uwekeze muda wako wote 24 hours utaishia kupoteza pesa bora kufanya biashara zingine hata kuuza karanga.
 
Hiyo ni figure ya watu wanaofeli kabisa sio kuwa matajiri. 95% wanapoteza kabisa hela zao sio kuwa matajiri au kuendesha maisha yani hawapati kitu wanapoteza hata kile walichoweka.

Sawa mkuu.
Ngoja nikimalizana na ujana na takataka zote nikitulia nijifunze. Nitakuletea mrejesho au sio?
 
Uwe unaelewa nimesema kuzaliwa na ku Africa sijajichagua mimi ila nature, nimejikuta nipo africa so shule sio kwamba inakufanya kuwa na pesa hata ukombozi wa fikla tu
sisi wengi shule imetufikisha hapa tulipo tunaoneka bora kwenye jamii na familia kwa sababu ya shule
Wote hatuwezi kuwa wakina vunja bei
Yani hayo maneno "ukombozi wa fikra" nimeanza kuyasikia siku nyingi kweli ila hayana impact chanya yoyote.

Tanzania ukisoma sana unaishia kuwa mwizi, usiposoma unakuwa fukara wa kutupwa! Na ukisoma kidogo unapata kakibarua!

Hapo ulipo unahimiza watoto wasome ilihali wewe huna unachonufaika na kusoma kwako, himiza watu kusaka hela TU wawe matajiri
 
Forex haitaki vilaza. Ukiwa kilaza, vilaza waliochangamka watakutumia kama fursa yao ya kutoboa kimaisha.

Forex inataka watu wenye akili. Na watu wanaojishughulisha kwa bidii. Inataka watu ambao watalala masaa yasiozidi matano. Inataka watu ambao wataachana na mambo ya kufuatilia umbea, kuangalia tamthilia na vitu vyote ambavyo sio muhimu na huo muda autumie kwenye hiyo biashara ya forex.

Sasa mtu genge tu unashindwa kuliendesha mtaji unakufa halafu unataka ufanye forex?

Masaa yote upo insta umbea, ukitoka unaingia tiktok, ukitoka unakuja Jf ukimaliza hapo unaenda whatsap kupost memes halafu ukishachoka ndio unaenda sasa kuangalia
Candlesticks?
Na kweli dear Mimi na uvivu huu nshafeli
 
Back
Top Bottom